- Kibwana Shomari beki wa Yanga SC akimbizwa hospital kwa matibabu zaidi
- Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC NBC Premier League 2025/26
- Dupe afunga kwa penati, apewa tuzo ya mchezaji bora
Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC ni matokeo rasmi Tanzania Premier League. Walima zabibu walianza kufunga goli kupitia kwa William Edger dakika ya 42. Mshambuliaji wa Yanga SC, Depu alifunga goli la kuweka usawa dakika ya 45 na kuongeza goli la pili dakika ya 61. Prince Dube alizamisha jahazi la Dodoma Jiji kwa goli la tatu dakika ya 67, Uwanja wa KMC Complex.
SOMA HII: Yanga SC haijapoteza mechi 2025/26 NBC Premier League / Kariakoo Dabi inanukia, matokeo, rekodi
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.

Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC Depu mchezaji bora

Wakishinda Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC, Januari 27,2026 Depu amechaguliwa kuwa mchezaji bora. Kamati imepitisha jina la mchezaji huyo ambaye amekabidhiwa tuzo yake na wadhamini. Huu ni mchezo wa pili kwa Depu akifunga magoli mawili na kufikisha matatu katika ligi ya NBC Premier League.
Beki wa Yanga SC Kibwana Shomari alikimbizwa hospitali kwa huduma zaidi. Mchezaji huyo alianguka uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC. Taarifa kuhusu maendeleo yake itatolewa mara baada ya vipimo.
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC matokeo yao
| 27/01/2026 | Yanga SC | 3 | 1 | Dodoma Jiji FC |
| 22/06/2025 | Yanga SC | 5 | 0 | Dodoma Jiji FC |
| 25/12/2024 | Dodoma Jiji FC | 0 | 4 | Yanga SC |
| 22/05/2024 | Dodoma Jiji FC | 0 | 4 | Yanga SC |
| 05/02/2024 | Yanga SC | 1 | 0 | Dodoma Jiji FC |
| 13/05/2023 | Yanga SC | 4 | 2 | Dodoma Jiji FC |
| 22/11/2022 | Dodoma Jiji FC | 0 | 2 | Yanga SC |
Msimamo wa Yanga SC vs Dodoma Jiji FC
| MP | W | D | L | PTS | |
| 1. Yanga SC | 8 | 7 | 1 | 0 | 22 |
| 12. Dodoma Jiji FC | 11 | 2 | 4 | 5 | 10 |
Kikosi cha Yanga SC vs Dodoma Jiji FC
Langoni
Djigui Diarra.
Mabeki
Kibwana Shomari
Zimbwe Jr
Bacca
Assinki
Viungo
Conte Balla
Maxi Nzengeli
Mudathir Yahya
Pacome
Washambuliaji
Depu
Prince Dube.
Wachezaji wa akiba
Masalanga, Abubakar, Nondo, Boka, Sheikhan, Damaro, Duke Abuya, Kouma, Mzungu na Okello.
SOMA HII: Yanga SC vs Dodoma Jiji FC (5-0) |Simba SC yawaka moto kwa matokeo ya Ligi Kuu NBC Bara

Kikosi cha Dodoma Jiji FC vs Yanga SC

Ally Salim.
Nelson Munganga
Salmin Hoza
Andy Bikoko
Dickson Mhilu
Andayson Solomon
Mwana Kibuta
Kelfin Salim
Abdi Banda
William Edger
Idd Kipagwile.
Wachezaji wa akiba
Augustino Nsata, Karib Seif, Yassin Ngaza, George Makang’a, Gasper Damiani, Faraji Kayanda, Wazir Junior, Daniel Mrope, Layson Layson, Daud Milandu.
Hitimisho
Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC inawarejesha kwenye uongozi wa ligi mabingwa watetezi huku wakulima wakiporomoka nafasi mbili. Kutoka nafasi ya 10 sasa nafasi ya 12, JKT Tanzania nafasi ya pili.

