- Mchezo wa kufuzu AFCON 2027 Taifa Stars 0-2 Guine-Bissau, Uwanja wa New Amaan Complex
- Seleman Mwalimu, Kibu Dennis, Simon Msuva walianza kikosi cha kwanza kwa Stars
- Mchezo unaofuata ni Septemba 29 itakuwa Taifa Stars vs Madagascar
Mchezo wa kwanza katika Kundi L umekamilika kwa ubao kusoma Taifa Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau.Mlinda mlango wa Stars Zuber Foba alianza kufungwa dakika ya 33 baada ya mabeki Bakari Nondo na Bacca kushindwa kuokoa hatari.Mabao ya wageni yamefungwa na Francullino Dju dakika ya 33 na Mama Balde dakika ya 58, Uwanja wa New Amaan Complex.
SOMA HII PIA: Taifa Stars vs Guinea-Bissau AFCON 2027 |H2H | Prediction | SportPesa Blog
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Taifa Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau taaarifa muhimu
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | Kuwania kufuzu AFCON 2027 |
| Hatua | Makundi, Kundi L |
| Matokeo | Taifa Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau |
| Uwanja | New Amaan Complex |
H2H Taifa Taifa Stars vs Guinea-Bissau
| Tarehe | Matokeo |
| 27/01/2021 | Tanzania 2-2 Guinea |
| 10/09/2024 | Guinea 1-2 Tanzania |
| 25/09/2026 | Taifa Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau. |
Mabadiliko yaliyofanywa kwa Taifa Stars
Kwenye mchezo wa leo Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi alifanya mabadiliko kipindi cha pili. Dakika ya 62 Himid Mao, Charles M’mombwa na Seleman Mwalimu walikwenda benchi na Mudathir Yahya, Alphonce Mabula na Tarryn Allarakhia waliingia. Licha ya mabadiliko hayo bado ngoma ilikuwa nzito kwa wenyeji.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa Guinea-Bissau
Iano Simao alitumia dakika 55. Ni dakika 10 zilimtosha kipindi cha pili nafasi yake akachukua Adramane Cassama. Dakika 3 mbele Guinea wakafunga bao la pili kwenye mchezo.
Hitimisho
Taifa Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau ni matokeo rasmi mchezo wa ufunguzi kuwania kufuzu AFCON kwa wenyeji. Mchezo ujao kwa Stars ni Septemba 29, 2026 itakuwa dhidi ya Madagascar utakaochezwa Morocco. Kwenye Kundi L timu nyingine ni Nigeria, fainali zinatarajiwa kuanza Juni 19 hadi Julai 19, 2026 itafanyika katika nchi 3 ambazo ni Tanzania, Uganda na Kenya.


