- Leo Jumatano Round ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League), itaendelea tena.
- Kama ilivyokuwa jana Jumanne, leo Jumatano zitapigwa tena mechi 4.
- Real Madrid vs Manchester City na PSG vs Chelsea ndio mechi zinazosubiriwa kwa uzito mkubwa.
- Hizi ni zaidi ya mechi, hizi zinatarajiwa kuwa vita ya visasi. Makala hii inakuletea dondoo muhimu kuhusu mechi ya Real Madrid vs Manchester City.
Huku Real Madrid vs Manchester City, kule PSG vs Chelsea katika hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Hatua hiyo itaendelea tena leo Jumatano usiku, kwa mechi 4 za uzito mkubwa kupigwa katika viwanja mbalimbali. Hizi ni zaidi ya mechi, bali ni vita ya visasi kutokana na historia ya kila timu. Makala hii inachambua kwa ufupi, dondoo muhimu kuhusu mchezo wa Real Madrid vs Manchester City.
SOMA HII PIA: Mbappe ‘out’ Atletico Madrid vs Real Madrid: Live score, h2h, lineups, utabiri, habari za timu
Hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Real Madrid vs Manchester City H2H

Timu hizi zimekutana katika michezo 15 kwenye mashindano yote, ambapo mechi kati yao huwa ni ngumu. Takwimu zinaonyesha mpaka sasa, Real Madrid wamefanikiwa kushinda mechi 5, huku Manchester City wao wakishinda mechi 5. Mechi 5 zilizosalia timu hizi zilimaliza kwa matokeo ya sare.
Vikosi vinavyotarajia kuanza Real Madrid vs Manchester City
Real Madrid:

Kipa: Courtois
Walinzi: Alexander-Arnold, Asencio, Rudiger, Mendy
Viungo: Valverde, Tchouameni, Camavinga
Washambuliaji: Guler; G. Garcia, Vinicius Jr
Manchester City:

Kipa: Donnarumma
Walinzi: Nunes, Dias, Guehi, Ait-Nouri
Viungo: Bernardo, Rodri, O’Reilly
Washambuliaji: Semenyo, Haaland, Marmoush
SOMA HII ZAIDI: MANCHESTER CITY vs REAL MADRID-Kumbukumbu ya msimu uliopita
Real Madrid vs Manchester City, habari za timu
Mchezo huu mkali na unaosubiriwa kwa hamu utapigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, leo Jumatano usiku. Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana katika katika hatua ya 16 bora. Real Madrid itashuka dimbani kwa ajili ya kampeni yao, ya kusaka ubingwa wa 16 wa mashindano hayo ya Ulaya.
Real Madrid ililazimika kupitia hatua ya playoff ya mtoano, baada ya kumaliza nafasi ya tisa katika hatua ya ligi. Hii ilikuwa ni nafasi moja tu, kulinganisha na Manchester City walipomaliza. Licha ya kuwa na nyakati ngumu msimu huu, Real Madrid wana rekodi bora wakifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora kwa msimu wa 23 mfululizo msimu wa 2003–04.
Kwenye La Liga, Madrid wamekuwa na matokeo mchanganyiko, ambapo wanakamatia nafasi ya pili. Pengo la pointi na vinara, Barcelona mpaka sasa ni pointi 4, huku kukisalia mechi 11 tu kufunga msimu wa ligi. Katika mechi 5 zilizopita wakicheza Uwanja wa Bernabeu, Real Madrid wameshinda mechi 4 na kupoteza mechi moja pekee katika mashindano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Manchester City wanauendea mchezo huu wakiwa na kumbukumbu nzuri, hii ni baada ya kushinda mechi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Hii ilikuwa ni katika mchezo uliopigwa Desemba. Faida nyingine kwa Manchester City ni kuwa, Real Madrid imepoteza mechi 4 za mwisho wakicheza dhidi ya timu za England.
Taarifa za majeruhi
Real Madrid

Real Madrid wanapitia kipindi kigumu cha kuwakosa baadhi ya mastaa wao muhimu, ambao wana majeraha na mazuio mengine. Kylian Mbappe (goti), Jude Bellingham (misuli ya nyuma ya paja). Wengine walio na majeraha ni Rodrygo aliyefanyiwa upasuaji, Eder Militao, Dani Ceballos na Alvaro Carreras ambao pia wako nje.
Bado haijathibitishwa kama, David Alaba atapatikana. Eduardo Camavinga anatarajia kurudi uwanjani, winga Vinicius Junior, ambaye hajafunga bao katika mechi 6 zilizopita vs Manchester City anatarajiwa kuanza.
Manchester City
Kocha, Pep Guardiola hana sababu kubwa ya kuwa na hofu kwani, majeruhi pekee waliopo kikosini kwake ni Josko Gvardiol, Mateo Kovacic na Rico Lewis. Erling Haaland anatarajiwa kurejea kikosini, baada ya kupumzishwa mechi iliyopita. Mshambuliaji huyo wa Norway tayari ana mabao 56 katika mechi 56 za Champions League, na amefunga mabao 10 katika mechi 10 za mwisho dhidi ya timu za Hispania.
SOMA HII PIA: ‘Manchester derby’ Manchester United vs Manchester City: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Hitimisho na Utabiri
Real Madrid vs Manchester City ni zaidi ya mechi. Hii ni vita ya kisasi kwa wababe hawa ambao wamekutana mara nyingi katika miaka ya karibuni. Pigo kubwa la idadi kubwa ya majeruhi, linatarajiwa kuwa tishio kwa Real Madrid lakini watakuwa na kila sababu ya kupambana. Mchezo huu Manchester City ana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, pia upo uwezekano mkubwa kila timu ikapata angalau bao moja.

