Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025 ni leo October 18, 2025,lineup, H2H

ByLunyamadizo Mlyuka

October 18, 2025
Yanga SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier LeagueIbrahim Bacca (-)Ibrahim Bacca (-)
  • Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League mchezo mkali wa mchujo utachezwa leo Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu.
  • Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC taarifa yake mpya kuelekea mchezo.
  • Silver Strikers itaanzia nyumbani na mchezo ujao itakuwa Dar, Uwanja wa Mkapa.

 Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni leo Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu-Malawi. Silver Strikers inatajwa kuwa na hatari ikiwa nyumbani kwa kuwa haikupoteza mechi hivi karibuni. Wananchi msimu mpya walipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Wiliete.

SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League | H2H, takwimu muhimu, utabiri
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League nani kukosekana?

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League
Mzize Clement mshambuliaji Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Kuna baadhi ya wachezaji muhimu ambao huenda watakosekana uwanjani. Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League mshambuliaji Clement Mzize ni asilimia chache kucheza. Mzize alikuwa na maumivu ya goti na tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga SC. Yao beki hayupo kwenye mipango kwa kuwa hayupo fiti.

Kwa upande wa Silvers Strikers kuna mshambuliaji ambaye amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu. Anaitwa Chinsis Maonga huyu huenda akakosekana kwenye mchezo wa leo. Wachezaji wengine wapo fiti asilimia kubwa.

Aziz Andamwile kiungo wa Yanga SC maoni yake

Aziz Andambwile
Aziz Andambwile kiungo wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

“Tunaamini mchezo utakuwa mgumu, wachezaji tumejiaanda vizuri kwa asilimia 90 tupo tayari ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu.

“Kuna namna ambavyo tumepewa maelekezo kwa ajili ya mchezo wetu. Timu ambayo tunacheza nayo ni nzuri na tunaamini mchezo utakuwa mzuri nasi wachezaji tupo tayari,”.

Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Silver Strikers

Kipa

Djigui Diarra

Mabeki

Israel Mwenda

Boka

Dickson Job

Ibrahim Bacca

Viungo

Balla Conte

Maxi Nzengeli

Kouma

Pacome

Aziz

Mshambuliaji

Dube

SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

image

Mechi 6 za Yanga SC zilizopita

Romain Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki).

Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).

Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika

Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).

Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).

 Mechi 6 za Silver Strikers zilizopita

Silver Strikers 1-0 Chitipa United, mchezo wa League Agosti 27 2025.

Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup

Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.

Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.

SOMA HII: Wiliete SC 0-3 Yanga SC CAF Champions League 2025 | Magoli yote, takwimu muhimu, super sub

image

H2H

Silver Strikers FC vs Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.

Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.

Orodha ya wachezaji wa Yanga SC waliopo Malawi

Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Khomein, Israel Mwenda, Kouma, Boka, Mohamed Hussein, Dickson Job, Assinki, Bakari Nondo, Ibrahim Bacca.

Aziz Andambwile, Balla Conte, Mudathir Yahya, Duke Abuya, Doumbia, Pacome, Edmund John, Chikola, Clement Mzize, Ecua, Maxi Nzengeli, Prince Dube na Boyeli.

SOMA HII: Ratiba ya Caf Champions League 2025/26: Elewa kiundani droo zilizofanyika kwenye hii michuano mikali

image

Hitimisho

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League ni mchezo mkali kwa wababe hawa wawili. Licha ya Yanga SC kupewa nafasi kubwa ya kushinda bado mchezo hautakuwa mwepesi. Silver Strikers ni wagumu wakiwa nyumbani.

Share this: