- Tanzania Premier League 2024/25 tuzo zake zinasubiriwa baada ya taji la ubingwa kuwa mikononi mwa Yanga SC.
- Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora NBC Premier League 2024/25. Rekodi zake ni moto wa kuotea mbali.
- Jean Ahoua wa Simba SC jina lake linatajwa kwa wenye nafasi kutwaa tuzo hiyo yenye heshima kubwa.
Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora NBC Premier League 2024/25. Ni jambo ambalo linasubiri majibu huku mshindani wake mkubwa akitajwa kuwa ni Jean Ahoua wa Simba SC. Wanaotajwa kuwania tuzo hiyo ya MVP wote wawili ni raia wa Ivory Coast, Pacome ana miaka 28 na Ahoua miaka 23. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Desemba 2025 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF).
SOMA HII: Pacome Zouzoua na Jean Ahoua nani mkali? MVP kazi ipo
Vuna mamilioni sasa hivi
Ni rahisi sana kuvuna mamilioni ikiwa utacheza Aviator. Unapaisha Kindege, kikiwa hewani wewe unashinda. Kila siku kuna mgao, wahi na ucheze sasa.

Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora 2024/25 NBC Premier League- rekodi zake zasemaje?

Itawezekana Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora 2024/25? Bado haijafahamika ila kitambo kidogo kila kitu kitakuwa wazi. Mwanzoni mwa Desemba tuzo hizo kubwa zitatolewa.
Katika kipegele cha mchezaji bora, (MVP) hapa kumekuwa na mvutano mkubwa. Kiungo wa Simba SC, Jean Ahoua rekodi zinaonyesha ni kinara wa ufungaji. Ahoua alifunga magoli 16 na alitengeneza pasi 9 za magoli akihusika katika magoli 69 2024/25.
Wababe hawa walipokutana mechi zote mbili za NBC Premier League Yanga SC walikuwa wababe. Mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na ule mzunguko wa pili Yanga SC 2-0 Simba SC. Ni pointi sita walivuna Yanga SC mbele ya Simba SC katika Kariakoo Dabi.
Kwenye magoli matatu ambayo Simba SC ilifungwa, Pacome alihusika katika mawili. Alifunga goli moja na kutoa pasi moja ya goli. Ahoua alikuwa shuhuda wakipoteza pointi sita uwanjani.
SOMA HII: Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? | Wachambuzi wajibizana Edo Kumwembe vs Jemedari
Rekodi za Pacome 2024/25
Pacome alicheza jumla ya mechi 26 alitumia dakika 1,626. Alikosekana kwenye mechi nne za ligi. Hivyo alikuwa ni chaguo la kwanza zama za kocha Miloud Hamdi.
Nyota huyo alihusika katika magoli 22. Alifunga magoli 12 na kutoa pasi 10 za magoli. Pasi yake ya 10 alitoa kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Mkapa alimpa Clement Mzize.
Juni 25 2025, Yanga SC 2-0 Simba SC alihusika kwenye magoli yote mawili. Alifunga goli moja kwa mkwaju wa penati na alitoa pasi kwa Mzize. Kwenye mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
SOMA HII: Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi/ Bingwa 2024/25/ Pacome balaa

Timu alizozifunga Pacome NBC Premier League

JKT Tanzania aliwafunga goli moja.
Namungo FC Novemba 30 2024.
Fountain Gate aliwafunga magoli mawili.
Singida Black Stars aliwafunga goli moja
Kagera Sugar aliwafunga goli moja kwa mkwaju wa penati.
KenGold aliwafunga goli moja
Coastal Union aliwafunga goli moja
Azam FC aliwafunga goli moja.
Tanzania Prisons aliwafunga magoli mawili.
Simba SC aliwafunga goli moja.
SOMA HII: Pacome Zouzoua yupo Yanga SC asaini miaka miwili | Magoli na rekodi zake akiwafunga Simba SC

Kazi imeanza msimu wa 2025/26

msimu wa 2025/26 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara amecheza jumla ya mechi tatu akitumia dakika 185. Kahusika kwenye magoli matatu kati ya 9. Kafunga goli moja na kutoa pasi mbili za magoli.
Novemba 9,2025, Yanga SC 4-1 KMC FC, alihusika katika magoli mawili.Alifunga moja na kutoa pasi moja ya goli. Kwenye mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
SOMA HII: Pacome Zouzoua mkataba umeisha Yanga SC | Chama, Aucho kwenye orodha | Hatma ipo hivi
Hitimisho
Pacome Zouzoua kutwaa tuzo ya mchezaji bora 2024/25? Vigezo vya hii tuzo mara nyingi hutazama rekodi na mchango wa mchezaji. Msimu wa 2023/24 Aziz Ki wa Yanga SC alitwaa tuzo hiyo. Je nani atatwaa 2024/25?

