Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SCMoriceee
  • Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SC mwenye kipaji tajika kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania.
  • Abraham ana miaka 22, mchezaji huyu alijiunga na Simba SC kutoka klabu ya Serbia inayojulikana kama RFK Novi.
  • Kutokana na ushujaa wake kwenye kucheza mpira, Morice aliteuliwa kuchezea kikosi kikuu cha Taifa Stars.

Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SC, kipaji chake kinazidi kuwa bora kila anapopata nafasi yakuwakilisha timu anayochezea. Morice mchezaji mwepesi na mwenye bashasha katika uwanja, ni ingizo jipya katika Ligi Kuu ya NBC 2025/26. Kabla ya kujiunga na mnyama Simba aliwahi kuchezea Klabu ya Spartak Subotica na RFK Novi za Serbia. Kwa sasa yupo ndani ya Tanzania Premier League inayodhaminiwa na NBC akionyesha uwezo wake.

SOMA HII: Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo, kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Morice Abraham Career

Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SC
Morice Abraham kiungo mshambuliaji wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Morice Abraham ni mchezaji wa zamani wa kituo cha kukuza vipaji cha Alliance kilichopo Mwanza. Septemba,2021 alisaini mkataba wa kuitumikia Klabu ya Spartak Subotika. 2023-24 alitolewa kwa mkopo Klabu ya RFK Novi kisha 2025 alisajiliwa na Simba SC.

Mechi za Morice Abraham

TimuMechiMagoli
Spartak Subotika200
RFK Novi70
Timu ya Taifa80
Simba SC Ligi30
Simba SC CAF30

Mechi za Morice Abraham Ligi Kuu Tanzania Bara

Simba SC 3-0 Fountain Gate, Uwanja wa Mkapa Septemba 25,2025 alitumia dakika 45.

Simba SC 3-0 Namungo FC, Uwanja wa Mkapa, Oktoba Mosi alitumia dakika 68.

JKT Tanzania 1-2 Simba SC, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo alitumia dakika 30.

Mechi za Morice Ligi ya Mabingwa Afrika

Morice Kipaji
Morice kwenye moj ya mchezo wa ushindani 2025/26. Source: Simba SC.

Simba SC 1-1 Gaborone United, Uwanja wa Mkapa alitumia dakika 90.

Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, alitumia dakika 24.

Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, Uwanja wa Mkapa alitumia dakika 58.

Morice Abraham Super Sub

Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs alianzia benchi. Nyota huyo aliingia dakika ya 66 akichukua nafasi ya Mutale. Morice alitoa pasi moja ya goli kwa Kibu Dennis katika mchezo huo ugenini.

Winga huyo alikuwa katika ubora mchezo dhidi ya JKT Tanzania. Kwenye mchezo huo ugenini alianzia benchi na alipoingia alibadilisha kasi ya mchezo. Alitoa pasi ya goli la ushindi lililofungwa na Jonathan Sowah.

Ni dakika 30 zilitosha kutimiza majukumu yake. Aliingia dakika ya 60 akichukua mikoba ya kiungo Joshua Mutale. Mnyama alikomba pointi tatu ugenini.

SOMA HII: Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs CAF Champions League Oktoba 26,2025

image

Semaji Ahmed Ally kuhusu Morice Abraham

KIMATAIFA
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa Morice ni mchezaji bora. Ameongeza kwa kubainisha kwamba akianza kikosi cha kwanza ama akianzia benchi bado anakuwa imara.

“Amekuwa kila akipata nafasi anaonyesha ubora wa hali ya juu. Tangu amekuja tayari tumecheza mechi tatu kwenye ligi ya NBC na tumecheza mechi 4 za Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwenye mechi ambazo anapata nafasi akianza ama akiingia kutoka kwenye mabadiliko amekuwa na matokeo chanya uwanjani. Tunaona namna anavyofanya kazi yake na sisi tunafurahia kuona burudani.

“Ana uwezo wa kupiga pasi ana uwezo wa kupasua eneo lenye ulinzi mkubwa akatimiza majukumu yake. Ni mchezaji ambaye amekamilika kwa asilimia 100.

“Bado kuna kazi kubwa ya kuendelea kufanya kuiboresha timu yetu. Kwenye kutengeneza nafasi na kuzitumia uwanjani. Hiyo ni kazi ya mwalimu wetu Dimitar Pantev. Mashabiki ni kuwa pamoja katika mechi zote na kuhakikisha tunahanikiza ushindi kwa kushangilia,”.

SOMA HII: Simba SC 1-1 Gaborone United CAF Champion League

image

Hitimisho

Morice Abraham kiungo mshambuliaji Simba SC, ni mchezaji ambaye anajitolea kila mechi anazocheza kwa asilimia 100. Jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji walioitwa katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morocco 2024 kwenye AFCON, rekodi zinaonyesha alicheza mechi tatu pekee za ushindani.

Share this: