- EPL itaendelea tena leo Jumamosi kwa mechi kali na ya kukata na shoka.
- Hii ni mechi ya wababe Manchester United vs Chelsea, ni vita ya jiji la Manchester dhidi ya London.
- Rekodi ya mechi 5 za hivi karibuni kati ya timu hizi mbili inaonyesha hakuna mbabe.
- Katika mechi hizo 5, Man Utd wameshinda mechi 2, Chelsea nao wameshinda mechi 2, huku mchezo mmoja ukienda sare.
Presha inazidi kupanda kwa kocha mkuu wa Man United, Ruben Amorim. Hii ni kutokana na mchezo mgumu ambao unaweza kuamua hatima yake, mechi ya Manchester United vs Chelsea. Ikumbukwe ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Burnley, kabla ya mapumziko ya kimataifa unabaki kuwa ushindi wake pekee msimu huu.
SOMA HII PIA: Manchester City vs Manchester United 14/09/2025: Manchester Derby h2h, vikosi, utabiri Highligts
Unahitaji pesa? Shinda mamilioni ya kindege ‘Aviator’ cha SportPesa sasa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani Aviator ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda sasa kirahisi kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu mechi ya Manchester United vs Chelsea

Huu ni mchezo wa tano wa EPL kwa timu hizi, ambapo Mashetani wekundu wanauendea mchezo huu, wakuwa na kumbukumbu mbaya tangu kuanza kwa msimu. Mpaka sasa United wamepoteza michezo mitatu msimu huu, dhidi ya Arsenal, Grimsby Town na mahasimu wao wa jiji Manchester City. Hali hii inaleza kumweka katika wakati mgumu kocha Amorim.
Ni wazi kumekuwa na dalili za maboresho ya kikosi cha United msimu huu, lakini zimezimwa haraka na makosa binafsi na matokeo yasiyoridhisha. Sasa wanahitaji sana mwamko mpya, kufuatia kipigo kutoka kwa City. Kipigo hicho kimewafanya kuwa na hali duni ya kujiamini katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Old Trafford.
Chelsea watakuwa na hamu ya kuokota pointi kwa United licha ya uchovu walionao, kufuatia ushiriki wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chelsea wanauendea mchezo huu wakitoka kwenye kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich.
Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca bado ana imani kuwa kikosi chake kitaweza kurejea kwenye ushindi baada ya mechi mbili bila ushindi. Kipigo dhidi ya Bayern kikifuata sare ya wiki iliyopita dhidi ya Brentford. Chelsea bado hawajafungwa katika mechi za ligi ya ndani, na wanaingia kwenye mechi hii wakipewa nafasi kubwa zaidi.
SOMA HII ZAIDI: Tottenham 1-0 Manchester United mabingwa wa Europa League wapatikana, ukame wa miaka 17 wafutwa
Dondoo muhimu za mchezo kwa ufupi:
Mahali: Manchester, Uingereza
Uwanja: Old Trafford
Tarehe: Jumamosi, Septemba 20
Refarii: Peter Bankes
VAR: Craig Pawson
Mechi 5 h2h hakuna mbabe
Rekodi ya Mechi za 5 za hivi karibuni kati ya timu hizi mbili inaonyesha hakuna mbabe kwani; Man Utd wameshinda mechi 2, Chelsea nao wameshinda mechi 2, huku mchezo mmoja ukiisha kwa matokeo ya sare. Mechi ya mwisho kuzikutanisha timu hizi kwenye Ligi Kuu England Chelsea walishinda 1-0 Man Utd Mei 16, 2025.
Cunha, Mount waongeza nguvu

Taarifa ambazo zimethibitishwa na uongozi wa Man United ni kuwa kiungo mshambuliaji wao, Matheus Cunha atarejea kikosini. Hii ni baada ya nyota huyo kukosa mchezo dhidi ya City iliyopita kutokana na majeraha. Kocha Amorim amethibitisha pia kuwa kiungo mshambuliaji mwingine, Mason Mount naye amerejea kikosini.
Hata hivyo, Amorim ataendelea kuwakosa walinzi wake watatu: Diogo Dalot, Lisandro Martínez na Tyrell Malacia. Dalot hajacheza tangu kipindi cha mechi za kimataifa. Martínez yuko karibu kurudi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi saba, lakini bado hajawa tayari. Malacia, ambaye hakuweza kuhamia klabu nyingine majira ya kiangazi, bado anarejea taratibu katika hali nzuri ya mwili.
SOMA HII PIA: Man United vs Arsenal ‘live’ Old Trafford: Vikosi, Utabiri, Habari za timu.
Kikosi Kinachotarajiwa cha Man Utd dhidi ya Chelsea
Muundo: 3-4-2-1
Wachezaji:
Bayındır; Yoro, De Ligt, Shaw; Mazraoui, Casemiro, Fernandes, Dorgu; Mbeumo, Amad; Šeško.
Garnacho kuongoza jeshi la Chelsea Old Trafford

Nyota wa zamani wa United aliyejiunga na Chelsea, Alejandro Garnacho amethibitishwa na kocha wake mpya, Maresca kuwa yuko tayari kuanza mechi hii. Nyota huyo anatarajiwa kukumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Man United. Chelsea pia inatarajia kuwakosa: Dário Essugo, Liam Delap na Levi Cowlill. Wakati huo huo, Roméo Lavia na Benoît Badiashile wako mashakani.
Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa dhidi ya Man Utd

Muundo: 4-2-3-1
Wachezaji:
Sánchez; James, Fofana, Chalobah, Cucurella; Caicedo, Fernández; Estêvão, Palmer, Garnacho; Pedro.
Hitimisho: Utabiri wa Matokeo
Man Utd vs Chelsea ni miongoni m,wa michezo migumu katika historia ya soka la England. Hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Hali ya sasa ya United inatoa shinikizo kubwa na linaweza kuwazidi wachezaji wa Amorim.
Chelsea pia hawako kwenye msimamo wa kiwango bora sana, lakini wanabaki kuwa timu bora katika mchezo huu. Hii ni kwa kuwa wana kikosi bora zaidi na kina upana mkubwa kuliko United. Wanazo silaha za kushambulia, ambazo zinaweza kupenya safu ya ulinzi ya United ambayo bado haijapata clean sheet msimu huu.
Amorim alifungwa kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea mwezi Mei, na huenda hali hiyo ikajirudia Jumamosi hii.

