- Sajenti Bacca kukaa nje kwa muda wa wiki tatu anasumbuliwa na nyonga.
- Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi.
- Wachezaji 6 kukosekana kwenye mipango ya Pedro Goncalves kutokana na kutokuwa fiti.
Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi kutokana na huduma zao kukosekana uwanjani. Furaha ya mchezaji ni kuwa fiti na maumivu yanamfanya awe nje kwa muda akipambania hali yake. Dickson Job, Clement Mzize, Bacca ni miongoni mwa wanaopambania kurejea kwenye ubora.
SOMA HII: Depu straika mpya Yanga, Gueye huyoo Simba: Tetesi usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi

Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi kwa wapenda soka. Burudani iliyokuwa inapatikana kutoka kwao haitapatikana mpaka watakaporejea katika ubora. Kuna orodha ya nyota 6 ambao ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.
Taarifa iliyotolewa na Yanga SC imeeleza kuwa wachezaji hao ni majeruhi. Watakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 2 mpaka 3.
Orodha ya wachezaji 6 wa Yanga SC wanaosumbuliwa na majeruhi
Bacca
Ibrahim Abdullah (Bacca) amepata jeraha la nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha Wiki tatu. Huyu ni beki. Alianza kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Azam FC. Huyu ni Sajenti ambaye alipadishwa cheo Machi 2025. Alianza soka Jang’ombe Boys 2027.
Depu

Laurindo Dilson (Depu) amepata majeraha ya nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Mfungaji wa goli la ushindi vs Tanzania Prisons. Ni mshambuliaji tegemeo kikosi cha Yanga SC.
SOMA HII: Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC NBC Premier League/ Highlights, stats

Boka
Chadrack Boka amepata jeraha la enka ya mguu wa kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Huyu ni beki.
Edmund
Edmund John amepata jeraha la bega na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Huyu ni mshambuliaji.
Job
Dickson Job beki wa Yanga SC alipata maumivu kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC. Atakuwa nje kwa muda akipatiwa matibabu.

Mzize
Mshambuliaji Clement Mzize alipata maumivu mwanzo wa msimu 2025/26. Alitarajiwa kurejea uwanjani Februari 2026. Aliporudi uwanja wa mazoezi alijitonesha tena hivyo yupo chini ya uangalizi.
SOMA HII: Yanga SC 3-0 JS Kabylie CAF Champions League/ Depu score, highlights, standings

Hitimisho
Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi il ani sehemu ya maisha. Madaktari wa mabingwa hao watetezi wanaendelea kuwapa huduma. Hivyo kuna uwezekano baada ya wiki mbili kupita taarifa mpya itatolewa.

