Maiko Mathew Namkoloma , wikiendi iliyopita amejishindia jumla ya Sh 11,346,314, kama Supa Jackpot bonus, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 kati ya 17, alizocheza.
Maiko, ambaye ni mkazi wa Mbezi, Dar-Es-Salaam, alianza kucheza na SportPesa miaka mitano iliyopita, baada ya kushawishiwa na rafiki yake (hakutaka kumtaja jina) na pia baada ya kuwa anawaona washindi wa Jackpot za SportPesa wakitangazwa mara kwa mara katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter.

Haikuwa rahisi kwa namna ambavyo kila mtu anaona mimi ni mshindi. Nakumbuka wakati ndio nimeanza nilikuwa mara nyingi nacheza mwenyewe, kuna muda nilikuwa nacheza mechi zikiwa live. nilijaribu kuweka ubashiri wangu kwenye Supa Jackpot mara mbili na baada ya kutoambulia chochote nilicheza Mid-Week Jackpot ambapo napo sikufanikiwa kushinda Jackpot wala bonus za Jackpot. Ila kwenye Multibet nimefanikiwa kushinda kama laki 8, laki 7, laki 5.
Akiongelea mkeka wake huu wa Supa Jackpot ambao umeshinda bonus, Maiko anasema yeye huwa na kawaida ya kufuatilia mikeka ya Supa Jackpot mara nyingi kuanzia Alhamisi, na kisha huchukua kama masaa mawili hadi matatu kufanya tathmini.

Mara nyingi huwa naangalia hizi timu zimesha kutana mara ngapi, na matokeo yake yalikuwaje. Kisha hutizama fomu ya timu kwa muda huo. Kwa mfano katika mechi 5 zilizopita matokeo ya timu husika yalikuwaje?
Muda mwingine huwa nachagua timu ambazo zinatoka ligi moja kama zipo kwenye mkeka. Kwa mfano timu za Championship au ligi ya daraja la pili ufaransa, ujerumani, uturuki, uholanzi etc.
Au naweza nikakadiria matokeo kutokana na namna odds za timu husika zilivyowekwa. Nikimaliza hapo, huwa natizama mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana matokeo yalikuwaje na kama wachezaji wa wakati ule mpaka muda wanaenda kukutana ni hao hao au kuna mabadiliko makubwa katika kikosi.
Baada ya kujiridhisha na taarifa nilizoziona kuhusiana na timu zilizowekwa, hufanya maamuzi ya kuweka mikeka 3 na kusubiria matokeo.
Nilifurahi sana baada ya kuwa nimeweza kupatia mkeka wa kwanza ambao ndio ulionipa bonus, mkeka wa pili ulitoa mechi 10 na mkeka wa 3 ulitoa mechi 5. Sms ya ushindi niliipata nikiwa kwenye harusi na marafiki zangu kuwa nimeshinda11,346,314 kama Supa Jackpot bonus’’. Niliwaonyesha baadhi ya marafiki zangu ile sms, kuna wengine waliamini na kuna ambao hawakuamini.” Alisema Maiko.Kuhusu atafanyia nini kiasi hichi alichoshinda Maiko anasema pesa hii itakuwa mtaji kwake wa kumalizia vyumba za wapangaji ambazo amekuwa anazijenga, na nyingine ataongezea kwenye biashara zake anazofanya.
‘’Unajua kwa sasa mimi nipo katika ujenzi wa vyumba vinne vya wapangaji, hivyo hela hii itanisaidia kumalizia vyumba hivyo ili wapangaji waweze kuingia kwa haraka, pia nitaongezea mtaji kwenye biashara zangu zingine.
Akitoa neno la pongezi kwa mshindi, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Majuto kwa kufanikiwa kushinda Supa Jackpot bonus na kumtaka aendelee kucheza ili aweze kushinda zaidi.
Nianze kwa kukupongeza kwa ushindi wako wa Supa Jackpot na pia nichukue nafasi hii kuwahamasisha watanzania ambao bado hawataki kuamini SportPesa ndio baba wa Jackpot zote nchini.
Maiko ni ushuhuda mwingine kwenu, kama alivyosema yeye alianza kucheza miaka 5 iliyopita, ana ameweza kufanikiwa kushinda hela za kiwango tofauti tofauti na leo hii ameibuka kuwa mshindi wa SupaJackpot Bonus, Sidhani kama ukicheza Jackpot au mikeka mingine kama ya multibet unakuwa na kikomo cha kushinda.
Ni juhudi yako tu ya kucheza na kutokata tamaa, ukiamini siku yako itafika, basi na wewe mtanzania utafanikiwa.
