- SportPesa Blog tumekusogezea ratiba ya mechi za Yanga SC Juni 2025/26 NBC Premier League na CRDB Federation
- Yanga SC ana mechi ngumu ikiwemo Azam FC vs Yanga SC, Yanga SC vs TRA United na JKT Tanzania vs Yanga SC
- Mchezo uliopita Yanga SC ilipata ushindi wa magoli 3-1 Namungo FC, Uwanja wa KMC Complex.
- Hizi ni mechi za lala salama kwa mabingwa watetezi kupambania malengo
Ratiba ya mechi za Yanga SC Juni 2025/26 Premier League na CRDB Federation Cup ni kali kwa vinara wa ligi. Mashujaa FC vs Yanga SC ni mchezao ujao Juni 13, 2026 Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Mechi 5 zimesalia kwenye ligi na kuna mchezo mmoja hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup. Wanananchi ni mabingwa watetezi taji la NBC Premier League na CRDB Federation Cup.
SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Tumekuletea ratiba ya mechi za Yanga SC Juni 2025/26

Kuna kazi kubwa kwenye ratiba ya mechi za Yanga SC Juni 2025/26 NBC Premier League kutokana na ushindani uliopo. Vinara wa ligi wamecheza mechi 25 na kukusanya pointi 60. Mchezo uliopita kwenye ligi Mei 25, 2026 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga SC 3-1 Namungo FC.
Yanga SC wanaongoza ligi wakiwa na pointi 60. Mechi 25 wamecheza wakipata ushindi katika mechi 18, sare 6 na kupoteza mchezo mmoja. Je Yanga SC wataendeleza ubabe wao ndani ya ligi?
| Tarehe | Mechi | Mashindano | Uwanja |
|---|---|---|---|
| Juni 13, 2026 | Mashujaa FC vs Yanga SC | NBC Premier League | Uwanja wa Lake Tangayika, Kigoma |
| Juni 18, 2026 | Fountain Gate FC vs Yanga SC | NBC Premier League | Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha |
| Juni 21, 2026 | Azam FC vs Yanga SC | CRDB Federation Cup | Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza |
| Juni 24, 2026 | Yanga SC vs Azam FC | NBC Premier League | Uwanja wa Azam Complex, Dar |
| Juni 27, 2026 | Yanga SC vs TRA United | NBC Premier League | Uwanja wa KMC Complex, Dar |
| Juni 30, 2026 | JKT Tanzania vs Yanga SC | NBC Premier League | Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo, Dar |

Yanga SC kukabiliana na Azam FC mara 2
Mabingwa watetezi Yanga SC watakutana na Azam FC mara 2 ndani ya Juni. Mchezo wa kwanza ni hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup na mchezo wa 2 ni NBC Premier League. Mpaka sasa wababe hawa wamekutana mara moja kwenye ligi. Mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Azam FC 0-0 Yanga SC.
SOMA HII: Deal done! Roman Folz ‘out’, kocha mpya Yanga SC huyu hapa
Hitimisho
Ukitazama ratiba ya mechi za Yanga SC Juni 2025/26 NBC Premier League na CRDB Federation Cup zinaonyesha kuwa msimu unakwenda ukingoni. Wananchi watakuwa na mechi 6 kufunga msimu na wakitinga fainali watakuwa na mechi 7. Je matokeo ya mechi zijazo yatakuaje? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa matokeo na taarifa za hivi punde.

