Manchester City vs Real Madrid (-)Manchester City vs Real Madrid (-)
  • Nani anabaki, nani anakwenda Robo Fainali ya UEFA Champions League? Majibu yatapatikana Jumanne na Jumatano hii.
  • Mechi 8 zitapigwa, huku Manchester City vs Real Madrid ukiwa mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.
  • Hii ni zaidi ya mechi, hii itakuwa vita ya kisasi na kuamini katika kinachoonekana kuwa hakiwezekani miujiza.
  •  Makala hii inakuletea dondoo muhimu kuhusu mechi ya Real Madrid vs Manchester City.

Manchester City vs Real Madrid ndiyo Habari ya mjini, huu ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu Jumanne hii. Mchezo huu wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions League utapigwa Uwanja wa Etihad, majira ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika mashariki. Baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 ugenini Je, wenyeji Manchester City wataweza kufanya miujiza ya kupindua meza? Nani anakwenda Robo Fainali, nani anabaki? Makala hii inakuletea baadhi ya mambo kuelekea mchezo huu.

SOMA HII PIA: KATI YA REAL MADRID NA MANCHESTER CITY NANI KWENDA FAINALI UEFA?

Je, bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?

Kama hujashinda, sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

image

Manchester City vs Real Madrid H2H

Timu hizi zimekutana katika michezo 16 kwenye mashindano yote, ambapo mechi kati yao huwa ni ngumu na matokeo ya kushangaza. Takwimu zinaonyesha mpaka sasa, Real Madrid wamefanikiwa kushinda mechi 6, huku Manchester City wao wakishinda mechi 5. Mechi 5 zilizosalia timu hizi zilimaliza kwa matokeo ya sare.

Vikosi vinavyotarajia kuanza Manchester City vs Real Madrid

Manchester City:

Manchester City vs Real Madrid
Kikosi cha City

Kipa: Donnarumma

Walinzi: Nunes, Dias, Guehi, Ait-Nouri

Viungo: Bernardo, Rodri, O’Reilly

Washambuliaji: Semenyo, Haaland, Cherki

Real Madrid:

Kipa: Courtois

Walinzi: Alexander-Arnold, Huijsen, Rudiger, Fran Garcia

Viungo: Valverde, Tchouameni, Camavinga

Washambuliaji: Guler, Diaz, Vinicius Jr

SOMA HII ZAIDI: ‘Manchester derby’ Manchester United vs Manchester City: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu

Kuhusu mechi ya Manchester City vs Real Madrid

Manchester City vs Real Madrid
Manchester City vs Real Madrid

Manchester City wana hali ngumu baada ya kupoteza 3-0 katika mchezo wa kwanza, uliofanyika Santiago Bernabeu. Federico Valverde aliwashangaza City kwa kufunga hat-trick ya kuvutia kipindi cha kwanza. Kikosi cha kocha Pep Guardiola kilishindwa kurejesha bao hata moja. Kipigo hicho kimeiacha City ikihitaji mabadiliko makubwa katika mechi ya marudiano Uwanja wa Etihad.

Fomu ya hivi karibuni ya City pia imeibua wasiwasi kabla ya mechi hii, hasa katika safu ya ushambuliaji. Sare ya 1-1 dhidi ya West Ham United kwenye EPL wikiendi iliyoisha haikusaidia kuwaongeza kujiamini. Erling Haaland, ambaye kawaida ni mfungaji tegemezi wa City, amekuwa na ukame wa kufunga mabao akifanya hivyo mara 4 tu, katika mechi 17 zilizopita.

Hii itakuwa mara ya 5 mfululizo kwa vigogo hawa wa Ulaya kukutana katika hatua za mtoano za Champions League.

Real Madrid wanaenda Manchester wakiwa na hali nzuri, hii ni baada ya mfululizo wa matokeo mazuri katika mashindano mbalimbali. Kikosi cha kocha Alvaro Arbeloa kilipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Elche CF katika La Liga mwishoni mwa wiki. Ushindi huu uliwafanya kuandikisha ushindi wa 3 mfululizo.

Taarifa za majeruhi

Manchester City

Manchester City wana nyota wawili ambao wana majeraha kuelekea mchezo huu, Josko Gvardiol bado yuko nje kutokana na kuvunjika mfupa wa mguu. Rico Lewis naye hayupo, kutokana na jeraha la kifundo cha mguu. Hata hivyo, City wamepata nafuu kwa kurejea kwa Mateo Kovacic, ambaye alikuwapo kwenye benchi katika mechi dhidi ya West Ham.

Haaland anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji tena, huku Matheus Nunes akitarajiwa kurejea katika kikosi cha kwanza kama beki wa kulia. Katika ulinzi wa kati, Ruben Dias na Marc Guehi wanaweza kuanza Pamoja, huku Rayan Ait-Nouri akicheza upande wa kushoto.

Real Madrid

Rodrygo baada ya upasuaji
Rodrygo baada ya upasuaji

Kwa upande wa Real Madrid, bado Kylian Mbappe hayupo fiti asilimia 100 (jeraha la goti). Jude Bellingham anayeuguza jeraha la misuli ya paja naye yupo mgii ndani mguu nje. Rodrygo bado yuko nje kutokana na jeraha la ACL, Dani Ceballos, Alvaro Carreras na Alaba wana matatizo ya misuli. Eder Militao bado hajawa katika hali bora ya kucheza. Ferland Mendy hatacheza, huku Raul Asencio pia akiwa na tatizo la utimamu wa mwili.

SOMA HII PIA: Mbappe ‘out’ Atletico Madrid vs Real Madrid: Live score, h2h, lineups, utabiri, habari za timu

Utabiri na hitimisho

Real Madrid vs Manchester City h-h
h2h

Manchester City vs Real Madrid utakuwa mchezo wa dakika 90 za kufa na kupona. Manchester City wana deni la kuonyesha kiwango bora zaidi mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, lakini kufuta pengo la mabao matatu dhidi ya Real Madrid ni kazi ngumu. Hii ni kutokana na uzoefu mkubwa walionao vigogo hao wa Hispania katika Champions League. Lakini bado Manchester City anapewa nafasi kubwa ya kupata ushindi, hata kama hawatafuzu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.