- Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Spain inazidi kupamba moto.
- Leo Jumapili utapigwa mchezo mkali wa Madrid derby, kati ya Real Madrid vs Atletico Madrid ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.
- Real Madrid wakisaka kuwakaribia zaidi Barcelona kileleni, na kulipa kisasi cha kuchapwa 5-2 na Atletico kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza?
Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Spain inaendelea tena leo Jumapili. Mchezo mkali wa Madrid derby, kati ya Real Madrid vs Atletico Madrid ndio unasubiriwa kwa hamu kubwa. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, matokeo yoyote ya mchezo huu yatatoa taswira ya mbio za ubingwa. Je, Real Madrid watalipa kisasi cha kuchapwa 5-2, mchezo wa mkondo wa kwanza?
SOMA HII PIA: Real Madrid vs Atletico Madrid: 1 Epic Clash of Madrid Titans in La Liga
Hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Real Madrid vs Atletico Madrid, H2H

Katika historia ya ‘Madrid Derby’ timu hizi zimekutana katika michezo 304, ambapo Real Madrid wameshinda mechi 155. Atletico Madrid wao wameshinda mechi 76, huku michezo 73 ikiisha kwa matokeo ya sare. Hivyo mchezo huu unakwenda kuandika rekodi mpya kati ya wababe hawa.
Vikosi vinavyotarajiwa Real Madrid vs Atletico Madrid
Real Madrid:

Kipa: Lunin
Walinzi: Alexander-Arnold, Rudiger, Huijsen, Carreras
Viungo: Camavinga, Tchouameni, Valverde, Guler
Washambuliaji: Mbappe, Vinicius
Atletico Madrid:

Kipa: Musso
Walinzi: Molina, Pubill, Hancko, Ruggeri
Viungo: Simeone, Llorente, Cardoso, Lookman
Washambuliaji: Sorloth, Alvarez
SOMA HII ZAIDI: La Liga Table 2025/26
Habari za timu

Moja ya mechi kubwa itapigwa katika dimba la kifahari la Santiago Bernabeu, ambapo Real Madrid watakuwa wanasaka kulipa kisasi kwa mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid. Real Madrid kwa sasa wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga, wakiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya vinara Barcelona. Atletico wapo nafasi ya tatu, pointi tisa nyuma ya wapinzani wao wa jiji.
Kikosi cha Alvaro Arbeloa kina rekodi ya ushindi mara 21, sare tatu na vipigo vinne katika mechi 28 za ligi msimu huu. Kati ya ushindi huo mara 21, Madrid wameshinda mechi 12 nyumbani kati ya 14 walizocheza Santiago Bernabeu. Ari ya kikosi ni kubwa hasa wakiwa wanaingia kwenye mechi hii,baada ya ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya Man City katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Real wanapigania kutwaa mataji mawili (La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya), huku pia wakitaka kulipiza kisasi dhidi ya Atletico baada ya kufungwa 5-2 walipokutana mzunguko wa 1.
Atletico, wamekuwa na mwenendo wa panda shuka kwenye matokeo yao msimu huu. Mechi nne kati ya sita zilizopita za ligi kati ya timu hizi zimeisha kwa sare. Ikumbukwe Real Madrid hawajawafunga Atletico katika La Liga wakiwa Bernabeu tangu Desemba 2021.
Atletico pia wanapigania mataji mawili, baada ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, licha ya kufungwa 3-2 na Tottenham katika mechi ya marudiano. Watakutana na Barcelona katika hatua hiyo. Pia wako kwenye fainali ya Copa del Rey, ambapo watacheza na Real Sociedad Aprili 18.
Taarifa ya majeraha vikosini
Real Madrid

Real Madrid watamkosa Eder Militao (misuli ya paja), Dani Ceballos (ndama), Rodrygo (goti) na Thibaut Courtois (paja). Hata hivyo, Ferland Mendy, David Alaba na Raul Asencio wanaweza kurejea kikosini, huku Jude Bellingham akiwa tayari kucheza baada ya kupona jeraha. Kylian Mbappe pia anatarajiwa kuanza pamoja na Vinicius Junior, kwenye safu ya ushambuliaji. Alvaro Carreras naye anaweza kuanza upande wa kushoto wa ulinzi.
Atletico Madrid
Kwa upande wa Atletico, Pablo Barrios na Rodrigo Mendoza wote ni majeruhi, huku Jan Oblak akiwa na shaka kutokana na tatizo la nyonga. Marc Pubill anaweza kurejea katika safu ya ulinzi, huku Alexander Sorloth akipewa nafasi ya kuanza mbele, na Antoine Griezmann akianza benchi. Julian Alvarez ataendelea kuwa mchezaji muhimu, akilenga kuongeza idadi ya mabao yake 17 aliyofunga msimu huu.
Hitimisho na Utabiri
Real Madrid vs Atletico Madrid ni zaidi ya mechi, hii ni vita ya pointi 3 ngumu za dabi ambazo zinakwenda kutoa taswira yam bio za ubingwa. Kurejea kwa Mbappe na Jude ni faida kubwa kwa Real Madrid, na kikosi cha Arbeloa kina uwezo wa kupata ushindi muhimu katika dabi hii ngumu. Japo hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ugumu wa kikosi cha Simeone, lakini Real Madrid anapewa nafasi kubwa ya ushindi.

