Arsenal vs Manchester CityArsenal vs Manchester City
  • Uwanja wa Wembley leo Jumapili utawaka moto katika mchezo mkali wa Fainali ya Carabao Cup.
  • Ni mchezo wa Arsenal vs Manchester City. Swali kubwa ni je, nani watapanda ngazi maarufu za Uwanja wa Wembley Stadium kuchukua medali za ushindi na kombe?
  • Makala hii inakuchambulia kwa ufupi dondoo muhimu za mchezo huu mkubwa.

Moto utawaka katika Uwanja wa Wembley leo Jumapili. Ni katika mchezo mkali wa Fainali ya Carabao Cup kati ya Arsenal vs Manchester City. Swali kubwa ni je, ni Arsenal au Manchester City, ambao watapanda ngazi maarufu za Uwanja wa Wembley Stadium kuchukua medali za ushindi? Makala hii inakuchambulia kwa ufupi dondoo muhimu za mchezo huo.

SOMA HII PIA: MANCHESTER CITY VS ARSENAL- Mbabe wa EPL Msimu Huu Kujulikana Etihad.

Je, ujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Sportpesa-Aviator-Rain-Free-Bets----Mil-jpg

Arsenal vs Manchester City H2H

Timu hizi zimekutana mara 214 katika historia ya mashindano mbalimbali, ambapo Arsenal wamekuwa na rekodi bora wakifanikiwa kuandikisha ushindi mara 101. Manchester City wao wameshinda mechi 65 tu, huku Mechi 48 zilizosalia zikiisha kwa matokeo ya sare. Jukwaa la Uwanja wa Wembley leo linakwenda kuandika historia mpya kati yao.

Fomu za timu kwenye Carabao Cup

Arsenal

W W W W W

Manchester City

W W W W W

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Arsenal vs Manchester City

Arsenal

Kikosi cha Arsenal (-)
Kikosi cha Arsenal

Kipa: Kepa

Walinzi: Timber, Saliba, Gabriel, Hincapie

Viungo: Zubimendi, Rice, Saka, Eze, Trossard

Mshambuliaji: Gyokeres

SOMA HII ZAIDI: Arsenal vs Manchester United EPL: Live score, h2h, lineups, utabiri, Habari za timu

Manchester City:

Kikosi cha Manchester City
Kikosi cha Manchester City

Kipa: Trafford

Walinzi: Nunes, Dias, Stones, Ait-Nouri

Viungo: Silva, Rodri, O’Reilly, Cherki

Washambuliaji: Haaland, Semenyo

Habari za timu

Arsenal vs Manchester City (-)
Arsenal vs Manchester City

Hii ndiyo fainali ya kwanza kabisa ya Kombe la EFL kuzikutanisha timu zilizopo nafasi ya kwanza na ya pili, kwenye Ligi Kuu England. Kwa Arsenal mchezo wa leo ni sehemu ya kuisaka ndoto yao ya kutwaa mataji manne msimu huu. Kikosi hiko cha Arteta, kitalazimika kuondoa mkosi wa kukosa Kombe la EFL uliowasumbua kwa zaidi ya miaka 30.

Aprili 18, 1993 ndiyo ilikuwa mara ya mwisho Arsenal kushinda taji hilo. Mpaka sasa wamepoteza fainali sita za mashindano haya, mojawapo ni ile ya karibuni dhidi ya Manchester City mwaka 2018. Hii inawafanya Arsenal kuwa timu iliyopoteza fainali nyingi zaidi, kuliko timu yoyote nyingine.

Safari ya kuelekea Wembley haikuwa rahisi kwa Arsenal, lakini walifanikiwa kuwaondosha Port Vale, Brighton, Crystal Palace na hatimaye Chelsea. Arsenal wako kwenye kiwango bora, hawajapoteza mechi 14 mfululizo. Hii ni baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen kwenye Ligi ya Mabingwa Katikati ya wiki.

Manchester City hawajawa kwenye kiwango bora msimu huu, ukiachana na kufurushwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa, lakini wameshinda mara 1 tu, katika mechi 5 zilizopita. Historia ya Carabao inawabeba City kwani, wameshinda fainali nane kati ya tisa za EFL Cup, zikiwemo saba mfululizo tangu mwaka 1974. Guardiola anaweza kuwa kocha wa kwanza kushinda kombe hili mara tano.

SOMA HII PIA: Tetesi za soka usajili Gyokeres kwenda Arsenal, Man United kufanya ‘ubaya ubwela?’

Taarifa za majeraha

Arsenal

Eze (-)
Eze (-)

Kama ilivyo kawaida yake, Mikel Arteta hakutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu hali ya kikosi. Lakini bado kuna hofu juu ya hali ya Jurrien Timber aliyeumia kifundo cha mguu na nahodha Martin Odegaard (goti). Mikel Merino yuko nje kutokana na jeraha la mguu, lakini Eze anaonekana kuwa sawa licha ya kupata maumivu kidogo dhidi ya Leverkusen. Arteta pia hakuthibitisha nani ataanza golini kati ya, Kepa Arrizabalaga na David Raya, lakini Kepa ana uwezekano mkubwa.

Manchester City

gvardiol
gvardiol

Kwa upande wa Manchester City, Guardiola amethibitisha kuwa kipa, James Trafford ataanza golini badala ya Gianluigi Donnarumma. Josko Gvardiol ndiye mchezaji pekee aliye majeruhi, huku Marc Guehi akishindwa kucheza kutokana na kanuni za mashindano. John Stones anaweza kuanza badala ya Abdukodir Khusanov, huku Erling Haaland akilenga kufunga bao lake la kwanza Wembley katika jaribio la saba.

Hitimisho na Utabiri

Katika miaka ya karibuni mchezo wa Arsenal vs Manchester City umeonekana kuzidi kuwa wa ushindani, hii ni baada ya uwekezaji ambao kila upande umeufanya. Mechi za Arsenal na Manchester City zimekuwa na tahadhari kubwa ya kiufundi kati ya Guardiola na Arteta, hivyo si rahisi kutarajia mabao mengi. Kwa kuwa timu zote zinahitaji ushindi, mechi inaweza kuwa ngumu na yenye nafasi chache za kufunga lakini Arsenal wanapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.