Brazil vs JapanBrazil vs Japan
  • Brazil vs Japan Kombe la Dunia 2026, ni mechi ya pili ya hatua ya 32 bora ambayo inatarajiwa kupigwa leo Jumatatu 29 Juni 2026 katika Uwanja wa Houston, USA.
  • Mechi hii kali inatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mshindi wa mechi hii anafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.
  • Jeshi la Brazili linatarajiwa kuongozwa na staa wao hatari Vinicius Jr aliyefunga mabao 4, sambamba na Neymar Jr ambaye amerejea rasmi uwanjani.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

Mabingwa mara 5 wa Kombe la Dunia timu ya taifa ya Brazil, leo watakuwa wenyeji wa Japan katika mchezo mkali wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora ya mashindano hayo. Mechi hii inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Houston, USA kuanzia majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Brazil ikibebwa na mastaa kama Neymar Jr na Vinicius Jr inasaka nafasi ya kurejea katika rekodi za mashindano hayo.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Brazil vs Japan

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Brazil vs Japan
Brazil vs Japan

Maelezo ya Mechi

Brazil vs Japan h h
Brazil vs Japan
KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo wa hatua ya 32 Bora katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Tarehe na MudaPambano hili litapigwa Jumatatu, 29 Juni 2026, kuanzia saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
UwanjaMechi itafanyika katika Uwanja wa NRG, uliopo Houston, Texas, Marekani.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa Brazil vs   Japan

Mchezo kati ya Brazil na Japan ni miongoni mwa mechi zinazosubiriwa kwa hamu katika hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia 2026. Timu hizi zitakutana Jumatatu usiku kwenye Uwanja wa NRG, Houston. Ikumbukwe Brazil walimaliza kileleni mwa Kundi C, huku Japan wao wakimaliza nafasi ya 2 ya Kundi F. Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi wa mchezo mwengine wa hatua ya 32 bora, kati ya Ivory Coast vs Norway katika hatua ya 16 Bora.

Brazil wamefikia hatua hii baada ya mechi 3, ambapo walianza na sare ya mabao 1-1 dhidi ya Morocco, kisha Brazil 3-0 Haiti na Scotland 0-3 Brazil. Vinicius Junior na Matheus Cunha wamekuwa nyota wa kikosi cha Carlo Ancelotti, wakichangia Brazil kumaliza kileleni mwa Kundi C kwa tofauti ya mabao dhidi ya Morocco. Brazil hawajawahi kushindwa kufuzu hatua ya mtoano tangu mwaka 1982. Ikiwa watapata matokeo huenda wakavaana na mabingwa watetezi Argentina, katika hatua ya nusu fainali.

Mara ya mwisho Brazil na Japan kukutana, bila mabeki wao tegemeo Gabriel Magalhães na Marquinhos, Brazil ilifungwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Oktoba. Huu ulikuwa ushindi wa kwanza wa Japan dhidi ya Brazil, katika historia ya mikutano yao. Kwa upande wa Japan, ushindi huo uliwapa imani kubwa na kuonyesha uwezo wao wa kushindana na mataifa makubwa. Mwaka 2026 pia wameifunga England na kutoka sare dhidi ya Netherlands, jambo linalowafanya kutajwa kama timu inayoweza kufanya makubwa.

Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa

Brazil wapo hatarini kukosa huduma ya mshambuliaji wao na nahodha wa klabu ya Barcelona, Raphinha, ambaye alipata majeraha ya msuli wa nyuma wa paja dhidi ya Haiti. Hadi sasa hajarejea mazoezini kikamilifu, hivyo bado kuna mashaka kuhusu uwepo wake kwenye mchezo huu. Iwapo hatakuwa tayari, Carlo Ancelotti anatarajiwa kuendelea kutumia kikosi kilekile kilichoanza dhidi ya Scotland. Hii inaweza kumpa nafasi Rayan kuanza kwa mara ya kwanza, katika hatua ya mtoano wa Kombe la Dunia sambamba na Vinicius Junior.

Kwa upande wa Japan, beki wa kati Ko Itakura alitolewa mapema dhidi ya Sweden kutokana na majeraha, lakini taarifa zinaonyesha kuwa tatizo lake si kubwa. Hata hivyo, mshambuliaji Takefusa Kubo bado hajarejea mazoezini kikamilifu kutokana na maumivu ya goti.

Vikosi vinavyotarajiwa

Brazil

NafasiWachezaji
KipaAlisson Becker
MabekiDanilo, Marquinhos, Gabriel, Santos
ViungoBruno Guimarães, Casemiro
Washambuliaji wa PembeniRayan, Lucas Paquetá, Vinícius Júnior
Mshambuliaji wa KatiMatheus Cunha

Japan

Japan
NafasiWachezaji
KipaZion Suzuki
MabekiYukinari Ito, Takehiro Tomiyasu, Ko Itakura
ViungoRitsu Doan, Kaishu Sano, Ao Tanaka, Keito Nakamura
Washambuliaji wa PembeniDaichi Kamada, Daizen Maeda
Mshambuliaji wa KatiAyase Ueda

Utabiri (zaidi ya mabao 2, yaani over 1.5)

Ubora wa kikosi na uzoefu wa Brazil katika mashindano hayo makubwa, unaifanya timu hiyo kuwa tishio kwa Japan.  Ubora wa safu ya ushambuliaji ya Brazil, unatoa nafasi ya kupatikana kwa mabao, huku Japan nao wakiwa na rekodi bora ya kufunga. Tunatarajia mabao mawili au zaidi katika mchezo huu, ikumbukwe haya si matokeo halisi, bali ni maoni ya kitaalamu ya uhariri hivyo Bashiri kistaarabu.

KUJUA RATIBA NA UCHAMBUZI WA RATIBA YA BRAZIL, SOMA HII: FIFA Kombe la Dunia 2026 Ratiba ya Brazil | Mechi zote | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika | Je, Neymar Jr yuko tayari?

Rekodi ya Brazil vs Japan (H2H)

Timu hizi zimekutana mara 14 katika historia yao, ambapo Brazil wameshinda mechi 11, sare mechi 2 na kupoteza mara moja pekee.

Hitimisho

Brazil vs Japan Kombe la Dunia 2026
Neymar vs Japan

Utabiri wetu wa kiuhariri unayapa nafasi kubwa matokeo ya mabao mawili au zaidi yaani over 1.5 Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Brazil vs Japan na mechi nyingine za hatua ya 32 bora kwenye SportPesa. Tafadhali bashiri kistaarabu.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

DR Congo vs Uzbekistan Kombe la Dunia 2026
Kombe la Dunia

Brazil vs Japanitaanza saa ngapi?

Mechi itaanza saa 2 kamili kwa saa za Afrika Mashariki (EAT), leo tarehe 29 Juni 2026.

Brazili imeshinda mara ngapi kombe la Dunia?

Brazili ndiyo timu pekee ambayo imeshinda Kombe la Dunia mara 5, pia ikiwa ndiyo timu pekee ambayo imeshiriki michuano yote ya mashindano hayo tangu yaanze.

Brazil na Japan zimewahi kukutana?

Ndiyo Brazil na Japan zimekutana katika michezo 14 ambapo, Brazil wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 11 sare 2 na kupoteza mechi 1.

KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA IVORY COAST, SOMA HII: Prediction Ivory Coast vs Norway FIFA Kombe la Dunia 2026: H2H, team news, odds

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.