- Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27 Uwanja wa Airtel
- Clatous Chama mfungaji wa bao la kwanza Simba SC amechaguliwa kuwa Man of the Match
- Anthony Mligo beki wa unyamani ameonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 84
Mchezo umakamilika Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27. Ni mchezo wa tatu mnyama anashinda ugenini akikusanya pointi 9 akiwa anaongoza ligi. Mabao yamefungwa na Shekhan Ibrahim kwa Singida Black Stars dakika ya 23, Clatous Chama dakika ya 11 na De Reuck dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.
Ijue ratiba ya Simba SC: Ratiba ya Simba SC mwezi huu wa 6, 2026 | Ligi Kuu NBC na CRDB Federation Cup, Takwimu |Mechi 6 za kufa na kupona | SportPesa Blog

FT: Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27 taarifa muhimu

Doumbia alifunga mechi hii: Simba SC 2-1 Singida Black Stars Kagame Cup 2026 hatua ya makundi wametoana | Doumbia afungua akaunti ya mabao | SportPesa Cup
Matokeo: Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27
Uwanja: Airtel
Siku: Agosti 22, 2026
Mwamuzi: Ally Mnyupe
Kadi nyekundu: Anthony Mligo wa Simba SC dakika ya 84
Man of the match: Clatous Chama
Orodha ya wachezaji walioonyeshwa kadi za njano
Nyota wa Singida Black Stars watatu wameonyeshwa kadi ya njano. Ni Jeancy Mboma dakika ya 32, Jonathan Sowah dakika ya 50. Ibrahim Imoro dakika ya 52.
Simba SC na kadi nyekundu 2026/27
Mfumo mpya wa teknolojia ya FVS, (Football Video Support) ni mwiba kwa mnyama. Katika mechi 3 mfululizo wamekuwa wakimaliza pungufu kwa adhabu ya kadi nyekundu. David Kameta alianza kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar. Ibraheem Jabeer alifuata mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC. Mchezaji wa 3 ni Anthony Mligo mchezo dhidi ya Singida Black Stars.
Duchu maamuzi yalifanyika baada ya marejeo ya FVS kama ilivyotokea kwa Mligo. Ni rekodi mbovu ambayo imeandikwa kwa wachezaji wa unyamani. Nyota hawa watakosekana katika mchezo ujao wa Simba SC.
Hitimisho
Singida Black Stars 1-2 Simba SC Ligi Kuu ya NBC 2026/27 matokeo rasmi baada ya dakika 90. Mnyama ameanzia alipoishia msimu uliopita wa 2025/26 aliposhinda kwa mabao 2-1. Singinda Black Stars haijawahi kushinda dhidi ya Simba SC katika mechi za ligi.

