- Ugenini Eswatini katika mchezo wa kwanza Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC yalikuwa matokeo ya mchezo.
- Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League Oktoba 26 2025 Uwanja wa Mkapa utaamua mshindi atakayetinga hatua ya makundi Afrika.
- Ahmed Ally afuta matokeo ya ugenini, kazi inaanza upya saa 10:00 jioni Jumapili.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League ni mchezo wa maamuzi utakaopigwa Oktoba 26 Jumapili, Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo uliochezwa Oktoba 19 2025 ugenini mnyama alipata ushindi wa goli 3-0. Wababe hawa wanasaka tiketi kutinga hatua ya makundi, mshindi wa jumla atafahamika.
SOMA HII: Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC | CAF Champions League | Highlights | Magoli yote |
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League nani atashinda?

Huu ni mchezo wa maamuzi kutafuta tiketi ya hatua ya makundi. Kuelekea Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League asilimia kubwa mnyama anapewa nafasi ya kupata matokeo mazuri. Ni asilimia 69 zinaanguka kwa Simba SC ushindi, 16 kwa wageni na asilimia 15 ni sare. Hii ni kwa mujibu ya tovuti mbalimbali za kubashiri.
Licha ya Simba SC kupewa kipaumbele kwenye ushindi haifanyi mchezo huo kuwa mwepesi. Nsingizini Hotspurs sio timu ya kubeza na hatua za mtoano zina mbinu zake. Dakika 90 zitaamua nani atapata matokeo.
Simba SC yatua Dar, Ahmed Ally Semaji atoa maoni yake

Mara baada ya kumalizana na Nsingizini Hostspurs ugenini Eswatini, usiku wa Oktoba 20 msafara wa Simba SC urirejea Dar. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC alisema kazi bado haijaisha. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa.
“Kupata matokeo ugenini ni jambo kubwa nagumu. Unajua haikuwa kazi rahisi ukizingatia kulikuwa na siku chache za maandalizi. Meneja Dimitar Pantev na benchi la ufundi wamefanya kazi kubwa na wachezaji wakatupa furaha.
“Matokeo yaliyotokea Eswatini yasitupe kiburi tukaamini tumeshakwenda hatua ya makundi.Bado na mchezo wetu wa Jumapili tunakwenda kuanza upya. Mashabiki waliopo Dar na nje ya Dar ni muda wakujitokeza kwa wingi Jumapili kuishangilia timu yao,”.
SOMA HII: Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League | H2H, statistics, lineups

Matokeo ya mechi 7 za Simba SC
Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.
Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Matokeo ya mechi 7 za Nsingizini Hotspurs

Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika.
Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora, ilishinda kwa penalti 4-2, Septemba 28,2025 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Black Bulls 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 19,2025, mchezo wa kirafiki.
Sidvwashini United 0-5 Nsingizini Hotspurs, Mei 25 2025, mchezo wa MTN Premier League.
Nsingizini Hotspurs 2-1 Rangers Shiselweni, Mei 17 2025, MTN Premier League.
Mbabane Highland FC 2-1 Nsingizini Hotspurs, MTN Premier League, Mei 11 2025.
SOMA HII: Nsingizini Hotspurs vs Simba SC CAF Champions League| Mtihani wa kwanza wa Meneja Mkuu Pantev

H2H
Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.
Taarifa kuhusu wachezaji wenye maumivu Simba SC
Bado wachezaji wanne hawajatengamaa kwa sasa kutoka Simba SC. Moussa Camara mlinda mlango namba moja. Hamza Jr huyu ni beki, Mohamed Bajaber huyu ni kiungo na Allasane Kante kiungo mkabaji.
Hitimisho
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League mashabiki wa mnyama wataruhusiwa kuingia baada ya adhabu kuisha. Ushindi waliopata ugenini ni faida kwao wakitanguliza mguu mmoja mbele. Wapinzani Nsingizni Hostspurs wnahitaji angalua ushindi wa goli 4-0. Je maajabu ya mpira yataonekana? Tusubiri, hapa kwenye site ya SportPesa tutaendelea kukuletea taarifa muhimu.
Jishindie mamilioni na Supa Jackpot 17 kwa kubofya hapa chini


