- Mshindi apokea zawadi ya kufungia mwaka na bonasi za ziada
- Adam Alphonce Kuhodanga ajishindia TZS 247,825,550 kwa kubashiri kwa usahihi mechi zote 13/13 za Mid-Week Jackpot.
Dar es Salaam, Kampuni inayoongoza ya michezo ya kubashiri na burudani, SportPesa imeendelea kutoa tabasamu kwa wateja wake baada ya Desema 31, mwaka jana kumtangaza mshindi wa mwisho wa mwaka wa Mid-Week Jackpot ambapo Adam Alphonce Kuhodanga, mkazi wa Kimara Mwisho na mfanyabiashara wa vipuri vya magari, ameibuka na kitita cha TZS 247,825,550 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13.

Pamoja na ushindi huo wa Jackpot, Adam amepokea pia bonasi za nyongeza zenye thamani ya TZS 5,274,660, na kufanya jumla ya ushindi wake kuwa TZS 253,100,210.
MSHINDI ANASEMAJE?
Akizungumza mara baada ya ushindi, Adam alisema: “Nimekuwa nikicheza na SportPesa kwa zaidi ya miaka sita, lakini sijawahi kupata ushindi mkubwa kama huu. Mara nyingi nilikuwa nikitumia muda mwingi kuchambua matokeo ya mechi kabla ya kuweka ubashiri wangu. Hii ni mara ya kwanza niliweka ubashiri ndani ya dakika mbili tu, na matokeo yake ni ya kipekee. Ushindi huu utanisaidia kukuza biashara yangu na kufanikisha malengo yangu ya mwaka mpya. Naikubali sana SportPesa kwa kunipa nafasi ya kubadilisha maisha yangu!”
MAONI KUTOKA SPORTPESA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas, alisema: “Kwa niaba ya SportPesa, tunayo furaha kumpongeza Adam Alphonce Kuhodanga kwa ushindi huu mkubwa wa Mid-Week Jackpot. Ushindi huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuleta fursa za kipekee kwa wateja wetu na kubadilisha maisha yao kupitia michezo yetu. Ni matumaini yetu kuwa zawadi hii itakuwa mwanzo mzuri wa mwaka mpya kwa Adam.”
Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa, Tracy Humplick, aliongeza: “Tangu kuanzishwa kwetu, SportPesa imefanikiwa kutangaza washindi 14 wa Mid-Week Jackpot na kulipa zaidi ya TZS 5 Bilioni. Tuna furaha kumsherehekea Adam kama mshindi wetu wa 15 na wa mwisho wa mwaka 2024. Tunawahakikishia pia wateja wetu kwamba ushindi upo na kila mmoja ana nafasi ya kushinda”

“Kwa taarifa zaidi kuhusu bidhaa zetu na kuona jinsi mshindi wetu atakavyokabidhiwa zawadi yake, tembelea kurasa zetu rasmi za mitandao ya kijamii na tovuti ya SportPesa.”
Mwisho

