MANCHESTER CITY vs REAL MADRID-Kumbukumbu ya msimu uliopita
Klabu ya Manchester City leo usiku itashuka katika dimba la Etihad kupambana na timu ya Real Madrid, katika mchezo wa pili wa wa michuano ya Kombe la Klabu bingwa barani Ulaya.
Pambano hili la marudiano linawakuwakutanisha miamba wawili ambao, mmoja ni bingwa wa Kihistoria wa michuano hii na mwingine ni timu inayotafuta kuweka historia ya kushinda taji la klabu bingwa UEFA Ulaya, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.
Kama itakumbukwa, timu hizi mbili zilikutana wiki iliyopita nchini Hispania, katika Uwanja wa Santaigo Bernabeu na matokeo kuwa ya suluhu ya goli moja moja baina ya vigogo hawa wawili.
Mchezo huu unakuja wakati tayari Barcelona ameshinda taji la ligi kuu ya Uhispania hapo Jumapili na hivyo kuifanya Real Madrid kuwa na Kombe moja la Mfalme ambalo linajulikana zaidi kama Copa Del la Rey.
Kwa Upande wa Manchester City, wao bado wapo kwenye mbio za kuusaka ubingwa wa ligi kuu ya soka Uingereza, almaarufu kama English Premier League.
Mpaka sasa Manchester City ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu Uingereza, akiwa na jumla ya pointi 85, baada ya kucheza mechi 35, huku akiwa na mechi moja mkononi nyuma ya Arsenal ambaye alikuwa anaongoza ligi kwa kipindi kirefu.
Manchester City wanaingia dimbani katika mechi ya kesho, wakiwa hawajafungwa hata mechi moja katika mechi 22 za ligi kuu ya Uingereza ya EPL walizocheza.
Timu hiyo imekuwa na wastani mzuri wa ushindi, kwani mpaka sasa wameshinda mechi 15 mfululizo, katika uwanja wa Etihad.
Moja kati ya viungo matata kabisa wa timu hiyo Ilkay Gundogan, alifunga magoli mawili, mwishoni mwa wiki dhidi ya Everton, na kuwaweka vijana wanaonolewa na Pep Gurdiola, katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa EPL wa msimu huu.
Kwa upande wa Real Madrid wao hawatishwi na takwimu za Manchester City kwa kuwa wao ndio mabingwa wa kihistoria wa michuano hii wakiwa wamelichukuwa kombe la UEFA Champions League sio chini ya mara 14.
Tayari vijana hawa wa kocha Ancelloti, kwa msimu huu wana kombe la Mfalme kibindoni. Hivyo watakuwa kibaruani kujaribu kushinda taji la klabu bingwa UEFA, ili wafidie kombe la La Liga, ambalo Barcelona amelishinda juzi.
Sababu kuu inayopelekea mchezo huu kuwa na mvuto mkubwa sana, baina ya mafahari hawa wawili wa soka ni rekodi za hivi karibuni, hasa hasa zitokanazo na mechi za hatua kama hii.
Manchester City wanarudi katika uwanja wao wa nyumbani Etihad, wakiwa na kumbukumbu nzuri ya msimu uliopita, baada ya kuwafunga Real Madrid katika hatua kama hii ya nusu fainali kwa jumla ya magoli 4-3.
Kibao kiligeuka katika mechi ya marudiano ambapo Real Madrid aliifunga Manchester City kwa jumla ya magoli 3-1 na Los Blancos kufanikiwa kusonga mbele katika hatua ya fainali kwa aggregate ya magoli 6-5.
Swali linalorudi kwenye vichwa vya wapenzi wengi wa kandanda ni kwamba Je Manchester City atakubali kuondolewa tena kwa mara ya pili mfululizo katika hatua hii ya michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya?
Duru za soka barani Ulaya, zinaarifu kwamba Real Madrid hajaifunga Manchester City katika uwanja wa nyumbani katika mechi nne mfululizo.
Kitendo hicho cha kutoshinda katika uwanja wa Etihad, kinatafsiriwa kama nafasi ya ushindi wa moja kwa moja kwa Manchester City, baada ya matokeo ya awali ya 1-1.
Kuelekea mechi hii ya kesho timu zote mbili zimepata nafuu ambayo inaweza kuzipa ahueni timu zote mbili.
Klabu ya Mancheste City ilikuwa ina matumaini ya kumpata mchezaji majeruhi AKe, lakini jopo la madaktari linaonekana kusita kumshauri kocha PepGurdiola kumtumia katika mchezo huu.
Wakati huo huo Manchester City inategemewa kuwatumia wachezaji wake nyota Kevin De Bruyne, Jack Graelish, Bernado Silva na John Stones, ambao walipumzishwa dhidi ya Everton ili wawe tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Real Madrid.
Kwa upande wa Real Madrid, hofu kuu ipo kwa beki wao namba tatu Eduardo Camavinga, ambaye alipata majeraha ya mguu na kuanza kuchechemea mwishoni mwa mechi dhidi ya Getafe iliyopigwa mwishoni mwa wiki.
Na katika kuhakikisha hawapotezi nafasi ya kushinda, kocha wa Real Madrid aliwapumzisha baadhi ya nyota wake akiwemo Karim Benzema, David Alaba na Rodrygo.
Real Mdrid pia wamepata ahueni, baada ya wachezaji wake watatu wa nyuma Eder Militao, ferland Mendy na Carvajal ambao waliwakosa katika mechi iliyopita kutokana na kuwa na kadi za njano zaidi za moja kuwa huru kucheza mchezo huu.
Wachezaji wa kuchungwa zaidi kwa pande zote ni pamoja na washambiliaji Vinicius Junior wa Real Madrid na Erling Haaland wa Manchester City.
SportPesa ikiwa kama wadau wa michezo na burudani inakupa nafasi mteja wetu kubashiri mechi hii ambayo tayari ipo kwenye tovuti yetu sportpesa.co.tz au unaweza kupiga *150*87#