- Tanzania vs Senegal, echi kali ya Fainali ya U17 AFCON itapigwa kesho Jumanne 02/06/2026 nchini Morocco.
- Mechi hii inatarajiwa kupigwa majira ya saa 19:00 GMT, ambayo ni sawa na saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.
- Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat, ndio unabeba dhamana ya kubeba mchezo huu mkubwa.
- Makala hii inakuletea baadhi ya taarifa muhimu kuhusu mchezo huu.
Mechi kali ya Fainali ya U17 AFCON itapigwa kesho Jumanne nchini Morocco, ni Tanzania vs Senegal. Mechi hii inatarajiwa kupigwa majira ya saa 19:00 GMT, ambayo ni sawa na saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania. Mtanange huu mkali unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat. Makala hii inakuletea baadhi ya taarifa muhimu kuhusu mchezo huu.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano mbalimbali ya soka Msimu wa 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Bado hujashinda mamilioni? Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator: High-flying wins up to 800,000,000.
Kuhusu Fainali ya Tanzania vs Senegal U17 AFCON

Tanzania na Senegal, ndio timu Wanafainali wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Chini ya Miaka 17 (TotalEnergies CAF U-17 AFCON), Mashindano hayo kwa mwaka huu yanapigwa nchini Morocco 2026. Mshindi wa mchezo huu wa Jumanne usiku mjini Rabat, atatangazwa kuwa bingwa mpya wa ubingwa wa mashindano hayo ambayo yamekuwa ya kusisimua, yenye mvutano mkubwa na matokeo ya kushangaza.
Fainali hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu mbili zilizoonyesha uimara mkubwa wa kiakili na uwezo wa kupambana, hasa katika nyakati ngumu kwa kipindi chote cha mashindano. Tanzania itakuwa ikisaka kutwaa taji la TotalEnergies CAF U-17 AFCON kwa mara ya kwanza katika historia yake. Senegal wataingia katika mchezo huu wakitaka kuimarisha zaidi sifa yake, kama moja ya nchi bora barani Afrika katika kukuza vipaji vya vijana wa soka.
SOMA HII PIA: Aviator game Tanzania: Ingia, Cheza, Ushinde | SportPesa
Safari ya Tanzania na Senegal Kwenda Fainali

Timu zote mbili zilifanikiwa kufuzu fainali baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti katika michezo ya nusu fainali. Mechi hizo za Nusu Fainali zilikuwa ngumu na zenye ushindani mkubwa. Hii inafanya suala fainali hiyo, kusubiriwa kwa hamu kubwa.
Tanzania imetinga fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake, baada ya kuiondoa Misri kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya mud awa kawaida. Mafanikio hayo yanaongeza rekodi nzuri ya kikosi cha Serengeti Boys, katika kampeni yao bora kabisa ya mashindano haya. Mafanikio hayo hayashangazi sana kutokana na rekodi yao ya hivi karibuni katika Mashindano ya Soka ya Shule za Afrika ya CAF, ambapo walitwaa ubingwa wa wavulana mwaka 2024 na 2025. Baadhi ya wachezaji wa kizazi hicho, sasa wanacheza katika kikosi cha U-17.
Kwa upande wa Senegal, safari yao kuelekea fainali ilikuwa ya kusisimua pia, baada ya Simba Vijana wa Teranga kuwatoa wenyeji Morocco kwa ushindi wa penalti 7-6. Hii ni kufuatia sare ya 1-1 katika mud awa ziada, mchezo uliochezwa mbele ya mashabiki wengi hususani wa wenyeji Morocco, waliokuwa na shauku mjini Rabat.
Morocco vs Egypt kusaka mshindi wa tatu

Kabla ya fainali, Morocco na Misri zitakutana katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu utakaochezwa leo Jumatatu, tarehe 1 Juni. Ni wazi mchezo huu utakuwa wa ushindani, kwani kila timu itakuwa ikisaka kumaliza mashindano kwa matokeo mazuri. Dakika 90 zitatoa mbabe huku Wamorocco wakiwa na shauku zaidi ya kuona, angalau wanaandika rekodi nzuri.
SOMA HII ZAIDI: Macau vs Tanzania Fifa Series: Live score, h2h, prediction, matokeo, ratiba na habari za timu
Ratiba ya Michezo Iliyobaki
Mchezo wa Kuwania Nafasi ya Tatu
Jumatatu, 1 Juni 2026
Morocco vs Misri
Uwanja: CMVI – T8, Rabat
Saa ya kuanza: 19:00 GMT
Fainali

Jumanne, 2 Juni 2026
Tanzania vs Senegal
Uwanja: Moulay El Hassan Stadium, Rabat
Saa ya kuanza: 19:00 GMT
SOMA HII PIA: Morocco vs Tanzania AFCON 2025: Ratiba, Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Hitimisho: Baada ya AFCON, uelekeo ni Kombe la Dunia U17

Timu zote nne zilizofika hatua ya nusu fainali pamoja na zile zilizotolewa kwenye Robo fainali, ambazo ni; Côte d’Ivoire, Cameroon, Mali na Algeria, sambamba na washindi wa mechi za mchujo Mozambique na Uganda, zimefuzu Kombe la Dunia. Timu hizo zitashiriki Kombe la Dunia la FIFA kwa Wachezaji wa Chini ya Miaka 17 (U17), litakalofanyika Qatar baadaye mwaka huu. Hivyo wana nafasi ya kuandika historia kubwa zaidi.

