- Hatimaye UEFA Champions League best XI 2025/26 yaani kikosi bora cha mwaka cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kimetangazwa.
- Hii ni baada ya jana Jumamosi 30/5/2026 mashindano hayo kutamatika, huku PSG wakitetea ubingwa wao.
- Dakika 120 za Uwanja wa Puskas pale Hungary ziliisha kwa sare ya 1-1 huku matokeo ya Penalti yakiwa Paris Saint-Germain 4-3 Arsenal.
- Mastaa kama Dembele, Vitinha, Kvaratskhelia, Rice, Olise wang’aa
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), kupitia kundi la Waangalizi wa Kiufundi lao, limechagua Kikosi Bora cha Msimu wa UEFA Champions League best XI 2025/26. Hii ni baada ya jana Jumamosi 30/5/2026 mashindano hayo kutamatika, huku PSG wakitetea ubingwa wao. Dakika 120 za Uwanja wa Puskas pale hungary ziliisha kwa sare ya 1-1 huku matokeo ya Penalti yakiwa Paris Saint-Germain 4-3 Arsenal.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League 2025/26); Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu kikosi bora cha mwaka (UEFA Champions League best XI 2025/26)
Paris Saint Germain yatoa Nyota 5

Katika Kikosi hiko cha mwaka, Mabingwa watetezi Paris Saint-Germain wameingiza wachezaji 5 katika Kikosi Rasmi cha Msimu cha UEFA Champions League. Hii ikimjumuisha mchezaji bora wa msimu, Khvicha Kvaratskhelia. Staa huyo amechaguliwa nafasi yaw inga wa kushoto. Mchezaji Bora wa mechi ya Fainali, Vitinha pia amechaguliwa kuanza eneo la katikati ya uwanja.
Mastaa hao wawili wanaungana na wachezaji wenzao wa ulinzi; Marquinhos na Nuno Mendes ambao wameanza kwenye nafasi ya ulinzi wa kushoto na Katikati. Ousmane Dembélé anakamilisha idadi ya Nyota wa 5 akichaguliwa katika safu ya ushambuliaji.
SOMA HII PIA: Best Fifa Men’s 11 in 2025 – Mastaa wa PSG wateka tuzo nyingi za kikosi bora duniani mwaka huu
Arsenal yatoa Nyota 3

Wanafainali wenza, Arsenal wamefanikiwa kutoa Nyota 3 katika kikosi bora. Kipa namba moja wa Spain na Arsenal, David Raya amechaguliwa kuwa kipa wa kikosi hiko, huku kiungo wa kimataifa wa England na Arsenal Declan Rice akiingia kikosini pia. Mlinzi wa kimataifa wa Brazil, Gabriel Magalhães ambaye amekuwa gumzo, baada ya kukosa mkwaju wa mwisho wa Arsenal uliopelekea wapoteze ubingwa naye ameingia kikosini.
Bayern Munich wachezaji 2

Kikosi cha Bayern Munich ambao walitolewa na PSG kwenye Nusu Fainali, wameingiza wachezaji wawili. Nyota hao ni kiungo Mfaransa, Michael Olise na mshambuliaji wa Bayern na nahodha wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane. Nyota hao ni sehemu ya mastaa 3 ambao wamehusika na zaidi ya mabao 100 msimu huu wakiwa na Bayern.
SOMA HII ZAIDI: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics
Atletico Madrid mchezaji 1
Wana Nusu Fainali wengine Atletico Madrid ambao walitolewa na Arsenal nao wameandikisha Nyota mmoja. Marcos Llorente ndiye mchezaji pekee wa Atletico aliyeingioa katika kikosi bora cha mwaka. Ikumbukwe Nyota huyu pia anatumika katika kikosi cha timu ya Taifa ya Spain.
Hiki hapa Kikosi Bora cha Msimu (UEFA Champions League 2025/26 Best XI)

Kipa
David Raya (Arsenal)
Mabeki
Marcos Llorente (Atlético de Madrid)
Marquinhos (Paris Saint-Germain)
Gabriel Magalhães (Arsenal)
Nuno Mendes (Paris Saint-Germain)
Viungo
Michael Olise (Bayern München)
Declan Rice (Arsenal)
Vitinha (Paris Saint-Germain)
Khvicha Kvaratskhelia (Paris Saint-Germain)
Washambuliaji
Ousmane Dembélé (Paris Saint-Germain)
Harry Kane (Bayern München)
SOMA HII PIA: ENGLISH FOOTBALL Clash of Titans: PSG vs Barcelona in the UEFA Champions League Quarter-Finals
Hitimisho
Ukiachana na kikosi bora (UEFA Champions league best XI 2025/26), baadhio ya mastaa pia wameshinda tuzo mbalimbali. Nyota wa Real Madrid, Arder Guller ametajwa kuwa mchezaji bora mdogo wa mashindano hayo. Je, hali itakuwaje msimu ujao? Muda utaamua kwa kudra za Mungu.

