- Tanzania Prisons vs Yanga SC Juni 18 2025 Uwanja wa Sokoine, jasho kuvuja dakika 90 kwa wababe uwanjani.
- Yanga SC kamili kuwakabili Tanzania Prisons ugenini mzunguko wa pili msako wa pointi tatu muhimu.
- Tanzania Prisons hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi jambo litakaloongeza vita kwa wababe wote wawili.
Tanzania Prisons vs Yanga SC Juni 18 2025 Uwanja wa Sokoine ukiwa ni mchezo wa ligi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na wababe hao kuwa na hesabu kali katika kusaka pointi tatu muhimu. Yanga SC ambao ni vinara wa ligi wametia timu ndani ya jiji la Mbeya kamili gado kwa ajili ya kupambania pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90 za jasho katika mchezo wa ligi mzunguko wa pili saa 10:00 jioni.
Kiungo wa kazi karejea kazini Yanga SC

Khalid Aucho kiungo wa kazi Yanga SC ni miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo ambao wapo Mbeya kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa raundi ya 29 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Utakuwa ni mchezo wa mwisho Yanga SC kucheza ugenini msimu wa 2024/25.
Aucho ndani ya Yanga SC amekuwa mhimili eneo la kiungo mkabaji ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Katika mechi zilizopita hakuwa fiti asilimka 100 baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa ligi ilikuwa dakika ya 44 nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Mudathir Yahya ambaye yupo fiti pia kwa mchezo ujao.
Kwa sasa tayari Aucho amerejea katika ubora wake anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaopata nafasi kucheza mchezo ujao wa mzunguko wa pili. Kwenye msafara wa wachezaji waliopo Mbeya naye yupo. Mbali na Aucho kiungo mshambuliaji Dennis Nkane naye karejea kwenye ubora wake alifanya kazi kubwa kwenye Muungano Cup, Ibrahim Bacca beki wakupanda na kushuka, Dickson Job ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Tanzania Prisons vs Yanga SC kwenye vita
Yanga SC kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 27 inakutana na Prisons ambayo imecheza mechi 28. Tanzania Prisons ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 30 inapambana kujinasua kwenye nafasi ya kucheza play off.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 71 ikisa ni timu namba moja kufunga mabao mengi huku Prisons safu ya ushambuliaji imetupia mabao 23. Inakutana na Prisons ambayo haijawa kwenye ubora katika eneo la ufungaji
Vita ya Yanga SC na Simba SC kwenye ligi
Mchezo wa Juni 18 2025 kati ya Tanzania Prisons vs Yanga SC unachochea vita ya wababe wawili walio nafasi mbili za juu ambao wote wanawania ubingwa. Yanga SC ni bingwa mtetezi Simba SC nafasi ya pili kwenye msimamo.

Soma hii: Simba SC kuachana na makipa wote kuelekea 2025/26
Baada ya kucheza jumla ya mechi 27 ambazo ni dakika 2,430 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga jumla ya mabao 71 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 34 kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi.
Ikumbukwe kwamba ni timu namba moja ambayo imepata ushindi mkubwa kwenye mechi zake ikipata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC na iliwatungua mabao 6-1 Ken Gold kwenye mechi za ligi zote zilichezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Wakati ikiwa namba moja kwenye ligi na pointi zake 73 kibindoni, watani zao wa jadi Simba SC wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa namba mbili kwa timu yenye mabao mengi ikiwa imetupia mabao 63 baada ya kucheza mechi 27 na pointi zao ni 72.

Katika dakika 2,430 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38 ndani ya uwanja. Mkali wakutupia ndani ya kikosi cha Simba SC ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua mwenye mabao 15 ndani ya ligi.
Faida ya mabao kuibeba Yanga SC

Soma hii: Ibenge & Maxi watikisa taarifa mpya usajili Bongo
Kutokana na kufunga mabao mengi ambayo ni 71 tofauti ya mabao 8 na watani zao wa jadi Simba SC huenda ikawabeba Yanga SC ikitokea timu hizi mbili mwisho wa msimu zikagongana pointi baada ya mechi 30.
Watani hawa wa jadi mchezo wan amba 184 ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 25 2025 ikiwa timu hizi mbili zote zikashinda mechi mbili ambazo zipo mbele yao raundi ya 29 na 30 itakuwa ni zaidi ya fainali. Simba SC atashuka uwanja kwenye mchezo huo akigomea kuwa daraja la Yanga SC kutwaa ubingwa mbele yake na Yanga SC ataingia uwanjani kutetea taji lake alilotwaa msimu wa 2023/24.

