- Presha inazidi kuwa kubwa mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City.
- Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Swali ambalo jibu lake litajulikana hivi punde.
- Ali Kamwe afafanua hali ilivyo na kinachoendelea Jangwani.
Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa timu hiyo hawajaridhishwa na mwendo wa kocha huyo. Licha yakutopoteza kwenye mechi 6 zilizopita. Huyu ni mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi aliyeipa ubingwa Yanga SC 2024/25.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mkwanja

Muda ni sasa kupaisha Kindege cha SportPesa na kuvuna mkwanja. Ni rahisi kweli, usiache kuwa hewani mara baada ya kusoma makala haya. Cheza sasa Aviator upate mgao wako.
Je Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC?

Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Bado ni swali linaloulizwa Yanga SC kutokana na timu kucheza katika kiwango cha chini. Mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Pamba Jiji licha ya ushindi timu haikucheza katika kiwango bora. Dakika 45 za kipindi cha mwanzo wapinzani wao walitawala mwanzo mwisho.
Habari za ndani zinaeleza kuwa kutokana na kutokuwa katika kiwango bora huenda akafutwa kazi. Mchezo dhidi ya Mbeya City ugenini unatajwa kukoleza moto kwa kocha kuondoka. Licha ya kwamba taarifa rasmi bado hazijatolewa na uongozi wa Yanga SC kuhusu kufutwa kazi kwa kocha huyo.
Ligi ya NBC bado mbichi
Ligi ya NBC bado mbichi ikiwa ni mzunguko wa kwanza 2025/26. Ipo wazi kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wamecheza mechi mbili. Katika mechi hizo ambazo ni dakika 180 moja walikuwa nyumbani nyingine ugenini.
Awali ilikuwa inatajwa kuwa amepewa mechi tatu kufundisha lakini inatajwa mambo yamebadilika. Kuna hatihati akaondoka mapema na hizo tatu akazikosa. Hivyo muda wowote kuanzia sasa Yanga SC wanaweza kutoa taarifa mpya.
SOMA HII: Rayon Sports FC 1-3 Yanga SC: Highlights, magoli yote

Mechi tatu zijazo kwa Yanga SC Oktoba 2025
Mabingwa watetezi wana mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi. Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini Malawi Okotba 18 na ule wa marudiano utapigwa nyumbani kati ya tarehe 24-26. Mshindi wa jumla kwenye mechi hizi atatinga hatua ya makundi.
Mchezo mmoja ni wa ligi ya NBC itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar. Ni Oktoba 29 2025 Uwanja wa Mkapa mchezo huo unatarajiwa kuchezwa. Awali ulikuwa unatajwa kuwa mchezo wa mwisho kutazama mwendo wake.
SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Haya hapa matokeo ya mechi 6 za Yanga SC

Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Alichosema Folz mara baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City
Romain Folz mchezo wake wa sita ilikuwa dhid ya Mbeya City. Ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Mbeya City 0-0 Yanga SC. Ilikuwa ni mara ya kwanza anadondosha pointi mbili kwenye ligi.
Kocha huyo alibainisha kuwa walijitahidi kutafuta ushindi walikwama. Sababu kubwa ni aina ya uwanja ambao waliutumia. Mbali na hilo nafasi ambazo walitengeneza hazikubadilishwa kuwa magoli.
“Tulikuwa tunahitaji ushindi lakini uwanja haukuwa rafiki kwetu. Licha ya kujaribu kubadili wachezaji bado hali haikuwa nzuri. Hakuna ambaye amefurahia matokeo haya nina amini tutafanyia kazi makosa ili kuwa imara,”.
SOMA HII: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 | Vita yao na Simba SC balaa zito

Ali Kamwe kuhusu Folz

Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amebainisha kuwa bado Folz ni kocha wa timu hiyo. Amewaomba mashabiki wawe watulivu. Ikiwa kutakuwa na jambo taarifa itatolewa.
“Romain Folz ni Kocha Mkuu wa Yanga SC. Kwa sasa wachezaji wamepewa mapumziko. Wanatarajia kurejea kambini kwa maandalizi ya mechi zijazo za Ligi ya Mabingwa Afrika,”.
Hitimisho
Romain Folz amefutwa kazi Yanga SC? Ni taarifa inayosubiri majibu kutoka kwa uongozi wa Yanga SC. Timu hiyo kwa sasa ina kibarua kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutinga hatua ya pili.


