Real Madrid vs JuventusReal Madrid vs Juventus
  • Vita nzito ya vigogo wawili wa soka la Ulaya kupigwa leo Jumatano usiku.
  • Ni Real Madrid vs Juventus mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
  • Timu hizo zimekutana mara 21, Real Madrid wameshinda mechi 10. Juventus wameshinda 9, huku michezo 2 ikiisha kwa sare.

Real Madrid vs Juventus ni vita ya vigogo wawili wa soka la Ulaya, ambayo itapigwa leo Jumatano usiku katika Uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu. Huu ni mwendelezo wa michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Ulaya. Ushindi katika mchezo wa leo ni muhimu kwa pande zote mbili, katika safari ya kufuzu hatua ya mtoano.

SOMA HII PIA: Arsenal vs Atlético Madrid UEFA Champions League: live score, H2H, vikosi, utabiri

Ushindi mzito wa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Sasa ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

SEO Banner LV

H2H Real Madrid vs Juventus

Real Madrd vs Juve H-H
Real Madrd vs Juve H-2-H

Timu zimekutana mara 21 katika mashindano ya Ulaya ambapo, Real Madrid wameshinda mechi 10. Juventus wao wameshinda mechi 9, huku michezo miwili ikiisha kwa matokeo ya sare. Huu ni mchezo wa mabao mengi kwani, kati ya michezo hiyo 21 waliyokutana wamefungana jumla ya mabao 51. Ikumbukwe mara 2 kati ya walizokutana ilikuwa hatua ya fainali, ambapo Real Madrid waliibuka mabingwa.

SEO Banner LV

Mechi 5 zilizopita za Real Madrid

19 Oct Getafe 0-1 Real Madrid

04 Oct Real Madrid 3-1 Villarreal

30 Sep Kairat Almaty 0-5 Real Madrid

27 Sep Atletico Madrid 5-2 Real Madrid

23 Sep Levante 1-4 Real Madrid

Mechi 5 zilizopita za Juventus

19 Oct Como 2-0 Juventus

5 Oct Juventus 0-0 AC Milan

1 Oct Villarreal 2-2 Juventus

27 Sep Juventus 1-1 Atalanta

20 Sep Verona 1-1 Juventus

Kikosi cha Real Madrid kinachotarajiwa kuvaana na Juventus

Real Madrid vs Juventus
Kikosi cha Madrid

Kipa: Courtois

Walinzi: Valverde, Militao, Asencio, Carreras.

Viungo: Tchouameni, Camavinga, Mastantuono, Guler. Washambuliaji: Vinicius, Mbappe.

SOMA HII ZAIDI: Real Madrid 3-2 Celta Vigo: Mbappe airudisha Madrid kwenye mbio za ubingwa

Kikosi cha Juventus kinachotarajiwa vs Real Madrid

Como vs Juve
Como vs Juve

Kipa: Di Gregorio

Walinzi: Gatti, Rugani, Kelly

Viungo na Wing-backs: Kalulu, Thuram, Koopmeiners, Cambiaso, Conceicao,

Washambuliaji: Yildiz, David

Habari za timu zote kwa ujumla Real Madrid vs Juventus

Kocha wa Madrid Xabi Alonso, ameonesha nia ya kushinda taji la UEFA msimu huu. Kuonyesha dhamira yake tayari ameanza kwa kishindo, kwa kushinda mechi zake mbili za kwanza. Ushindi hu oni wa mabao 2-1 dhidi ya Marseille na baadaye kuichapa Kairat Almaty mabao 5-0. Kylian Mbappe alifunga hat-trick katika ushindi huo.

Madrid wamekuwa na rekodi bora wakicheza nyumbani, kwani wamepata ushindi katika mechi 12 kati ya 13. Mpaka sasa wamepoteza mara moja tu, dhidi ya AC Milan. Mabingwa hao wa kihistoria wa Ulaya, wanauendea mchezo huu wakitoka kushinda 1-0 dhidi ya Getafe wikiendi iliyopita.

Kutokana na matokeo hayo, Madrid wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye La Liga. Uongozi huo ni wa alama mbili mbele ya mahasimu wao wa jadi Barcelona. Timu hizo sasa zinangojea mchezo wa El Clasico ya kwanza ya msimu huu, itakayopigwa Jumapili ijayo.

Juventus bila Cristiano Ronaldo

Ronaldo akipambana
Ronaldo akipambana

Baada ya Ronaldo kuondoka, Juventus wanaonekana kupungua nguvu ndani ya Italia na barani Ulaya. Hawajafanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa miaka ya hivi karibuni. Ikumbukwe msimu uliopita walitolewa na PSV Eindhoven kwenye hatua ya mtoano.

Malengo yao msimu huu ni kufuzu moja kwa moja hadi 16 bora. Matumaini yao yanakabilia na upinzani mkubwa, kutokana na namna walivyoanza hatua za awali. Hii ni baada ya sare ya mabao 4-4 dhidi ya Borussia Dortmund. Mechi iliyofuata pia walitoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Villarreal. Sare hizo zinaifanya Juve kuwa na rekodi ya sare tano mfululizo, hii ni rekodi yao mbaya zaidi kwa karibu miaka 20.

SOMA HII PIA: Barcelona vs Real Madrid El Clasico ya 261 kinawaka leo: H2H, Vikosi, Uchambuzi, Utabiri

Taarifa ya majeruhi

Kikosi cha Juve
Kikosi cha Juve

Real Madrid wanatarajia kukosa huduma ya baadhi ya mabeki wao muhimu wakiwemo, Antonio Rudiger na Dani Carvajal. Mlinzi mwinginme wa Madrid, Dean Huijsen yuko mashakani. Trent Alexander-Arnold na Ferland Mendy wameanza mazoezi lakini huenda wakawekwa benchi kusubiri El Clasico.

Kwa upande wa Juventus, Tudor anatarajiwa kuwatumia Francisco Conceicao na Kenan Yildiz, kumsaidia mshambuliaji mmoja wa kati. Wageni hao pia watamkosa beki wa kati Bremer na beki wa kushoto Juan Cabal. Fabio Miretti amerejea mazoezini, na Edon Zhegrova anaweza kuwemo kwenye benchi.

SEO Banner LV

Utabiri

Kutokana na fomu ya timu zote mbili kama ambavyo imeainishwa, Real Madrid wanapewa nafasi kubwa ya ushindi.

Hitimisho

Real Madrid vs Juventus ni ‘Crash of the titans’. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na mabao, kwani rekodi zinaonyesha hakuna mechi yoyote kati ya 61 za mwisho za Real Madrid katika hatua ya makundi iliyomalizika bila bao. Hii ni rekodi ya nmfululizo wa miaka 10 na inatarajiwa kuwa mwelekeo huo utaendelea.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.