Simba SC imetinga robo fainali CRDBSeleman vs Dodoma Jiji FC
  • Simba SC (3) vs Dodoma Jiji FC (1) CRDB Federation Cup
  • Mshambuliaji wa Simba SC Seleman Mwalimu afunga magoli mawili dakika ya 54 na 57.
  • Clatous Chama aulainisha mchezo kipindi cha pili Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha

Simba SC (3) vs Dodoma Jiji FC (1) matokeo rasmi kwenye CRDB Federation Cup Aprili 12, 2026. Khleffin Hamdoun alianza kufunga goli kwa Dodoma Jiji FC dakika ya 9. Goli hilo lilidumu mpaka dakika ya 54 likisawazishwa na Seleman Mwalimu aliyefunga mawili lingine dakika ya 57. Clatous Chama alilainisha mchezo alipotoa pasi ya goli kwa Anicet Oura dakika ya 60.

SOMA HII: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Simba SC (3) vs Dodoma Jiji FC (1) CRDB Federation Cup

Simba SC imetinga robo fainali CRDB
Clatous Chama vs Dodoma Jiji FC.

Simba SC (3) vs Dodoma Jiji FC (1) CRDB Federedation Cup. Mnyama alipindua mezakipindi cha pili baada ya Djibr Kassali kuanza kufungwa dakika ya 9. Khleffin Hamdoun wa Dodoma Jiji FC alifungua ukurasa wakufunga magoli kwenye mchezo huo. Nickson Kibabage alianza kutoa pasi ya goli la kwanza kwa Seleman Mwalimu.

Dodoma Jiji FC walishuhudia magoli matatu kipindi cha pili. Matokeo hayo yanaifungashia virago timu hiyo hatua ya 16 bora. Mnyama anaungana na timu 8 ambazo zimekata tiketi hatua ya robo fainali.

Singida Black Stars 5-1 Mbeya City

Aucho
Khalid Aucho wa Singida Black Stars.

Singida Black Stars 5-1 Mbeya City magoli ya Khalid Aucho dakika ya 16, Lamine Jarjou dakika ya 58. Ibrahim Imoro dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 78,  Horso Mwaku dakika ya 66. Goli la Mbeya City limefungwa na Daniel William dakika ya 81. Ni ushindi mkubwa kwa wenyeji ndani ya dakika 90. Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Airtel, Aprili 12, 2026.

SOMA HII: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Namungo FC 0-2 TRA United

Namungo FC 0-2 TRA United magoli yakifungwa na Ally Ng’anzi dakika ya 12, Denis Nkane dakika ya 58. Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Majaliwa. Kiungo wa TRA United, Mzamiru Yassine amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, Aprili 12, 2026.

Azam FC 4-0 Fountain Gate FC

Azam FC 4-0 Fountain Gate FC, CRDB Federation Cup, magoli yakifungwa na Jephte Kitambala dakika ya 15, Abah Abel dakika ya 21. Asharafu Kibeku dakika ya 81 na Alobogast Kyobya dakika ya 90, Uwanja wa Azam Complex. Matajiri walifunga magoli mawili kila kipindi, Aprili 12, 2026.

Mabingwa watetezi wawafungashia virago TMA Stars

Simba SC imetinga robo fainali CRDB
Yanga SC kwenye moja ya mchezo wa ushindani 2025/26.

Yanga SC 1-0 TMA Stars. Goli la ushindi likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 69. Uwanja wa KMC Complex, Aprili 11, 2026. Maxi alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.

Coastal Union 2-0 Pamba Jiji FC

Coastal Union 2-0 Pamba Jiji FC magoli yakifungwa na Gradi Lassa Kisala dakika ya 30 na Ally Msangi dakika ya 35. Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Aprili 11, 2026. Msangi alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.

Mashujaa FC yatinga kwa mikwaju ya penati

 Aprili 10, 2026: Geita Gold FC 0-0 Mashujaa FC Pen: (2-4)

Aprili 10, 2026: JKT Tanzania 3-0 Mbuni FC

Orodha ya timu ambazo zinawania ubingwa

Ijue orodha ya hivi punde kwa timu zilizotinga hatua ya robo fainali zikiwania ubingwa wa CRDB Federation Cup. Ni Yanga SC hawa wanamiliki taji kwa sasa. Wametwaa taji hilo mara nne mfululizo.

Yanga SC

Coastal Union

Azam FC

TRA United

Singida Black Stars

Simba SC

Mashujaa

JKT Tanzania

SOMA HII: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Hitimisho

Simba SC (3) vs Dodoma Jiji FC (1) CRDB Federation Cup. Inaungana na timu nyingine 7 kufikisha jumla ya timu 8 hatua ya robo fainali. Bingwa mtetezi ni Yanga SC. Nani atatwaa taji hili 2026?

Share this: