- Mchezo wa nusu fainali FIFA Kombe la Dunia 2026 England vs Argentina unatarajiwa kuchezwa Julai 15, 2026
- Lionel Messi kinara wa ufungaji akiwa amefunga mabao 8 anakutana na Harry Kane nahodha wa England
- Mabingwa watetezi watakuwa kazini kupambania nafasi kutinga hatua ya fainali itakayopigwa Jumapili, Julai 19
Mchezo mkali nusu fainali FIFA Kombe la Dunia 2026 England vs Argentina unasubiriwa kwa shauku kubwa. Hii inatokana na rekodi za timu hizo kuwa katika viwango bora wakishinda mech izote sita. Mabingwa watetezi watakuwa kazini kwenye mchezo wa nusu fainali Jumatano saa 10:00 usiku mjini Atlanta.
Utabiri wa England vs Argentina: Prediction | England vs Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026: Nusu fainali, Ratiba, Live score, h2h, odds na habari za timu
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya England vs Argentina
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

England vs Argentina safari za timu
England, haijawahi kuonyesha kiwango cha kushawishi katika michuano hii yote, iliifunga Norway mabao 2-1 baada ya muda wa ziada (extra time) hatua ya robo fainali. Hii ni nusu fainali yao ya nne ya michuano mikubwa tangu mwaka 2018.
Kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel kimeshinda mechi zake zote za hatua ya mtoano kwenye kombe la Dunia kwa tofauti ya bao moja tu. Wanakabiliwa na wapinzani wagumu Argentina ya Lionel Messi.
Argentina nao walilazimika kucheza muda wa ziada katika mchuano robo fainali dhidi ya Uswisi, na hatimaye kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ili kujihakikishia nafasi katika nusu fainali ya pili mfululizo. Messi anaongoza orodha ya wafungaji bora wa michuano hiyo akiwa na mabao 8, akilingana na Kylian Mbappe wa Ufaransa.
Kikosi cha Lionel Scaloni kimeshinda mechi zote 6 walizocheza kwenye Kombe hili la Dunia 2026. Mabao 17 yanawafanya kuwa wafungaji bora wa mashindano hayo wakati wakisaka kuweka historia ya kushinda mataji mawili mfululizo.
England walitolewa katika hatua ya nusu fainali mwaka 1990 na 2018, hivyo wanatumai kuvunja mwiko huo hapa ili kufuzu hatua hiyo ya fainali ambayo imekuwa ngumu kwao kuifikia. Mara ya mwisho walicheza fainali ya Kombe la Dunia ilikuwa pale waliposhiriki kama wenyeji na kulitwaa taji hilo mwaka 1966.
England vs Argentina wachezaji watakaokosekana

Ijue ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Jarell Quansah bado anatumikia adhabu ya kusimamishwa kwa upande wa England baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Mexico katika hatua ya 16 bora. Anaungana na Declan Rice anayeugua, ambaye pia hatashiriki mchezo huu.
Reece James aliingia kutokea benchi kwenye mchezo dhidi ya Norway na anaweza kupata nafasi ya kuanza hapa, akitengeneza pacha ya kipekee na Elliot Anderson kwenye safu ya viungo. Bukayo Saka naye anatarajiwa kuanza mchezo huu, huku Noni Madueke akirejeshwa benchi.
Eberechi Eze na Morgan Rogers nao waliingia kutokea benchi katika mchezo uliopita, na hali hiyo hiyo inatarajiwa kuwakuta tena hapa, huku Anthony Gordon akitarajiwa kuanza kikosi cha kwanza (starting XI).
Nahodha Harry Kane na Jude Bellingham wa Real Madrid ndio wanaoongoza kwa ufungaji kwa England wakiwa na mabao 6 kila mmoja, na wote wanatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza.
Kwa upande wa Argentina, Lionel Messi amekuwa chimbuko kubwa la hamasa na ataongoza safu ya ushambulizi. Anaingia kwenye mchezo huu akiwa mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia (mabao 21) na kinara wa kutoa pasi za mabao (pasi 10). Lautaro Martinez aliingia kutokea benchi katika ushindi dhidi ya Uswisi na huenda akalazimika kusubiri tena benchi hapa huku Julian Alvarez akihifadhi nafasi yake ya kuanza.
Mfungaji wa bao Cristian Romero pamoja na Leandro Paredes walichechemea kutoka nje katika ushindi wa robo fainali, lakini wote wanatarajiwa kuwa fiti kuanza mchezo huu.
Rekodi ya Mechi Zilizopita (Head-to-Head) na Fomu ya Sasa
Timu zote mbili hazijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi zao tano zilizopita kuelekea nusu fainali hii ya kusisimua, huku Argentina wakiwa na rekodi ndefu zaidi ya ushindi wakishinda mechi zao 13 zilizopita katika mashindano yote.
Fomu ya Sasa:
Uingereza – WWWWD (Ushindi, Ushindi, Ushindi, Ushindi, Sare)
Argentina – WWWWW (Ushindi, Ushindi, Ushindi, Ushindi, Ushindi)
Mechi Zilizopita (Head-to-Head)
| Tarehe | Mashindano | Matokeo |
| Novemba 12, 2005 | Mechi ya Kirafiki | England 3-2 Argentina |
| Juni 7, 2002 | Kombe la Dunia la FIFA | Argentina 0-1 England |
| Februari 23, 2000 | Mechi ya Kirafiki | England 0-0 Argentina |
| Juni 30, 1998 | Kombe la Dunia la FIFA | Argentina 2 (4) – 2 (3) England (Argentina ilishinda kwa penati) |
| Mei 25, 1991 | Kombe la Skol (Mechi ya Kirafiki) | England 2-2 Argentina |
Hitimisho
Ni nusu fainali FIFA Kombe la Dunia 2026 England vs Argentina Julai 15,2026. Saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki mechi hii kali itapigwa. Mshindi atacheza fainali Julai 19, Jumapili vs mshindi wa mchezo wa Ufaransa vs Hispania.

