- Mchezo wa mwisho wababe hawa kucheza Uwanja wa Sokoine ubao ulisoma Mbeya City 3-3 Yanga SC.
- Yanga SC vs Mbeya City burudani ya soka inakwenda kushuhudiwa katika dakika 90 ndani ya NBC.
- Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC na Malale Hamsini Kocha Mkuu wa Mbeya City wapigiana hesabu kali.
Yanga SC vs Mbeya City mchezo mkali wa ligi ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Matokeo ya 2022/23 wakati Mbeya City inashuka daraja yalikuwa yakushangaza. Ubao ulisoma Mbeya City 3-3 Yanga SC wakigawana pointi mojamoja. Huu unakuwa mchezo wa kwanza baada ya Mbeya City kurejea kwenye ligi ya NBC.
SOMA HII: SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7 kupitia Ofa kubwa ya kihistoria
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda wa kupaisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni. Rahisi sana na hakuna longolongo kwenye hili. Cheza Aviator sasa upate mgao wako.

Yanga SC vs Mbeya City H2H

Yanga SC vs Mbeya City zipo rekodi zao mechi tano zilizopita ndani ya NBC. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Mbeya City ilishuka daraja. Imerejea ndani ya ligi kwa mara nyingine 2025/26.
| 13/02/2021 | Mbeya City 1-1 Yanga SC |
| 05/02/2022 | Yanga SC 0-0 Mbeya City |
| 25/06/2022 | Mbeya City 1-1 Yanga SC |
| 26/11/2022 | Yanga SC 2-0 Mbeya City |
| 6/6/2023 | Mbeya City 3-3 Yanga SC |
Mbeya City wakiwa nyumbani wagumu
Mechi 5 sare 4. Katika hizo 3 Mbeya City walikuwa nyumbani na moja ugenini. Yanga SC wamekuwa imara kupata matokeo mbele ya Mbeya City wakiwa nyumbani.
Mechi tano za Mbeya City za hivi karibuni

Fountain Gate 0-1 Mbeya City, ligi.
Azam FC 2-0 Mbeya City, ligi.
Mbeya City 1-1 Namungo FC, mchezo wa kirafiki.
Mtibwa Sugar 1-0 Mbeya City, mchezo wa kirafiki.
Mbeya City 0-2 Azam FC, mchezo wa kirafiki.
Safu ya ushambuliaji ya Mbeya City inaonekana haijawa imara. Katika mechi 5 ni magoli 2 ilifunga. Safu ya ulinzi imeruhusu magoli 6.
SOMA HII: Young Africans SC vs Wiliete SC CAFCL 27 Sept 2025: live score, Takwimu, vikosi, H2H, Utabiri

Mechi tano za Yanga SC hivi karibuni
Yanga 1-0 Bandari ya Kenya, (mechi ya kirafiki).
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC imekuwa imara kwenye eneo la ushambuliaji. Katika mechi tano imefunga jumla ya magoli 10. Safu ya ulinzi haijaruhusu goli ndani ya uwanja.
Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa dhidi ya Mbeya City

Mlinda mlango
Djigui Diarra
Mabeki
Kibwana Shomari
Ladack Boka
Bakari Nondo
Ibrahim Bacca
Viungo
Aziz Andambilwe
Maxi Nzengeli
Duke Abuya
Mudathir Yahya
Pacome Zouzoua
Mshambuliaji
Andy Boyel
SOMA HII: Yanga SC inawadai Simba SC 2024/25

Kikosi cha Mbeya City kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Yanga SC
Mlinda mlango
Beno Kakolanya
Walinzi
Ibrahim Ame
David Mwasa
Kelvin Kingu
Viungo
Yahya Mbegu
Habib Kyombo
Omary Chibada
Radilly Buha
Matheo Anthony
Washambuliaji
Vitalisy Mayanga
Riphat Msuya
Malale Hamsini Kocha wa Mbeya City kuhusu mchezo
“Utakuwa ni mchezo mgumu kwa kuwa tunakutana na mabingwa watetezi uwanjani. Tunamshukuru Mungu tupo salama baada ya kutoka Dar kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Maadalizi kiujumla yapo vizuri na tunaamini tutapata matokeo kwenye mchezo wetu.
Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC kuhusu mchezo
“Tunazidi kuimarika taratibu kutokana na mechi ambazo tunacheza. Ninaona kuna maoni ambayo yanatolewa hilo ni jambo zuri wachezaji wanazidi kuwa imara. Mchezo wetu ujao ni muhimu ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri,”.
Hitimisho
Yanga SC vs Mbeya City saa 10:00 jioni wanaume watakuwa uwanjani. Utakuwa ni mchezo wa tatu kwa wenyeji Mbeya City ukiwa wapili kwa Yanga SC. Kutokana na Yanga SC kuwa katika mwendelezo wa ushindi anapewa nafasi kubwa kupata matokeo katika mchezo huo.


