AS FAR Rabat vs Yanga SC CAF Champions LeagueMzize na tuzo
  • Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari 2026 ama Februari mwanzoni
  • Mudathir Yahya hatofanyiwa upasuaji tatizo lake, Yao mambo safi
  • Ijue ratiba kamili ya mabingwa watetezi wanaopeperusha bendera katika CAF Champions League

Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari 2026. Mbali na Mzize ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti kiungo Mudathir Yahya hatafanyiwa upasuaji wa tatizo lake. Hivyo ni habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo yenye makao makuu mitaa ya Jangwani, Dar.

SOMA HII: Angalia Clement Mzize alivyoshinda goli bora la mwaka CAF 2025

Ushindi mnene wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini uwe miongoni mwa washindi sasa hivi.

image

Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari, orodha ya wengine hii hapa

Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari
Mzize kwenye majukumu yake hivi karibuni. Source: Yanga SC.

Ukiweka kando Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari 2026 kuna orodha ya wachezaji wengine. Ikumbukwe kwamba Nyota huyo kwa sasa ameanza mazoezi mepesi ili kurejea katika ubora. Ana tuzo ya goli bora la CAF aliyotwaa 2025 ikiwa ni tuzo kubwa Afrika kwa Nyota huyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC, Ali Kamwe amesema Mzize anazidi kuimarika. Licha ya kuanza mazoezi ripoti za madaktari zinaeleza anaweza kurejea uwanjani Januari mwishoni ama Februari mwanzoni, 2026.

“Clement Mzize ameanza mazoezi mepesi lakini sio ya fitness ila ni mazoezi mepesi kutokana na majeraha yake yakumrejesha katika ubora wake naye anaweza kurejea uwanjani Januari mwishoni ama Februari.

Taarifa kuhusu Yao Yao

“Yao Yao Habari njema ni kwamba amemaliza kipindi cha kuwa chini ya medical na sasa atakuwa chini ya fitness. Kitendo cha kuruhusiwa kutoka kwenye medical mpaka fitness ni hatua kubwa ya kurejea katika pitch. Nafasi ya kurejea inatarajiwa Januari mwishoni ama Februari mwishoni anaweza kurejea uwanjani.

SOMA HII: Mudathir Yahya ameongeza mkataba miaka miwili Yanga SC | Simba SC yapishana naye | Orodha ya wanaofuata

image

Habari kuhusu Mudathir Yahya

Mudathir Yahya
Mudathir Yahya kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

“Mudathir Yahya huyu aliondolewa katika kikosi kilichosafiri kuelekea Misri kwa maandalizi ya Afcon nchini Morocco. tatizo lake sio la kufanyiwa upasuaji hapana kuna taratibu ambazo zinafanyika na huyu madaktari wamesema kuwa anaweza kuwa uwanjani Januari.

Israel Mwenda, Edmund John na Aziz

“Israel Mwenda hakuwepo mchezo dhidi ya Coastal Union yeye alipata Malaria, Edmund John alipata Homa ya kawaida na Aziz Andambilwe hawa walipata homa hivyo kuanzia sasa wanaendelea vizuri.

SOMA HII: Aziz yupo sana Jangwani mpaka 2027/ Orodha ya wachezaji wapya Yanga SC hii hapa

image

Taarifa kuhusu mapumziko ya Yanga SC

Ali Kamwe (-)
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

“Benchi la ufundi limetangaza mapumziko kuanzia Desemba 7 mpaka Desemba 15, wakirejea Desemba 15 watafanya mazoezi mpaka Desemba 20 kisha watapumzika tena mpaka Desemba 28.

 “Wachezaji watapata fursa ya kwenda kusherehekea sikukuu na familia zao, kabla ya kurejea tena mazoezini Desemba 29 kwa ajili ya maandalizi na wote tunafahamu kuwa mwezi Januari tuna mechi za kimataifa pamoja na za nyumbani kwa kutegemea ratiba ya bodi ya ligi itakavyopangwa.

“Kipekee ninapenda kuwapongeza mashabiki kwa kuwa nasi katika nyakati zote. Kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Coastal Union hakika mlionyesha ukomavu mkubwa. Kuwa na timu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo ilionyesha kuwa mnaamini matokeo yanapatikana muda wowte ule,” alisema Kamwe.


Hitimisho

Clement Mzize wa Yanga SC kurejea uwanjani Januari 2026 ni habari njema kwa familia ya michezo. Nyota huyo hakuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Coastal Union ugenini. Kuna nafasi kubwa wachezaji wa timu hiyo waliokuwa nje ya uwanja kurejea ifikapo Januari 2026.

Share this: