- Ujerumani vs Paraguay FIFA Kombe la Dunia hatua ya 32 bora inatarajiwa kuchezwa Juni 29,2026
- Saa 5:30 usiku wababe hawa wawili wanatarajiwa kukutana saa za Afrika Mashariki, Uwanja wa Gillette, Foxborough, Massachusetts, Marekani
- SportPesa Blog tumekuletea makala ya uchambuzi mchezo huu mkubwa, takwimu na makutano ya timu hizi
Ujerumani vs Paraguay FIFA Kombe la Dunia 2026 wanakutana hatua ya 32 bora Uwanja wa Gillette, Foxborough, Massachusetts, wakigombea nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora. Timu ya Ujerumani, chini ya kocha Julian Nagelsmann, ilimaliza hatua ya makundi ikiwa kinara baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja. Walipoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Ecuador kwa mabao 2-1,tayari walikuwa wamejihakikishia tiketi ya kufuzu kutokana na ushindi dhidi ya Curacao na Ivory Coast.
Hii hapa ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Taarifa kuhusu mechi
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | FIFA Kombe la Dunia 2026 |
| Hatua | Raundi ya 32 |
| Mchezo | Ujerumani vs Paraguay |
| Muda | Saa 5:30 usiku (EAT) |
| Siku | Jumatatu |
| Tarehe | Juni 29, 2026 |
| Uwanja | Uwanja wa Gillette, Foxborough, Massachusetts, Marekani |
| Jukwaa la kubashiri | SportPesa |
Ujerumani vs Paraguay taarifa za timu
Paraguay ni mtihani mkubwa wanakabiliana na timu yenye historia kubwa ya mafanikio katika mashindano ya kimataifa. Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkali, ikizingatiwa kwamba ni hatua ya mtoano ambapo kila kosa linaweza kugharimu safari ya timu kuelekea hatua ya juu zaidi.
Ujerumani (Die Mannschaft) wameonyesha tena ubora wao wa kushambulia, wakiwa na vijana wenye kipaji kama Jamal Musiala, Florian Wirtz, Leroy Sané na Kai Havertz wakicheza nafasi muhimu. Mshambuliaji Deniz Undav amevutia kwa kiwango huku kikosi hiki cha vijana wa Ujerumani kikiendelea kuchanganya ubunifu na uzoefu wa wachezaji wakongwe.
Kwa upande wa Paraguay (La Albirroja), wamerejea katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia baada ya kampeni ya kuvutia hatua ya makundi. Licha ya kupoteza kwa kipigo kikubwa dhidi ya Marekani, walionyesha uthabiti kwa kurejea na ushindi wa 1-0 dhidi ya Uturuki, kisha wakapata sare tasa dhidi ya Australia ambayo iliwawezesha kufuzu hatua ya 32 bora.
Kocha mkuu Gustavo Alfaro ameunda kikosi cha nidhamu kinachotegemea ulinzi imara na mashambulizi ya haraka. Julio Enciso anaendelea kuwa tishio kubwa la ubunifu kwa Paraguay, huku Gabriel Ávalos na Isidro Pitta wakitoa chaguo za kushambulia mbele.
Taarifa za wachezaji
Ujerumani hawana wasiwasi mkubwa wa kusimamishwa wachezaji kuelekea mchezo wa mtoano na wanatarajiwa kuanza na kikosi chenye nguvu.Julian Nagelsmann ana uwezekano mkubwa wa kuendelea na Jamal Musiala na Florian Wirtz wakicheza nyuma ya mshambuliaji Deniz Undav, huku Kai Havertz na Leroy Sané wakiwa chaguo za kuongeza nguvu ya mashambulizi.
Joshua Kimmich anatarajiwa tena kuongoza safu ya kiungo sambamba na Felix Nmecha, huku Antonio Rüdiger akisimamia safu ya ulinzi mbele ya kipa mkongwe Manuel Neuer.Kwa ujumla, kikosi cha Ujerumani kinaonekana kuwa uwiano wa uzoefu na ubunifu, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kuendelea mbele katika mashindano haya.
Julio Enciso atabeba matumaini makubwa ya mashambulizi ya Paraguay, huku Gabriel Ávalos na Isidro Pitta wakipigania nafasi mbele. Nahodha Gustavo Gómez anatarajiwa kuongoza safu ya ulinzi sambamba na Omar Alderete, na kipa Orlando Gill ana uwezekano mkubwa wa kuanza langoni.
Ujerumani vs Paraguay vikosi vinavyotarajiwa kuanza
- Ujerumani XI ya kuanza: Manuel Neuer; Joshua Kimmich, Jonathan Tah, Antonio Rüdiger, David Raum; Aleksandar Pavlovic; Felix Nmecha, Jamal Musiala, Florian Wirtz; Denis Undav, Leroy Sané
- Paraguay XI ya kuanza: Orlando Gill; Juan Cáceres, Gustavo Gómez, Omar Alderete, Alexandro Maidana; Cubas, Villasanti; Enciso, Almirón, Sosa; Ávalos
H2H Ujerumani vs Paraguay

Utabiri wa Uholanzi vs Morocco huu hapa: Prediction Uholanzi vs Morocco FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, Predknockout preview, h2h, odds
| Kipengele | Ujerumani | Paraguay | Jumla |
|---|---|---|---|
| Mechi Zilizochezwa | 2 | 2 | 2 |
| Ushindi | 1 | 0 | 1 |
| Sare | 1 | 1 | 1 |
| Magoli Jumla | 4 | 3 | 7 |
Juni 15, 2002 – Raundi ya 16, FIFA Kombe la Dunia: Ujerumani 1-0 Paraguay (Bao la Oliver Neuville dakika ya 88).
Agosti 14, 2013 – Mchezo wa kirafiki: Ujerumani 3-3 Paraguay ( Kaiserslautern, Ujerumani).
Prediction Ujerumani vs Paraguay
Paraguay wamekuwa na mashindano mazuri na wana ubora wa kuendelea kushindana, hasa kupitia Julio Enciso na Miguel Almirón katika mashambulizi ya kushtukiza. Lakini ubora wa kiufundi wa Ujerumani, kina cha kikosi chao cha kushambulia na udhibiti wa kiungo vinatarajiwa kuwa maamuzi ya mwisho. Timu ya Nagelsmann huunda nafasi mara kwa mara na ina wachezaji kadhaa wanaoweza kufungua ulinzi mgumu.
Paraguay huenda wakafanya mchezo kuwa mgumu kwa muda mrefu, lakini ubora wa Ujerumani unatarajiwa kuonekana hatimaye na kuwapeleka hatua ya 16 bora. Matokeo: Ujerumani 1-2 Paraguay. Haya ni maoni sio matokeo kamili.

Jinsi ya Kubashiri kwenye SportPesa
Fungua ukurasa wa tukio la Ujerumani vs Paraguay kwenye SportPesa.
Chagua soko lako — Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB) mara tu mechi itakapoanza.
Weka dau lako na thibitisha ubashiri.

