
- FT: Simba SC 6-1 Mashujaa FC NBC Premier League, Uwanja wa Uhuru, Oktoba 13,2026
- Ellie Mpanzu amefunga mabao mawili na kuchaguliwa kuwa Man of The Match
- Seleman Bwenzi wa Mashujaa FC amefunga bao dakika ya 63 akitibua rekodi ya hati safi kwa mlinda mlango Kassali
- Makala hii inachambua kwa ufupi matukio muhimu ‘highlights’ za mchezo huu.
Simba SC 6-1 Mashujaa FC ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier uliochezwa Uwanja wa Uhuru Oktoba 13,2026. Mabao ya Simba SC yamefungwa na Libase Gueye dakika ya 16 kwa asisti Neo Maema, Ellie Mpanzu dakika ya 33 na 58 Oura dakika ya 52, Abraham Morice dakika ya 61 na Ismail dakika ya 68.Ellie Mpanzu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Mashujaa FC walipachika bao dakika ya 63 kupitia kwa Seleman Bwenzi.Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa ndani ya NBC Premier League 2026/27 kwa Simba SC.Simba SC inafikisha mchezo wa 8 bila kufungwa chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker inaongoza ligi ikiwa na pointi 24.
SOMA HII PIA:Simba SC 2-1 Yanga SC Kariakoo Dabi 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mpaka milioni 800 ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.Rubani huku mkwanja upo wakutosha unakusubiri.Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC 6-1 Mashujaa FC yamefungwa mabao makali
Wakati ubao ukisoma Simba SC 6-1 Mashujaa FC yamefungwa mabao makali ndani ya uwanja. Miongoni mwa hayo ni lile la Gueye akitumia pasi ya Maema. Mashujaa FC kupitia kwa Bwenzi aliyeanzia benchi ameonyesha uwezo wake akitibua rekodi ya Kassali kupata hati safi.
Takwimu za dakika 45 kipindi cha pili
Simba SC walifanya mabadiliko kipindi cha pili ambapo Maema alikwenda nje nafasi yake ilichukuliwa na Abraham Morice.Ibrahim Doumbia aliingia akichukua nafasi ya Ellie Mpanzu, Ismail Mgunda aliingia akichukua nafasi ya Clatous Chama na Makglwa aliingia akichukua nafasi ya Libase Gueye.
Mashujaa FC ni Michael alitoka nafasi yake ikachukuliwa na Mishano dakika 45. Nyota Samson Madeleke alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 75.
Takwimu za dakika 45 za mwanzo
Kwenye dakika 45 za mwanzo ubao wa Uwanja wa Uhuru ulikuwa unasoma Simba SC 2-0 Mashujaa FC. Mabao ya Simba SC yalipachikwa na Libase Gueye dakika ya 16 akitumia pasi ya Neo Maema na Ellie Mpanzu alifunga bao la pili dakika ya 33.
Hassan Dilunga nyota wa Mashujaa FC alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 45 baada ya kumchezea faulo Anthony Mligo.Mpoki Mwakinyuke alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 30 alimchezea faulo Ibrahim Jabaar.
Simba SC vs Mashujaa FC vikosi vilivyoanza
Kikosi cha Simba SC: Mahamadou Kassali, Nathaniel Chilambo, Libasse Gueye, Anthony Mligo, Ibraheem Jabaar,Ellie Mpanzu, Clatous Chama, Neo Maema, Yusuph Kagoma, Ismael Toure na Anicet Oura.
Wachezaji wa akiba ni Kibabage, Semfuko Daud, Bakari Seleman, Kaletso Makgalwa, Duchu, Ibrahim Nindi, Morice Abraham, Hussen Abel, Ibrahim Doumbia na Ismail Mgunda.
Kikosi cha Mashujaa FC: Mussa Malika, Abdulajid Mangalo, Haroun Lyawatwa, Crispin Ngushi, Mgandila Shaban, Mpoki Mwakinyuke, Hijja Shamte, Tariq Simba, Samson Madeleke, Hassan Kabunda na Michael Joseph.
Wachezaji wa akiba ni Haruni Chanongo, Abdallah Mfuko, Salum Kihimbwa, Mapinduzi Balama, Yusuph Ruben, Mundhir Vuai, Lameck Kanyonga, Mishamo Daud, Juma Mahadhi na Seleman Bwenzi.
SOMA HII PIA:Simba SC 2-0 Mashujaa FC Ligi Kuu Bara NBC: Mnyama afufuka! Highlits,Matokeo, Ratiba
Hitimisho
Simba SC 6-1 Mashujaa FC mwendelezo wa ushindi katika Uwanja wa Uhuru. Mechi imekusanya mabao 7 na pointi 3 zikibaki kwa mnyama. Unakuwa mchezo wa 8 kwenye ligi Simba SC inaendeleza rekodi yakutopoteza.

