- Pacome Zouzoua mchezaji bora Juni Ligi Kuu NBC mkataba umeisha Yanga SC baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho.
- Clatous Chama, Khalid Aucho kwenye orodha ya wachezaji ambao mikataba yao imefika ukingoni hivyo kwa sasa wapo huru.
- Ali Kamwe azungumzia suala hilo na kinachotakiwa ili abaki ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Pacome Zouzoua mchezaji bora Juni Ligi Kuu ya NBC mkataba wake umeisha ndani ya Yanga SC. Jitihada zinafanyika na mabosi wa timu hiyo ili asaini mkataba mpya. Ikiwa hawatafikia makubaliano kuna uwezekano kiungo huyo akaondoka bure.

Soma hii: SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yatajwa
Muda wa kuvuna mamilioni sasa hivi
Cheza Aviator ushinde mkwanja mrefu sasa hivi. Unapaisha kindege kikiwa kinapaa wewe unashinda. Ni rahisi sana kila siku kuna mgao wa mamilioni.

Ali Kamwe kuhusu Pacome
Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe aliweka wazi kuwa mchezaji huyo mkataba wake umeisha. Mbali na Pacome, kiungo Clatous Chama, Khalid Aucho nao pia wapo kwenye orodha. Kinachohitajika kwa sasa ni fedha ili kuwapa mikataba mingine.
“Kuna wachezaji ambao mikataba yao imeisha, una Pacome, Clatous Chama, Maxi Nzengeli. Ili wasaini mikataba mipya wachezaji hela inahitajika. Hivyo ni jukumu la kila Mwanayanga kuchangia kwenye kampeni ya Tofali la Ubingwa,” alisema Kamwe.
Yanga SC ikiwa imecheza jumla ya mechi 30 kacheza mechi 26. Nyota huyo alikosekana kwenye mechi nne ambazo ni dakika 360. Ni chaguo la kwanza kwa msimu wa 2024/25 chini ya Miloud Hamdi.
Kiungo huyo ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili. Ila ule wa kulia ni mguu wake wenye nguvu kwenye kufunga akiwa uwanjani. Mguu wake wa kushoto nao umekuwa na hatari kwenye mapigo ya vichwa hakutisha sana eneo hilo.
Yanga SC ikiwa imecheza jumla ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 Pacome kacheza mechi 26. Kwenye mechi 26 alikomba jumla ya dakika 1,626. Ni dakika 1,074 hakuvuja jasho uwanjani katika mechi za ligi.
Mabao aliyohusika kufunga ndani ya ligi

Soma hii; Kiungo Pacome amesema walistahili kutinga nusu fainali 2024
Kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika inayodhaminiwa na NBC, Pacome alihusika katika mabao 22. Alifunga mabao 12 na kutoa pasi 10 zilizoleta mabao. Pasi yake ya 10 alitoa kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Mkapa alimpa Clement Mzize.
Juni 25 2025, Pacome alikuwa kwenye ubora wake hasa kipindi cha pili. Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga SC 2-0 Simba SC alihusika kwenye mabao yote mawili. Pacome alifunga bao moja kwa mkwaju wa penati na alitoa pasi moja ya bao iliyotumiwa na Mzize.
Ujanja wake Pacome upo hapa
Ujanja wa Pacome kwenye kufunga mabao upo katika mguu wa kulia. Huu ni mguu wake ambao amewatesa mara nyingi zaidi makipa kwenye mechi za ushindani. Ni mabao 7 alifunga kwa mguu wa kulia. Mguu wa kushoto alifunga mabao manne na alifunga kwa kichwa bao moja.
Kwa mapigo ya penati alifunga mabao mawili. Timu ya kwanza ilikuwa ni Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Katika mchezo huo langoni alikuwepo Ramadhan Chalamanda. Kipa huyo alidaka penati moja iliyopigwa na Aziz Ki, Yanga SC walipopata penati ya pili mpigaji alikuwa Pacome.
Timu ya pili kuifunga kwa penati ilikuwa Simba SC. Kwenye mchezo huo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 Pacome alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Langoni alikaa kipa namba moja wa Simba SC, Mousa Camara.
Zijue timu ambazo alizifunga Pacome kwenye ligi
JKT Tanzania, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kwa mguu wake wa kushoto. Mchezo huu ulichezwa Oktoba 22 alitumia pasi ya Clatous Chama aliyempa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.
Namungo FC aliwafunga bao moja mzunguko wa kwanza. Ilikuwa Novemba 30 2024. Fountain Gate aliwafunga mabao mawili, Uwanja wa KMC Complex.
Singida Black Stars aliwafunga bao moja, Uwanja wa New Amaan Complex. Kagera Sugar aliwafunga bao moja kwa mkwaju wa penati dakika ya 77, Uwanja wa KMC Complex.
KenGold aliwafunga bao moja Uwanja wa KMC Complex. Bao pekee la kichwa alifunga kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Ni dakika ya 32 alipachika bao hilo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Aprili 7 2025.
Alifunga bao moja mbele ya Azam FC. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ilikuwa Azam FC 1-2 Yanga SC. Mabao mawili alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine.
Bao la 12 alifikisha kwa kufunga mbele ya Simba SC. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 25 2025. Yanga SC ilisepa na pointi zote tatu mbele ya Simba SC.
Mataji ndani ya Yanga 2024/25

Soma hii: Yanga SC 2-0 Singida Black Stars fainali ya kibabe
Yanga SC ilitwaa mataji matano na Pacome akiwa na uzi wat imu hiyo 2024/25. Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Muungano na CRDB Federation Cup. Ilipishana na taji la Ligi ya Mabingwa Afrika pekee katika mataji iliyokuwa ikipambania.
Hitimisho
Pacome ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwania tuzo ya MVP. Juni 2025 alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya NBC na kocha bora alikuwa ni Miloud Hamdi. Rekodi zinaonyesha kuwa Juni Pacome alicheza jumla ya mechi tatu akifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao akihusika kwenye mabao manne ndani ya dakika 242 alizotumia.


