
Ijue ratiba ya ligi: Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Mechi zote 240 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Polisi Tanzania ni moja ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, ligi kuu ya soka nchini Tanzania. Klabu hii yenye makao yake mkoani Kilimanjaro, imerejea kwa mara nyingine ikitokea Championship. Msimu wa 2026/27 wameanza kwa utofauti katika mechi za mwanzo wakipata ushindi katika mechi 2, sare 1 na kupoteza mchezo 1.
Makala haya yanakuletea uchambuzi wa kina kuhusu Polisi Tanzania, ikijumuisha ratiba yao kamili ya mechi zijazo, matokeo ya hivi karibuni, na msimamo wao katika Ligi Kuu Bara. Pia tutaangalia fomu ya timu, wachezaji muhimu, na matarajio yao kwa msimu huu. Ni muhimu kwa mashabiki na wadau wa soka kufahamu mwenendo wa timu hii.
Ijue ratiba na matokeo mzunguko wa 5: Ratiba ya Ligi Kuu mzunguko wa 5 | Fountain Gate 0-2 Yanga SC | Simba SC 2-0 Geita Gold | Msimamo | SportPesa
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.
Ratiba kamili ya Polisi Tanzania Ligi Kuu Bara 2026/27
Polisi Tanzania walifungua pazia kwa mchezo wakiwa nyumbani dhidi ya Azam FC. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ilikuwa Agosti 15, 2026. Matokeo rasmi ilikuwa 1-1 wakigawana pointi mojamoja na matajiri wa Dar.
| Tarehe | Muda | Mechi | Uwanja |
| 06-Sep-2026 | 16:00 | Polisi Tanzania vs Coastal Union | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid |
| 8-Oktoba-2026 | 16:00 | Mashujaa FC vs Polisi Tanzania | Uwanja wa Lake Tanganyika |
| 17-Oktoba-2026 | 16:00 | Kagera Sugar vs Polisi Tanzania | Uwanja wa Kaitaba |
| 23-Oktoba-2026 | 16:00 | Pamba Jiji FC vs Polisi Tanzania | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid |
Ratiba hii inaweza kubadilika kulingana na matangazo rasmi kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB). Mashabiki wanashauriwa kufuatilia vyanzo rasmi kwa taarifa sahihi zaidi.
Matokeo ya hivi karibuni ya Polisi Tanzania
Polisi Tanzania 1-1 Azam FC, matokeo ya mchezo wa ufunguzi wakiwa nyumbani.Polisi Tanzania 2-0 JKT Tanzania ulikuwa mchezo wa pili.
Dodoma Jiji FC 0-1 Polisi Tanzania ushindi muhimu ugenini. Waliambulia kipigo kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars walipofungwa mabao 4-2 Uwanja wa Airtel.
Msimamo wa Polisi Tanzania kwenye Ligi Kuu Bara
| Nafasi | Timu | Mechi | Ushindi | Sare | Poteza | Pointi |
| 7 | Polisi Tanzania | 4 | 2 | 1 | 1 | 7 |
| 8 | Mashujaa FC | 4 | 2 | 0 | 2 | 6 |
| 9 | Namungo FC | 5 | 2 | 0 | 3 | 6 |
| 10 | Dodoma Jiji FC | 4 | 1 | 1 | 2 | 4 |
| 11 | JKT Tanzania | 4 | 1 | 1 | 2 | 4 |
Uchambuzi wa fomu na wachezaji muhimu
Wachezaji imara na wenye uzoefu wapo ndani ya Polisi Tanzania. Kwenye lango Beno Kakolanya yupo eneo la walinda mlango. Mshambuliaji Habib Kyombo ni muhimu kikosi cha kwanza.
Anuary Jabir amekuwa na mwendelezo mzuri kwenye kufunga mabao muhimu safu ya ushambuliaji. Christopher Nyakanda, Denis Mushi, Joseph Majagi, Ken Mwambungu, Jamal Mtegeta, Juhudi Balayaz, Baraka Mwambule, Emmanuel Mpuka. Oscar Masai hawa wanaingia kwenye rekodi ya wachezaji walioanza kikosi cha kwanza mara baada ya kurejea kwenye ligi.
Matarajio ya Polisi Tanzania msimu huu
Chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata timu hiyo imebainisha kwamba inahitaji kuwa ndani ya 10 bora. Imejenga uimara eneo la ushambuliaji ikifunga mabao 6 katika mechi 4. Eneo la ulinzi imeruhusu kufungwa mabao 5.
Wachezaji akiwemo Kakolanya wamebainisha kwamba malengo ni kupata matokeo katika mechi za ushindani. Jaffary Kibaya amesema wapo tayari kuipambania timu kila wanapoingia uwanjani.
Hitimisho
Polisi Tanzania imerejea kwa kishindo kwenye ligi 2026/27. Katika mechi 4 za mwanzo imepoteza mchezo mmoja pekee ikishinda mechi mbili.Kwa ratiba iliyo mbele yao na matokeo ya hivi karibuni, ni wazi bado wana kazi kubwa kupambana kwa mechi zijazo. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi na uchambuzi wa kina wa Ligi Kuu Bara.


