- Tetesi za usajili 2026/27: Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs, Makabi Lilepo
- Israel Mwenda beki wa Yanga SC anatajwa kuwa katika hesabu za Singida Black Stars
- Yanga SC itaweka kambi kwa maandalizi ya msimu ujao Avic Kigamboni, Dar
Katika dirisha la usajili 2026/27, Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs, Makabi Lilepo kuongeza nguvu katika kikosi. Wananchi wanatajwa kuwa kwenye mpango mzito kuboresha kikosi hicho kuelekea msimu ujao. Lengo la timu hiyo ni kuhakikisha wanaendeleza ubora wao na kutetea ubingwa wa ligi.
Msome kocha mpya Yanga SC: Kocha mpya Yanga SC 2026/27 CV yake hii hapa kazi inaanza upya | SportPesa Blog
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs Makabi Lilepo

Historia ya Yanga SC na usajili: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Tetesi zinadai kwamba Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs, Makabi Lilepo kuelekea msimu ujao. Mabingwa hao watetezi wanatajwa kuwa katika mazungumzo kukamilisha dili jipya. Lilepo ni raia wa DR Congo ana miaka 28.
Ni chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi ambaye ni kocha mpya akirithi mikoba ya Pedro Goncalvels aliyefutwa kazi mwishoni mwa msimu. Kuna uwezekano mkubwa winga huyo akaja Tanzania.Mbali na Yanga SC Far Rabat na Al Ahly zinatajwa kuwania saini ya nyota huyo.
Mohamed Mussa
Ukiweka kando jina la Lilepo tetesi zinaeleza kuwa kuna beki mwingine anafuatiliwa kwa ukaribu na Yanga SC. Ni mlinzi wa kati wa Mashujaa anaitwa Mohamed Mussa. Ni kandarasi ya miaka miwili ameandiliwa beki huyu.
Mpango mkubwa wa Yanga SC ni kuwa na kikosi chenye ushindani mkubwa. Katika eneo la ulinzi wanahitaji kuwa bora zaidi. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2025/26 ilikuwa namba moja kwa kufungwa mabao machache.
Abdulnasir Gamal
Nyota mwingine anayetajwa kufuatiliwa na mabingwa watetezi ni Abdulnasir Gamal. Huyu ni beki wa kulia anatajwa kuandaliwa kandarasi ya miaka miwili. Huyu ni beki ambaye 2025/26 alikuwa akivaa uzi wa Mashujaa FC inayotumia Uwanja wa Lake Tanganyika kwa mechi za nyumbani.
Emmanuel Flomo
Tetesi zinaeleza kuwa Yanga SC wanafuatilia saini ya winga Emmanuel Flomo. Nyota hyu ana miaka 18. Ni raia wa Liberia anacheza Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan. Ikiwa makubaliano yatafika katika hatua nzuri kuna uwezekano akawa ni njano na kijani.
Hawa hapa kuondoka Yanga SC
Israel Mwenda
Beki huyu anatajwa kuwa ataondoka katika kikosi cha Yanga SC. Timu ambayo huenda akaitumikia msimu wa 2026/27 ni Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Airtel kwa mechi za nyumbani.
Prince Dube
Tayari mshambuliaji huyu ameshaaga ndani ya kikosi cha Yanga SC. Atakuwa nchini Zimbabwe akirejea nyumbani kwa kazi. Ni Klabu ya Hardrock amesaini mara baada ya kumaliza mkataba wake na watotot wa Jangwani.
Dube alisema kuwa maisha yake ndani ya Yanga SC yalikuwa na furaha ataendelea kuwafuatilia akiwa Zimbabwe. “Nimerejea nyumbani kwa sasa. Licha ya kwamba nitakuwa hapa bado nitakuwa ninaifuatilia kwa ukaribu timu. Ninawashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi,” .
Shekhani Khamis
Kijana mwenye mashuti makali ndani ya kikosi cha Yanga SC anatajwa kuwa ataondoka. Ni Shekhani Khamis ambaye hakuwa na nafasi kiksi cha kwanza msimu uliopita. Singida Black Stars wanatajwa kuhitaji saini ya nyota huyo.
Kambi ya Yanga SC
Kwa mujibu wa Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema kuwa timu hiyo itaweka kambi Avic Town.
Hitimisho
Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs, Makabi Lilepo ikiwa ni hesabu kuelekea msimu mpya. Wananchi watapeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika jambo linalofanya wawe sokoni. Mbali na Ligi ya Mabingwa Afrika wanapambana kutetea taji la ligi.

