- Hali si shwari huko kati ya Taifa la Senegal na Shilikisho la soka Afrika CAF.
- Hii ni baada ya CAF kuwavua ubingwa wa AFCON 2025 Senegal, na kuwatangaza Morocco kuwa mabingwa.
- Maamuzi hayo yamezua gumzo, huku kila upande ukionyesha nguvu zake. Kufuatia mtifuano huo Rais wa Senegal naye ameishambulia CAF akiitaja Rushwa.
Hali ya mambo imezidi kuchafuka kati ya Taifa la Senegal na Shirikisho la Soka Afrika CAF, baada ya timu ya Taifa ya Senegal kuvuliwa ubingwa wa AFCON 2025. Suala hilo limechukua taswira mpya baada ya Serikali ya Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye kuishambulia CAF. Serikali ya Senegal inataka CAF ichunguzwe kwa madai ya Rushwa.
SOMA HII PIA: AFCON 2025: Mabingwa Senegal wapewa mapokezi ya Kihistoria Dakar
Hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Kuhusu Senegal kuvuliwa ubingwa wa AFCON 2025
Baada ya miezi miwili kupita baada ya fainali iliyojaa matukio mengi yenye utata kati ya Senegal vs Morocco kumalizika. Fainali iliyoshuhudia, Senegali wakitawazwa mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa dakika 120. Katika mchezo huo yalikuwepo baadhi ya matukio tata, yaliyofanya mchezo huo kusimama kwa zaidi ya dakika 15 huku Senegal wakitishia kususia mchezo kutokana na maamuzi tata ya refa.
Ni yapi maamuzi ya bodi ya Rufaa kuhusu bingwa wa AFCON 2025?

Kufuatia sekeseke hilo, bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imetoa taarifa kuwa ilibaini kuwa Senegal walikiuka kanuni za AFCON kwa kuondoka uwanjani wakati wa fainali iliyochezwa Januari 18. Hii ni baada ya Morocco kupewa penalti yenye utata. Wachezaji wengi wa Senegal walitoka uwanjani wakiongozwa na kocha wao Pape Thiaw. Hii ilisababisha mchezo huo kusimama kwa takriban dakika 17, kabla ya nahodha Sadio Mane kuwashawishi kurudi.
Kifungu cha 82 cha kanuni za AFCON kinaeleza kuwa timu itakayokataa kucheza, au kuondoka uwanjani bila ruhusa ya mwamuzi itachukuliwa kuwa imepoteza na itaondolewa mashindanoni. Kifungu cha 84 kinaongeza kuwa timu itakayokiuka kifungu hicho itapoteza kwa mabao 3-0. Na vifungu hivi ndivyo vilitumiwa na Uongozi wa Shirikisho la soka la Morocco kupitia rufaa yao.
Tamko la Serikali ya Rais wa Senegal, Faye

Serikali ya Senegal imetaka kufanyika kwa “uchunguzi huru wa kimataifa” kuhusu “tuhuma za rushwa” ndani ya CAF. Hii ni baada ya kuivua Senegal ubingwa wa AFCON 2025, na kuwapa Morocco.
Katika taarifa hiyo ya Serikali, Senegal ilisema uamuzi huo “usio wa kawaida na wenye uzito mkubwa” ulitokana na “tafsiri potofu ya wazi ya kanuni, iliyosababisha uamuzi usio halali na usio wa haki kwa kiwango kikubwa”. Iliongeza: “Senegal inakataa kabisa jaribio hili lisilo na msingi la kupokonywa haki.”
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 sanctions: Senegal, Morocco zapewa adhabu nzito na CAF Hakimi, Ndiaye wafungiwa
Swali ni kwa nini imechukua miezi miwili?
CAF haijatoa maelezo kwa nini kanuni hazikutumika mara moja wakati wa tukio. Baada ya rufaa ya Morocco, CAF ilichambua upya kanuni zake, kuhusu matukio ya utata yaliyotokea fainali. Hatimaye, bodi ya rufaa ilichukua hatua isiyo ya kawaida ya kubadilisha matokeo na kumpa Morocco ushindi wa 3-0.
Senegal watakiwa kurudisha medali na kombe

Kufuatia maamuzi hayo Shirikisho la soka la Senegal, wamepewa taarifa ya kutakiwa kurudisha kombe hilo Pamoja na medali. Hapa ndipo panapoonekana kuwa sehemu ngumu zaidi, hili bado halijulikani, hasa kutokana na mchakato wa rufaa unaotarajiwa kuanza kwa upande wa Senegal. Baadhi ya wachezaji wa Senegal wamebeza uamuzi huo mitandaoni, wakichapisha picha za sherehe zao na kombe.
SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Senegal vs Egypt: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Hitimisho: Ni kwa kiasi gani AFCON imechafuliwa?

Kupitia taarifa yao, Shirikisho la Senegal limeuita uamuzi huo kuwa “usio wa haki, wa ajabu na usiokubalika,” likisema umeharibu sifa ya soka la Afrika. Katibu mkuu wa shirikisho hilo aliuita “aibu kwa Afrika.” Kwasasa, Morocco wanahesabiwa rasmi kama washindi wa fainali kwa mabao 3-0, wakimaliza kusubiri kwa miaka 49 kushinda taji lao la pili la AFCON.
Bila kujali matokeo ya mwisho, AFCON 2025 tayari imechafuliwa na namna suala hili lilivyoshughulikiwa, na mabingwa wapya watabeba doa hilo mbele ya mashabiki.
