- Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said ameongoza Mkutano Maalum, wa Kamati ya Utendaji kujadili kuhusu mradi wa Uwanja.
- Ujenzi Uwanja wa Yanga SC ni ahadi kuu ya uongozi wa Hersi ambayo mpaka sasa haijatimizwa.
- Katika hali inayoonekana kuwa uongozi wa Yanga umepania kujenga uwanja, tayari Bilioni 1 imetengwa kwa maandalizi.
Mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC umezidi kushika kasi. Mara baada ya kukamilisha mchakato wa hati ya eneo la Jangwani, uongozi wa Yanga SC umefanya kikao Kizito. Kikao hiko kikiwa na lengo la kujadili mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja. Kkikao hiko kiliongozwa na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kuhusu ujenzi Uwanja wa Yanga SC
Taarifa rasmi kutoka Yanga SC iliyochapishwa kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii ilieleza: “Rais wa Klabu ya Young Africans SC, Eng. Hersi Said leo asubuhi ameongoza Mkutano Maalum, Mkutano huu ni wa Kamati ya Utendaji kujadili kuhusu mradi wa Uwanja. Mkutano huu umefanyika Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani jijini Dar Es Salaam.
“Mkutano huo ulihudhuriwa ana kwa ana na wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, isipokuwa wawili ambao walijiunga kwa njia ya mtandao. Wawili hao ni Makamu wa Rais, Arafat Haji na Mjumbe Mhe. Seif Gulamali walishiriki kwa njia ya mtandao. Hii ni kutokana na kuwa na changamoto za majukumu.
SOMA HII PIA: Yanga SC 1-0 Bandari FC kilele Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Mkapa | Highlights, goli, rekodi muhimu
Safari ilianzia Super Dome mkutano mkuu wa mwaka 2025
Sakata hili ni ahadi ya muda mrefu ya Rais Hersi ambayo bado haijatimizwa. Hivi karibuni kupiti mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Super Dome, Serikali ilitoa ahadi ya kukamilisha mchakato wa hati ya Uwanja huo ndani ya wiki 2. Jambo hili limewapa mashabiki wa Yanga matumaini makubwa kukamilisha jambo hilo.
Hati yakabidhiwa Uwanja wa Mkapa

Katika tukio ambalo limevuta hisia za mashabiki wengi wa Yanga, ni kukabidhiwa kwa hati yao ya eneo la uwanja. Tukio hilo lilifanyika kwenye kilele cha wiki yam wananchi, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
SOMA HII ZAIDI: Injinia Hersi anaondoka au bado yupo Yanga? Mwenyewe afunguka mazito ishu ya siasa
Bilioni 1 yatengwa kuanza hatua za awali za ujenzi
Yanga SC kupitia kwa makamu mwenyekiti wao, Arafat Haji wameweka wazi kuwa kwa kuanza wameandaa Bilioni 1 kwa ajili za hatua za awali za ujenzi. Ikumbukwe mradi huo wa ujenzi wa Uwanja wa Yanga SC unafanywa kwa mashirikiano na Serikali, ambayo ina mradi mkubwa wa mto Msimbazi.
Bajeti kuu ya msimu 2025/26 ni Bilioni 33.4

Ikumbukwe bajeti ya Bilioni 1 ya maandalizi ya ujenzi wa awali ni miongoni mwa hoja ya bajeti iliyoshtua, kutoka kwenye taarifa ya fedha ya Yanga SC. Ikumbukwe bajeti ya Yanga kwa msimu uliopita wa 2024/25 ilikuwa Bilion 25, ambapo baada ya matumizi walibakiwa na bakaa ya milion takribani 300m. Kuelekea msimu wa 2025/26, Yanga SC imepanga bajeti ya Tsh Bilioni 33.4 hii ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi Bilioni 8. Kama ilivyo kawaida Ripoti ya fedha ilitolewa na makamu Rais, Arafat Haji.
SOMA HII ZAIDI: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26: Straika mpya Yanga huyu hapa, Chama ‘Out’
Usajili wa Bilioni 7 msimu mpya wa 2025/26

Sehemu nyingine ya taarifa ya kifedha, ambayo ilisomwa na kuidhinishwa na viongozi wa Wanachama wa Yanga, kupitia mkutano mkuu ni makadirio ya kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kwenye usajili ndani ya msimu huu mpya. Ikumbukwe tayari fedha hiyo imeanza kutumika kusajili mastaa wapya, na kuongeza mikataba wale waliokuwepo.
Miradi tanzu ya baadaye, inayoendana na ujenzi wa uwanja Yanga SC
Ukiachana na mradi wa ujenzi wa uwanja, uongozi wa Yanga SC umetangaza mipango yao mizito ya baadae. Kati ya miradi hiyo ni suala la kukuza soka la vijana na Wanawake. Kwa sasa uongozi unatazama hilo kama fursa ya kibiashara kuuza wachezaji nje ya nchi. Pamoja na hayo uongozi wat imu hiyo pia umeweka wazi mipango ya kuimarisha timu hiyo kiuchumi. Hii ni katika mkakati wa kuongeza mapato kupitia usajili wa wanachama na wateja wapya, pamoja na wadhamini wapya.
Hitimisho
Mipango hii ya muda mrefu ya Ujenzi Uwanja wa Yanga SC inadhihirisha uthabiti wa Yanga SC kuwa klabu bora na endelevu. Pia hii inaelezea utashi wa kuhakikisha wanachama wanashirikishwa, usawa wa kifedha na kuwa mstari wa mbele kwa miundombinu. Hii ni katika kukuza soka la bongo.

