Robo Fainali CRDB Federation CupRobo Fainali CRDB Federation Cup
  • Huu hapa muonekano wa matokeo ya droo ya Robo Fainali CRDB Federation Cup baada ya uchambuzi kukamilika leo.
  • Kufuatia droo hiyo timu zitakazovaana ni Simba SC vs TRA United, JKT Tanzania vs Yanga SC, Mashujaa FC vs Azam FC na Coastal Union vs Singida BS.
  • Robo Fainali hii itazikutanisha timu 8 ambazo ni; Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida BS, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union.
  • Fuatilia michezo yote ya CRDB Federation Cup ikiwemo taarifa mpya, droo, matokeo na takwimu kupitia SportPesa blog.

Matokeo ya droo ya Robo Fainali CRDB Federation Cup hatimaye yajulikana baada ya kukamilika kwa droo ya mashindano hayo. Robo Fainali hii ya wakubwa itazikutanisha timu 8 ambazo ni; Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida BS, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union. Droo hii itakuwa ni baina ya Simba SC vs TRA United, JKT Tanzania vs Yanga SC, Mashujaa FC vs Azam FC na Coastal Union vs Singida BS. Makala hii inakuchambulia kwa ufupi droo hiyo kwa ujumla.

Unaweza kufuatilia mwenendo wa mashindano ya CRDB Federation Cup na taarifa ya mechi za Robo Fainali, mabao, takwimu na habari za papo hapo kupitia SportPesa Blog.

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge
SportPesa Aviator Challenge

Ratiba ya mechi za Robo Fainali ya CRDB Confederation Cup

Baadhi ya viongozi wa timu zilizofika Robo Fainali na wadau wakifuatilia
Baadhi ya viongozi wa timu zilizofika Robo Fainali na wadau wakifuatilia

Hii ndo michezo ya Robo Fainali ya CRDB Federation Cup;

MechiTimu ya NyumbaniTimu ya UgeniniMaelezo Mafupi
Simba SC vs TRA UnitedSimba SCTRA UnitedSimba wanatarajiwa kutumia ubora wao wa kikosi dhidi ya TRA United wanaopambana kujijenga.
JKT Tanzania vs Yanga SCJKT TanzaniaYanga SCYanga wanaingia wakiwa na nguvu kubwa, huku JKT wakisaka matokeo ya kushangaza nyumbani.
Mashujaa FC vs Azam FCMashujaa FCAzam FCAzam wanaonekana kuwa na nafasi nzuri, lakini Mashujaa wanaweza kutoa ushindani mkali.
Coastal Union vs Singida BSCoastal UnionSingida BSMchezo unaotarajiwa kuwa wa ushindani, huku kila timu ikihitaji pointi muhimu.

Mechi hizi za Robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB zimepangwa kupigwa Mei 16 na Mei 17, mwaka huu. Hii ina maana mechi mbili za Robo Fainali ya kwanza zitapigwa Mei 16, na zile za 2 zitapigwa Mei 17. Katika michezo hiyo timu za Simba SC, JKT Tanzania, Mashujaa FC na Coastal Union zitakuwa Uwanja wa nyumbani. Timu za Yanga SC, Azam FC, Singida BS na TRA United zitakuwa ugenini.

Simba SC vs TRA United

Hii ni mara ya kwanza Simba SC vs TRA United zinakutana katika mashindano ya CRDB Federation Cup, ambapo Simba SC watakuwa wenyeji kwenye Uwanja wa Nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo. Timu hizi zimekutana mara mbili katika mashindano ya Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), msimu huu ambapo Simba wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja na mchezo mmoja umeisha kwa suluhu. Mshindi wa mchezo huu atakuwa amekata tiketi ya Nusu Fainali.

JKT Tanzania vs Yanga SC

JKT Tanzania vs Yanga SC ni safu nyingine ya timu ambazo zinakutana kwa mara ya kwanza katika mashindano ya CRDB Federation, lakini zina historia pana ya kukutana kwenye mashindano ya Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Katika h2h ya NBC timu hizi zimekutana mara 19, Yanga SC wameshinda mechi 14, JKT haijawahi kupata ushindi. Michezo 5 iliyosalia iliisha kwa matokeo ya sare. Mabao 47 yamefungwa walipokutana, ambapo Yanga SC imefunga mabao 44, na JKT Tanzania mabao 3.

Mashujaa FC vs Azam FC

Mashujaa FC vs Azam FC ni mchezo mwingine mgumu wa Robo Fainali ya CRDB Federation Cup. Hii inathibitisha na takwimu zilizorekodiwa za mikutano yao. Kwa ujumla Azam FC wameandikisha ushindi wa mechi 2, huku Mashujaa FC wakiwa bado hawajaonja ladha ya ushindi. Mechi 3 katika mikutano yao zimeisha kwa matokeo ya sare.

Coastal Union vs Singida BS

Coastal Union vs Singida BS ni vita nyingine ya kusaka tiketi ya Nusu Fainali. Timu hizi zinakutana kwa mara ya kwanza kwenye mashindano haya ya CRDB Federation Cup. Kwenye historia ya h2h yao kwenye NBC Premier League wamekutana mara 9. Coastal Union wameshinda mechi 4, huku Singida Big Stars wao wakishinda mechi 3. Mechi 2 zilizosalia ziliisha kwa matokeo ya sare.

Hitimisho

Robo Fainali ya CRDB Federation inatarajiwa kuwa ya kuvutia kutokana na ubora wa timu shindani. Wote tumeshuhudia ushindani mkali wa baadhi ya mikutano ya hizi timu kwenye Ligi Kuu ya NBC. Baadhi ya mechi kama Simba SC vs TRA United zimetoa matokeo ya kushangaza msimu huu, Yanga SC vs JKT Tanzania pia walitoana jasho vilivyo. Endelea kufuatilia taarifa za papo kwa papo kuhusu mashindano ya CRDB Federation Cup kupitia SportPesa blog, ili kujua mwenendo mzima.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.