- Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kupisha hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya CRDB Federation Cup, itakayopigwa wikiendi hii.
- Habari kubwa leo Mei 15, 2026ni Yanga SC kutangaza mkataba wa makubaliano, ya ujenzi wa uwanja wao mpya wa mechi.
- Yanga SC wanajenga Uwanja huo kwa makubaliano ya kiuwekezaji na Kampuni ya GSM ya 50/50.
- Mpaka sasa kuna timu 6 tu, zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo zinamiliki viwanja vyao vya mechi, makala hii inakuchambulia.
Uongozi wa klabu ya Yanga SC leo Mei 15, 2026 wametangaza kutia saini mkataba wa makubaliano, ya ujenzi wa uwanja wao mpya. huo. Ikiwa Yanga SC watafanikiwa kukamilisha ujenzi wa Uwanja huo, utakaojengwa kwa makubaliano ya kiuwekezaji na Kampuni ya GSM basi itakuwa timu ya 7 kufikia mafanikio hayo. Mpaka sasa kuna timu 6 tu, zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo zinamiliki viwanja vyao. Makala hii inakuchambulia.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Timu 6 zinazomiliki viwanja vyao Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)
Azam FC – Azam Complex

Azam ni miongoni mwa timu za awali kuleta mapinduzi makubwa ya kiuwekezaji hususani viwanja. Azam walizindua Uwanja wao wa mechi za Ligi Kuu uliopewa jina la Azam Complex kati ya mwaka 2009-13, uwanja huo umefanyiwa maboresho makubwa mara kadhaa. Uwanja wa Azam Complex una viwango vya kimataifa, kiasi cha kuruhusiwa mara kadhaa kutumika kwa mashindano ya CAF ukikadiriwa kuchukua watu 10,000.
SOMA HII PIA: Ligi Kuu ya Bara fixtures, results, scores and stats
JKT Tanzania – Meja Jenerali Isamuhyo
Miongoni mwa viwanja vilivyofanyiwa maboresho makubwa hivi karibuni. Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam, ulifanyiwa marekebisho ya uwekaji wa taa za michezo ya usiku mwezi Septemba 30, 2025. Uwanja huu una uwezo wa kubeba mashabiki 8,000 na umekuwa ukiruhusiwa kuandaa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Mechi ya Ligi Kuu ya NBC ya Kariakoo Derby Mei 3, 2026 ilipigwa kwenye Uwanja huu na mchezo kuisha Simba SC 2-2 Yanga SC.
Singida Black Stars – Airtel Stadium

Baada ya kutumia Uwanja wa CCM Liti kwa muda, klabu ya Singida Black Stars ilizindua rasmi uwanja wake mpya wa kisasa wa Airtel Stadium, uliopo eneo la Mtipa mkoani Singida tarehe 24 Machi 2025. Katika tukio la uzinduzi mgeni rasmi alikuwa, Naibu Waziri wa Utamaduni, sanaa na michezo, Hamisi Mwinjuma (Mwana FA). Mechi ya Ufunguzi ilizikutanisha Singida Black Stars, ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga SC kusindikiza uzinduzi huo. Ni uwanja wa kisasa uliokamilika kwa mashindano rasmi ya kitaifa.
SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC
KMC – KMC Complex

Huu ni Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni. Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam ulifunguliwa rasmi kwa mechi za Ligi Kuu ya NBC tarehe 17 Septemba 2025. Katika sherehe hizo, mchezo wa ufunguzi ulichezwa kati ya wenyeji KMC FC dhidi ya Dodoma Jiji FC. Mbali na KMC FC, uwanja huo pia ni Uwanja wa nyumbani kwa klabu za Simba SC na Yanga SC.
Namungo – Uwanja wa Majaliwa

Huu ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Namungo, ufunguzi rasmi wa uwanja huu uliopo Ruangwa mkoani Lindi, ulifanyika tarehe 11 Septemba 2022. Ufunguzi huo ulifuatia maboresho makubwa ya kuweka nyasi za kisasa, na majukwaa mapya. Serikali kwa ushirikiano na wadau ilifanya ukarabati mkubwa uliogharimu fedha nyingi, ili kufikia viwango vya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na CAF. Sherehe rasmi za ufunguzi wa muonekano mpya ziliongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya ukarabati kufikia zaidi ya asilimia 98.
Mtibwa Sugar
Kwa sasa wameutangaza Uwanja wa Jamhuri Morogoro kuwa Uwanja wao wa nyumbani, hii ni baada ya marekebisho yaliyofanywa kwenye Uwanja huo. Kabla ya hapo walikuwa wakitumia uwanja wa Jamhuri Dodoma. Ikumbukwe Mtibwa Sugar pia wanamiliki Uwanja wa Manungu.
SOMA HII PIA: Ligi Kuu Bara table & standings
Hitimisho
Maendeleo ya soka yanatemea sana uwekezaji katika miundombinu, taarifa za kuanza kwa ujenzi wa Uwanja mpya wa Yanga SC ni Habari njema. Hii inaonyesha dhamira ya wazi ya Uongozi wa timu hiyo kuleta mapinduzi ya kisoka. Yanga SC inafuata hatua kwa timu hizi 6 zilizotangulia, ni mfano bora kwa wengine kuiga.

