Newcastle United vs BarcaNewcastle United vs Barca
  • Round ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), inatarajiwa kurindima wiki hii.
  • Siku ya Jumanne kutapigwa mechi 4 za kwanza, huku siku ya Jumatano Kundi la pili la mechi pia zikichezwa.
  • Mechi iliyo na uzito mkubwa Jumanne ni ile ya Newcastle United vs Barcelona.
  • Hii ni zaidi ya mechi, hii ni vita ya ubora kati ya ligi mbili zinazotajwa kuwa bora zaidi duniani yaani La Liga na EPL.

Hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), inatarajiwa kurindima wiki hii. Jumanne kutapigwa mechi 4 za kwanza, huku siku ya Jumatano Kundi la pili la mechi pia zikichezwa. Mechi inayoonekana kuwa na uzito mkubwa Jumanne ni ile ya Newcastle United vs Barcelona. Hii ni zaidi ya mechi, hii ni vita ya ubora kati ya ligi mbili zinazotajwa kuwa bora zaidi duniani yaani La Liga na EPL.

SOMA HII PIA: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics

Hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

image

Newcastle United vs Barcelona H2H

Newcastle United vs Barcelona
Newcastle United vs Barcelona

Timu hizi zimekutana katika michezo 5 ambayo yote ni ya mashindano ya UEFA Champions League. Barcelona wameonyesha utawala mkubwa wakishinda mechi nne. Newcastle wao wameshinda mchezo mmoja pekee. Katika makutano yao hakujawahi kupatikana matokeo ya sare.

Vikosi vinavyotarajia kuanza Newcastle United vs Barcelona

Newcastle United:

Kipa: Pope

Walinzi: Trippier, Thiaw, Botman, Hall

Viungo: Willock, Tonali, Joelinton

Washambuliaji: Barnes, Wissa, Gordon

Barcelona

Kipa: J Garcia

Walinzi: Cancelo, Cubarsi, E Garcia, Martin

Viungo: Casado, Pedri, Yamal, Fermin,

Washambuliaji: Raphinha, Lewandowski

Newcastle United vs Barcelona, habari za timu

Kikosi cha Newcastle
Kikosi cha Newcastle

Uwanja wa St James’ Park wa Newcastle United utawakaribisha miamba ya Hispania, Barcelona katika mechi ya mkondo wa kwanza ya hatua ya 16 bora. Hii ni katika michuano ya UEFA Champions League. Ikumbukwe Newcastle waliwaondoa Qarabag FK ya Azerbaijan, kwa matokeo ya jumla ya mabao 9-3 hatua ya mchujo. Kikosi cha, Hansi Flick kilimaliza nafasi ya 5 katika hatua ya ligi na kupata tiketi ya moja kwa moja ya kufuzu 16 bora.

Ni zaidi ya miaka minne tangu Newcastle inunuliwe na wawekezaji wenye asili ya Saudi Arabia, kikosi cha kocha Eddie Howe sasa kimeandika historia. Hii ni kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka barani Ulaya, kwa ngazi ya klabu. Newcastle wamefika hatua ya mtoano ya Champions League kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Licha ya mafanikio hayo, matokeo ya ligi ya ndani yaani EPL yameendelea kuwa ya kusuasua wiki za karibuni. Pia wikiendi hii walitolewa kwenye FA Cup kwa kupoteza 3-1 dhidi ya Manchester City. Mustakabali wa Howe Newscastle bado haueleweki.

SOMA HII ZAIDI: Barcelona vs Real Madrid Supercopa Clasico: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Taarifa za majeruhi

Newcastle

Mastaa wawili ghali zaidi ndani kikosi chao, Nick Woltemade na Sandro Tonali, walirejea baada ya kuugua na majeraha. Pia, Jacob Ramsey atarejea baada ya kumaliza adhabu ya kusimamishwa. Hata hivyo, Newcastle itawakosa: Emil Krafth (goti), Lewis Miley (paja), Fabian Schar (kifundo cha mguu), Bruno Guimaraes (paja). Mfungaji wa mabao manne dhidi ya Qarabag, Anthony Gordon, anatarajiwa kurejea katika kikosi cha kwanza.

Barcelona

Lewandowski
Lewandowski

Kwa upande wa Barcelona, Marc Bernal alitolewa mapema katika mechi dhidi ya Athletic Bilbao kutokana na matatizo ya tumbo, lakini anatarajiwa kuwa fiti. Hata hivyo, Barcelona itawakosa: Alejandro Balde, Gavi, Frenkie de Jong, Jules Kounde na Andreas Christensen.

Yamal kuweka rekodi?

Nyota wa Barcelona, Lamine Yamal mpaka sasa tayari amehusika katika mabao 34 msimu huu, amefunga mabao 19 na kuasisti mara 15 katika michezo 36. Hii inamfanya kuwa karibu kuweka rekodi mpya, ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufikisha mechi 30 mapema katika Champions League. Tayari ameonyesha kuwa Nyota muhimu wa baadae kwa Barca.

SOMA HII PIA: FC Barcelona: Muhtasari Kamili wa Habari za Hivi Punde, Ratiba, Matokeo, Kikosi, Takwimu, Maelezo ya Mechi na Habari za Usajili

Utabiri na hitimisho

Newcastle United vs Barcelona ni zaidi ya mchezo, hii inatarajiwa kuwa vita ya kuthibitisha ubora wa ligi. Kwa miaka mingi La Liga na EPL, zimetajwa kama ligi bora zaidi duniani. Hivyo ni wazi kila upande hautaingia kinyonge. Barcelona hawajapata clean sheet katika michezo yao 11 iliyopita ya Champions League, na rekodi hiyo inaweza kuendelea katika uwanja wenye presha kubwa wa St James’ Park.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.