- Kivumbi Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27, maandalizi yamepamba moto, ratiba na kambi
- Yanga SC vs Simba SC Ngao ya Jamii Uwanja wa Uhuru, Agosti 12,2026
- Polisi Tanzania vs Azam FC mchezo wa ufunguzi kwa matajiri wa Dar itakuwa ugenini
Siku zinazidi kusonga kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 kabla ya pazia kufunguliwa rasmi.Agosti 12,2026 mchezo wa Ngao ya Jamii utawakutanisha Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa New Amaan Complex. Mwanzo wa Kariakoo Dabi ni ishara kwamba ligi imefunguliwa rasmi. Agosti 14,2026 msimu mpya utaanza kwa mechi kali kuchezwa.
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 upande wa kambi Simba SC, Yanga SC, Azam FC na S.B.S
Timu ambazo zilimaliza ndani ya nne bora maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 yamezidi kushika kasi. Yanga SC hawa ni mabingwa watetezi wa NBC Premier League. Kambi yao ilikuwa Dar, Avic Town Kigamboni. Hii yote ikiwa ni kuelekea katika mwanzo wa msimu kupambania kutetea taji walilolitwaa 2025/26.
Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Manqoba Mngqith ni raia wa Afrika Kusini alitambulishwa Julai 2026. Tayari yupo kambini na wachezaji akiendelea kuwapa mbinu za ushindi. Agosti 9,2026 wachezaji wote watanatarajiwa kutambulishwa, Uwanja wa Uhuru katika tamasha la Wiki ya Mwananchi.
Mtambue kocha mpya Yanga SC: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog
Simba SC kambi yao Rwanda na Dar
Mabingwa wa CRDB Federation Cup, Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker kambi yao ilianza Dar. Mara baada ya wachezaji kurejea kambini walikwea pipa kuelekea Rwanda waliposhiriki Kagame Cup. Mnyama aligotea hatua ya makundialipokusanya pointi 5.
Mechi 3 katika hatua ya makundi alicheza huku akipata sare 2 na ushindi mchezo mmoja. Ilikuwa Simba SC 1-2 Singida Black Stars. Huu ulikuwa ni mchezo wa mwisho na timu zote kutoka Tanzania ziliaga mashindano rasmi zikiishia hatua ya makundi.
Tayari kikosi cha Simba SC kimerejea Dar kwa maandalizi ya mwisho kuanza msimu. Ni Agosti 8,2026 wanatarajia kuwa na tamasha kubwa la Simba Day litakalofanyika Uwanja wa Uhuru. Hapa wachezaji wote wa kikosi hicho na benchi la ufundi watatambulishwa kwa mashabiki na dunia.
Azam FC Rwanda na Dar
Matajiri wa Dar, Azam FC nao kambi yao ilikuwa sehemu mbili kuelekea 2026/27. Walianza Dar mara baada ya wachezaji kurejea kisha wakakwea pipa kueleka Rwanda. Chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge wanaendelea na mazoezi nchini Rwanda.
Azam FC itarejea Dar mapema kwa maandalizi ya mwisho. Msimu wa 2025/26 timu hii ilimaliza ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo. Moja ya timu ambazo zimekuwa zikileta ushindani wa kweli katika mechi za ushindani.
Singida Black Stars, (S.B.S) ni Singida, Dar, Rwanda na Arusha
Kutoka Singida timu iliyopoteza taji la Kagame imeweka kambi katika maeneo matatu tofauti.Singida Black Stars walianza mazoezi Singida kisha Dar. Walikwea pipa kuelekea Rwanda ambapo walikuwa wanatetea taji la Kagame.
Hatua ya makundi waliishia kwa kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Simba SC. Timu hiyo ilishuhudia ubao ukisoma Simba SC 2-1 Singida Black Stars. Matokeo hayo yalikamilisha safari ya kutetea taji kuishia njiani. Kwa sasa wanamalizia maandalizi ya mwisho Arusha.
Uzinduzi wa jezi mpya
Timu 3 zimetambulisha jezi mpya za msimu wa 2026/27. Simba SC ilianza kutambulisha uzi mpya wa msimu kisha Azam FC matajiri wa Dar walifuata. Yanga SC inayodhaminiwa na SportPesa Agosti 6,2026 ilifanya uzinduzi rasmi wa uzi mpya.
Ijue ratiba ya Yanga SC:Ratiba ya Yanga SC NBC Premier League 2026/27 mechi 10 zamoto / Kariakoo Dabi Oktoba 10,2026
Mechi za mwanzo kwa wababe hawa
Polisi Tanzania vs Azam FC, Agosti 15,2026 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Namungo FC vs Yanga SC, Agosti 15,2026, Uwanja wa Majaliwa
Kagera Sugar vs Simba SC, Agosti 15,2026, Uwanja wa Kaitaba
Ratiba ya mechi za Agosti 14,2026
Pamba Jiji FC vs Dodoma Jiji FC, Uwanja wa CCM Kirumba
Mbeya City vs Geita Gold, Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Singida Black Stars vs Fountain Gate, Uwanja wa Airtel
Hitimisho
Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27 duru linatarajiwa kufunguliwa kwa mechi 3 kali kuchezwa Agosti 14,2026. Mabingwa watetezi Yanga SC mechi ya ufunguzi watakuwa ugenini dhidi ya Namungo FC. Simba SC watamenyana na Kagera Sugar ugenini. Matajiri Azam FC wataanza na Polisi Tanzania ugenini, Agosti 15,2026.



