- FT Gaborone United 1-1 Yanga SC CAF Champions League matokeo ya sasa hivi mchezo wa hatua ya awali, uliopigwa Botswana Septemba 5, 2026
- Mshambuliaji Seleman Mwalimu wa Yanga SC amefunga bao la kusawazisha dakika ya 90+6 likiwa ni muhimu kwa wageni
- Wenyeji walianza kufunga kipindi cha kwanza dakika ya 33 kupitia kwa Obrey Amsed aliyepiga faulo iliyomshinda mlinda mlango Djigui Diarra
Hatimaye Gaborone United 1-1 Yanga SC ni matokeo rasmi mchezo wa CAF Champions League uliopigwa Botswana National Stadium.Wachezaji bora wa Wananchi wakiwemo Peter Shalulile, Djigui Diarra, Maxi Nzengeli, Bakari Nondo walianza kikosi cha kwanza. Wenyeji Gaborone United walianza na wachezaji tegemeo akiwemo Obrey Amsed mtaalamu wa mapigo huru na mfungaji wa bao la kuongoza.

Takwimu za Gaborone United vs Yanga SC: Gaborone United vs Yanga SC Live Score, H2H & Predicted Lineups, Latest News- CAF Champions League 2026/27
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Gaborone United 1-1 Yanga SC
Timu zote mbili zimetoshana nguvu kwenye mchezo wa hatua ya awali uliochezwa Botswana.Wenyeji walianza kutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kupata bao la kuongoza. Ni shuti moja ambalo walipiga ndani ya dakika 45 likilenga lango.
Yanga SC kipindi cha kwanza walikamilisha bila kupiga shuti ambalo lililenga lango. Hii ilitokana na wenyeji kutumia mbinu ya kujilinda zaidi. Kipindi cha pili Wananchi waliongeza nguvu kwenye ushambuliaji.
Mabadiliko ya wachezaji akiwemo Aziz Ki aliyeingia dakika ya 45 akichukua nafasi ya Albert Kangwanda yaliongeza nguvu. Seleman Mwalimu mfungaji pekee wa bao la Yanga SC alianzia benchi. Mshambuliaji huyo aliingia dakika ya 81 akichukua nafasi ya Peter Shalulile.
H2H Gaborone United vs Yanga SC
Septemba 5, 2026, Gaborone United 1-1 Yanga SC
Septemba 12, 2026, Yanga SC vs Gaborone United
Hitimisho
Gaborone United 1-1 Yanga SC ni matokeo yakufurahisha kwa wageni Yanga SC kwa kupata bao la ugenini. Licha ya kufunga bado mchezo wa pili utaamua nani atasonga mbele. Shukrani kwa Seleman Mwalimu aliyeweka usawa katika mchezo huo ambao Wananchi walikuwa nyuma kwa kutanguliwa kufungwa bao.

