- Moto utawaka leo usiku kwenye Uwanja wa Camp Nou nchini Hispania.
- Ni katika mchezo wa Barcelona vs Newcastle United, mchezo huu ni wa marudiano wa mashindano ya UEFA champions League.
- Baada ya sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza, leo mshindi wa jumla atafuzu kucheza Robo Fainali.
- Barhtushwa na mashabiki 10,000 wa Newcastle United ambao wanaripotiwa kusafiri kuishangilia timu yao.
Moto utawaka leo usiku kwenye Uwanja wa Camp Nou nchini Hispania. Ni katika mchezo wa Barcelona vs Newcastle United, mchezo huu ni wa marudiano wa mashindano ya UEFA champions League, baada ya sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza. Mshindi wa matokeo ya jumla atakuwa amekata tiketi ya kucheza Robo Fainali ya mashindano hayo. Makala hii inachambua dondoo muhimu za mchezo huu.
SOMA HII PIA: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics
Je, bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Kama hujashinda, sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Barcelona vs Newcastle United h2h

Timu hizi zimekutana mara 6 katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA champions League). Barcelona wamekuwa na wakati mzuri zaidi, wakifanikiwa kushinda mechi 4. Newcastle wao wameshinda mchezo mmoja tu, huku mchezo mmoja uliosalia ukimalizika kwa matokeo ya sare. Mara ya mwisho walipokutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Machi 10, 2026, Barcelona walipata sare ya dakika za jiooni.
Vikosi vinavyotarajiwa Barcelona vs Newcastle United
Barcelona

Kipa: J. Garcia
Walinzi: Cancelo, Araujo, Cubarsi, Martin
Viungo: Bernal, Pedri; Yamal, Fermin, Raphinha
Mshambuliaji: Lewandowski
Newcastle United:

Kipa: Ramsdale
Walizni: Trippier, Thiaw, Burn, Hall
Viungo: Ramsey, Tonali, Joelinton, Elanga
Washambuliaji: Gordon, Barnes
Habari za timu

Mechi ya kwanza iliyochezwa wiki iliyopita katika uwanja wa St James’ Park England ilimalizika kwa sare ya 1-1. Newcastle walitangulia kwa bao la dakika ya 86 la winga wao, Harvey Barnes. Barcelona walirejea mchezoni kufuatia bao la penalti ya dakika ya 96 kutoka kwa kinda wao, Lamine Yamal.
Kocha mkuu wa Barcelona, Hansi Flick alikuwa wa kwanza kukiri timu yake haikucheza vizuri katika mechi ya kwanza. Pamoja na kusawazisha dakika za mwisho, amewataka wachezaji wake kucheza vizuri zaidi mechi ya marudiano kama wanataka kufuzu robo fainali. Barcelona wana imani kubwa ya kupata mabao katika mchezo wa leo kutokana na rekodi yao, wamefunga katika michezo yao 29. Hata hivyo, wamekuwa dhaifu kidogo katika safu ya ulinzi, wakishindwa kupata ‘Clean sheet’ katika michezo 12 mfululizo kwenye mashindano hayo.
Barcelona ambao ni mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wana rekodi nzuri katika hatua za mtoano. Wameshinda mara 23 kati ya mechi 29 za marudiano, katika nyakati ambazo mchezo wa kwanza uliisha kwa sare. Zaidi sana Barcelona pia, wana rekodi ya kuzifunga timu wapinzani kutokea England katika mechi tano zao zote za hatua ya 16 bora.
Baada ya sare yao dhidi ya Barcelona, Newcastle waliendeleza wimbi la matokeo yao mazuri hii ni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita. Staa wao, Anthony Gordon amekuwa na mwenendo bora, akifunga karibia kila mchezo. Ushindi dhidi ya Chelsea, ulikuwa wa nne katika michezo mitano ya ugenini kwenye mashindano yote.
Pamoja na rekodi hiyo ushindi huo pia umekuwa wa kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, tangu bao maarufu la Papiss Cisse mwaka 2012. Matokeo hayo yameongeza matumaini yao ya kufuzu mashindano ya Ulaya, wakipanda hadi nafasi ya tisa pointi 6 tu, kuifikia sita bora.
Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, Newcastle wamepoteza michezo miwili tu, kati ya 11 (ushindi 6, sare 3). Hata hivyo, hawajawahi kuvuka hatua ya 16 bora katika historia ya mashindano hayo. Ingawa wamepoteza mkondo wa pili mara moja tu, katika mechi 10 za hivi karibuni za UEFA.
SOMA HII ZAIDI: FC Barcelona: Muhtasari Kamili wa Habari za Hivi Punde, Ratiba, Matokeo, Kikosi, Takwimu, Maelezo ya Mechi na Habari za Usajili
Taarifa za Nyota wenye majeraha
Barcelona

Barcelona wataendelea kumkosa, Jules Kounde, Frenkie de Jong, Alejandro Balde (majeraha ya misuli) na Andreas Christensen (goti). Lamine Yamal alitokea benchi dhidi ya Sevilla baada ya kuugua, na anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza. Akiwa na miaka 18 na siku 249, anahitaji bao moja tu, kusawazisha rekodi ya Kylian Mbappe, ya kufunga mabao mengi ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kufikisha miaka 19 mabao 10.
Newcastle United
Kwa upande wa Newcastle, Bruno Guimaraes, Lewis Miley, Fabian Schar na Emil Krafth bado ni majeruhi, huku Sandro Tonali akifanyiwa vipimo baada ya kuugua. Anthony Gordon anatarajiwa kuanza, baada ya kukosa mechi ya kwanza kwa sababu ya ugonjwa. Ikumbukwe ni staa wa Madrid, Mbappe pekee aliyefunga mabao 13, ndio mwenye mabao mengi zaidi ya UCL msimu huu kuliko Gordon aliyefunga mabao 10.
Utabiri na hitimisho

Barcelona vs Newcastle United inatarajiwa kuwa mechi nyingine ya ushindani mkali, huku pia ikitarajiwa mabao kutoka kila upande. Newcastle baada ya kuivimbia Barcelona na kuzichapa Manchester United na Chelsea wameongeza kujiamini. Mashabiki zaidi ya 10,000 wa Newcastle wameripotiwa kusafiri kuishangilia timu yao, hivyo ni wazi italeta ushindani, lakini bado Barcelona wanapewa nafasi kubwa ya kushinda.

