Germany vs GhanaGermany vs Ghana
  • Leo Jumatatu mechi nyingine bora ya kimataifa ya kirafiki itapigwa katika Uwanja wa MHPArena.
  • Ni Germany vs Ghana mchezo wa kimataifa, ulio kwenye ratiba za shirikisho la soka la kimataifa FIFA.
  • Ghana wanaingia katika mchezo huu, wakitoka kwenye kipigo kizito kutoka timu ya Taifa ya Austria, huku ujerumani wakiwa kwenye wimbi la ushindi.

Mechi nyingine bora ya kimataifa a kirafiki itapigwa leo Jumatatu katika Uwanja wa MHPArena. Ni Germany vs Ghana mchezo wa kimataifa, ulio kwenye ratiba za shirikisho la soka la kimataifa FIFA. Ghana wanaingia katika mchezo huu, wakitoka kwenye kipigo kizito kutoka timu ya Taifa ya Austria.

SOMA HII PIA: Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo | Usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Sportpesa-Aviator-Rain-Free-Bets----Mil-jpg

Germany vs Ghana h2h

Germany vs Ghana H-H
Germany vs Ghana H-H

Timu hizi zimekutana mara 3, katika historia ya mechi za mashindano mbalimbali ya kimataifa. Katika kipindi hiko Germany wamekuwa na rekodi bora zaidi, wakishinda mechi 2 na kutoa sare mchezo mmoja. Hivyo huu unakuwa mchezo wanne, je Germany wataendeleza ubabe, au Ghana watarekebisha makosa?

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Germany vs Ghana

Kikosi cha Germany
Kikosi cha Germany

Kipa: Baumann

Walinzi: Kimmich, Thiaw, Rudiger, Brown

Viungo: Gnabry, Gross, Stach

Washambuliaji: Karl, Woltemade, Schade

Ghana

Kikosi cha Ghana
Kikosi cha Ghana

Kipa: Zigi

Walinzi: Senaya, Pfeiffer, Djiku, Mensah

Viungo: Issahaku, Partey, Sulemana, Semenyo

Washambuliaji: Adu, Ayew

Habari za timu

Germany vs Ghana
Semenyo

Mechi hii ni mtihani mwingine mgumu kwa Ghana. Kikosi cha Otto Addo kimepoteza mechi tatu mfululizo mpaka sasa, na kitahitaji kiwango kilichoboreshwa kwa kiasi kikubwa ili kuepuka kipigo cha nne. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, Germany kwa sasa ni timu iliyo kwenye mfululizo wa ushindi wa mechi sita.

Ghana iliyopangwa Kundi L la Kombe la Dunia Pamoja na timu za England, Panama na Croatia ilikubali kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa Austria. Hii ilimaanisha wamepoteza mechi tatu mfululizo, tangu walipoifunga Comoros 1-0 mwezi Oktoba 2025. Hii ni baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya Japan na 1-0 dhidi ya Korea Kusini mwezi Novemba. Hii ni mara ya kwanza kwa Ghana kufungwa mabao 5 tangu mwaka 2017 walipochapwa na Saudi Arabia.

Kwa bahati nzuri kwa Ghana, bado wana muda ingawa ni miezi mitatu tu, imebaki kurekebisha makosa kabla ya mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Panama tarehe 18 Juni. Germany wao wanaonekana kuwa na safu imara ya ulinzi, waliweka rekodi bora ya ushindi katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia. Walishinda bila kuruhusu bao katika mechi nne kati ya tano dhidi ya Luxembourg (4-0, 2-0), Northern Ireland (1-0) na Slovakia (6-0).

Staa wao Florian Wirtz alikuwa kwenye kiwango bora na alihusika moja kwa moja katika mabao yote manne, dhidi ya Uswisi akifunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao.

Kocha, Julian Nagelsmann anaweza kufanya mabadiliko katika kikosi kilichoendeleza mfululizo wa ushindi. Lakini kikosi chochote kitakachoanza jijini Stuttgart, kinatarajiwa kuendeleza presha dhidi ya Ghana.

Taarifa za Nyota walio na majeraha

Ghana

Kikosi cha Ghana kinaonekana kuwa salama, ingawa Antoine Semenyo, Jordan Ayew na Thomas Partey walicheza dakika 86 katika kipigo dhidi ya Austria, wote wanaweza kuanza tena leo. Kocha Addo anatarajiwa kupanga kikosi imara zaidi, huenda Ghana wakafanya mabadiliko katika nafasi za mabeki wa pembeni. Gideon Mensah na Marvin Senaya wanaweza kuchukua nafasi za Derrick Kohn na Caleb Yirenkyi. Ayew alifunga bao lake la 34 kimataifa katika kipigo dhidi ya Austria, na atatarajia kuwa mwiba kwa Germany.

Germany

Florian Wirtz
Florian Wirtz

Kama ilivyo kwa Ghana, kwa upande wa wenyeji wako salama japo kuna uwezekano wa kufanya mabadiliko mengi baada ya mechi ya mabao saba dhidi ya Uswisi. Kocha, Nagelsmann anafikiria kumpa chipukizi wa Bayern Munich, Lennart Karl, nafasi ya kuanza kwa mara ya kwanza. Karl aliingia kuchukua nafasi ya, Leroy Sane dakika ya 63, na anaweza kuanza kutokana na mechi hii kuchezwa nyumbani dhidi ya timu isiyo katika kiwango kizuri.

Nick Woltemade anaweza kuongoza safu ya ushambuliaji badala ya Kai Havertz, huku Pascal Gross na Anton Stach wakichukua nafasi za Angelo Stiller na Leon Goretzka kiungo. Katika safu ya ulinzi, Nathaniel Brown anaweza kuanza badala ya David Raum, huku Antonio Rudiger na Malick Thiaw wakicheza katikati. Mabadiliko haya ni katika kupata uwiano wa Nyota wanaoanza, na wanaotokea benchi.

Hitimisho na Utabiri

Germany vs Ghana ni kipimo kingine kwa pande zote mbili kuelekea Fainali za Kombe la Dunia 2026. Kwenye makaratasi Germany anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, kutokana na fomu yake kulinganisha na mpinzani. Lakini mtego kwa kocha wa Germany ni uhalisia kuwa Ghana haijaonekana kwebye mashindano makubwa kwa muda mrefu, hii inawafanya kutotabirika. Dakika 90 zitatoa majibu sahihi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.