- Yanga SC 2-0 Simba SC mchezo wa Kariakoo Dabi, matukio mawili yote ayafanikisha, ushindi na kutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2024/25.
- Pacome mbele ya Simba SC alikuwa kwenye siku bora kazini, mguu wake wa kulia ukihusika kwenye mabao yote mawili, alitoa pasi ya bao kwa Clement Mzize na kufunga bao mbele ya Simba SC.
- Shomari Kapombe, Mohamed Hussen walivuja jasho kutimiza majukumu, bahati haikuwa upande wao mbele ya Yanga SC.
Yanga SC 2-0 Simba SC kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Juni 25 2025 Yanga SC inatwaa ubingwa kwa kukusanya pointi tatu muhimu. Simba SC inagotea nafasi ya pili ikipishana na ubingwa kwa mara nyingine tena.

Ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Simba SC ilipoteza mbele ya Yanga SC. Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC. Ndani ya dakika 180 Simba SC imefungwa jumla ya mabao matatu na Yanga SC.
Hawa hapa wafungaji Kariakoo Dabi
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Pacome dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilisababishwa na kip awa Simba SC Moussa Camara kwenye harakati za kuokoa hatari. Mpigaji alikuwa ni Pacome ambaye hakufanya ajizi alijaza mpira nyavuni.
Pacome sasa anafikisha mabao 12 ndani ya ligi. Pasi za mabao ambazo anazo ni 9 hivyo kahusika kwenye mabao 21 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC. Kinara ni Jean Ahoua wa Simba SC mwenye mabao 16 na pasi 9 za mabao.

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Mshambuliaji Clement Mzize dakika ya 87 alipachika bao la pili. Mzize alianza benchi alichukua nafasi ya Prince Dube. Bao hilo linamfanya afikishe mabao 14 akiwa ni mzawa mwenye mabao mengi ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
Bao hilo alipachika akitumia pasi ya Pacome. Pacome alikuwa kwenye siku nzuri kazini akiwazidi wachezaji wa Simba SC kwenye kutengeneza hatari na spidi. Kazi imeisha msimu wa 2024/25.
Safu ya ushambuliaji Yanga SC balaa
Yanga SC safu yao ya ushambuliaji ni balaa. Kwenye mechi tatu imefunga jumla ya mabao 12. Ilikuwa Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC, Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji na Yanga 2-0 Simba SC. Ukuta wa Yanga SC chini ya Dickson Job ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi haujaruhusu bao.

Yanga SC ni namba moja kwa timu iliyofunga mabao mengi. Jumla ni mabao 83 imefunga. Timu namba mbili ni Simba SC ambayo imefunga mabao 69. Kinara wa utupiaji kwa Simba SC ni Ahoua.
Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Simba SC
Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Prince Dube, Pacome, Mudathir Yahya, Duke Abuya.
Simba SC kikosi kilichoanza dhidi ya Yanga SC
Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Chamou Karaboue, Che Malone, Kagoma, Ellie Mpanzu, Fabrince Ngoma, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Joshua Mutale
Waamuzi na rekodi zao
Mwamuzi wa kati kutoka Misri, Amin Omar, msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal na msaidizi namba mbili ni Samir Gamal Saad.

Soma hii: Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC balaa! kuna kadi nyukundu leo? – SportPesa Tanzania
Historia imeandikwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano, Juni 25 2025. Yanga SC ambao ni wenyeji wa Simba SC katika mchezo mkubwa wa Kariakoo Dabi. Ni matukio makubwa mawili yalikuwa yanasubiliwa mshindi na bingwa.
Jambo jingine la kihistoria ni kuwa katika mchezo huu ni matumizi ya waamuzi wa kigeni ambapo jopo zima la waamuzi watakaosimamia mchezo wanatokea nje ya Tanzania likiongozwa na waamuzi wanne wa Misri na mmoja wa Somalia huku Kamishina wa mechi akitokea Tanga.
Kadi za njano zimetembea
Namba za Mwamuzi wa derby, Amin Omar kwenye utoaji wa kadi ni hatari ila kwenye mchezo wa leo alikuwa amepoa. Rekodi zinaonyesha kuwa amechezesha jumla ya mechi (240), kwenye hizo mechi ametoa kadi za njano (826) ametoa jumla ya kadi nyekundu (47).
Kwenye mchezo wa leo mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano alikuwa ni Pacome. Pacome alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 21 ya mchezo. Hivyo anaingia kwenye rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano Kariakoo Dabi mzunguko wa pili.

Soma hii: Kizungumkuti Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi
Kwa upande wa Simba SC, nahodha Mohamed Hussen alionyeshwa kadi ya njano. Dakika ya 58 ya mchezo. Hiyo ilikuwa ni kadi ya kwanza kwa Simba SC kwenye mchezo wa leo.
Simba SC kwenye mechi 10 ambazo imekutana na Yanga SC imepata ushindi mchezo mmoja. Rekodi zinaonyesha kuwa tangu msimu wa 2020/21-2024/25 Yanga SC imeshinda mara nne, sare zikiwa ni nne. Kwenye misimu minne, Yanga SC imefunga mabao 13 na Simba SC mabao 6 pekee.

