- Mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ametua Bongo kwa ajili ya kuanza kazi kukinoa kikosi hicho 2025/26.
- Kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia zaidi akiwa uwanjani mfumo ambao utakuwa kipaumbele kazini.
- Ni mkataba wa miaka miwili amesaini ndani ya mitaa ya msimbazi analitambua soka la Afrika.
Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia zaidi akiwa uwanjani. Kocha huyo ni mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids ambaye amepata kazi Raja Casablanca. Mara baada ya kuwasili Tanzania, Oktoba 4 alisema yupo tayari kuanza majukumu mapya.
SOMA HII: Unamfahamu, Dimitar Pantev kocha mpya Simba SC? Hizi hapa rekodi zake, mifumo na mafanikio
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia zaidi

Kabla ya kuajiriwa mitaa ya msimbazi Pantev huyo alikuwa akikinoa kikosi cha Gaborone United. Kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia kwa kasi jambo litakaloongeza ushindani kwenye ligi. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 kinara wa ufungaji alikuwa Jean Ahoua aliyefunga magoli 16 huenda dozi ikaongezeka.
Pantev amesema anatambua ushindani ni mkubwa. Aliongeza kwamba ana uzoefu na soka la Afrika hivyo hakutakuwa na ugumu katika kuyazoea mazingira. Mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Nimefurahi kuwa hapa nipo tayari kwa ajili ya kuanza kazi. Ambacho ninapenda ni kuona timu inashinda, ninapenda kushambulia kwa kasi zaidi kwenye mechi zetu. Ila sio hivyo na muda mwingine huwa ninafanya kazi ya kulinda kwani kama utafunga unapaswa usifungwe.
“Kikubwa ni ushirikiano kwenye kila hatua. Ninatambua hakuna ligi nyepesi na kuna kazi kwenye mashindano ya kimataifa. Ukweli ni kwamba nimefurahi kuwa hapa ninatarajia tutafanya vizuri,”.
SOMA HII: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

Timu ambazo amefundisha Dimitar Pantev
Ni timu tano ambazo alipata kuzifundisha zilizopo Afrika. Miongoni mwa hizo ni Victoria United ya Cameroon, FC Johansen ya Sierra Leone, Orapa United na Gaborone United hizi za Botswana.
Kwa miaka ambayo amefundisha Afrika amekuwa na mafanikio ya kutwaa mataji. Ni mataji mawili ya ligi akiwa Cameroon na Botswana. Kwenye nchi mbili tofauti alitwaa taji ikiwa ni msimu wake wa kwanza.
Orodha ya wachezaji wapya atakaofanya nao kazi Simba SC
Rushine

Rushine De Reuck ni mchezaji mpya ndani ya kikosi. Huyu ni beki alitambulishwa Julai 29 2025. Beki. Kwenye mechi mbili za ligi alipata nafasi ya kuanza na kufunga magoli mawili.
Kante
Nyota Alassane Kante ambaye ni kiungo alikuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia. Atakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26. Alitambulishwa Julai 30 2025.
Morice
Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025. Nyota huyo amesema kuwa kuna kazi kubwa yakufanya katika changamoto mpya. Atakuwa kwenye mikono ya kocha mpya.
Semfuko
Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Atakuwa kwenye changamoto mpya mbele ya kocha mpya.
Sowah

Jonathan Sowah alitambulishwa Simba SC, Agosti Mosi 2025. Msimu wa 2024/25 alikuwa Singida Black Stars alifunga mabao 13. Kocha mpya ataanza naye kazi.
Bajaber
Agosti 2 2025 Simba SC ilimtambulisha Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya. Nyota huyu anatarajiwa kurejea uwanjani Jumatatu kwa kuwa hakuwa fiti.
Mligo
Antony Mligo beki wa kushoto alitambulishwa ndani ya Simba SC Agosti 5 2025 alikuwa Namungo FC. Kandarasi ya miaka mitatu. Beki huyo ni mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Camara
Ni Naby Camara alitambulishwa rasmi kuwa nyekundu na nyeupe Agosti 14 2025. Nyota huyo aliwahi kucheza Klabu ya Al Waab ya Qatar na CS Sfaxien. Camara ana umri wa miaka 23 ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na beki wa kushoto.
SOMA HII: Simba Day Septemba 10 2025 | Ali Kiba kutumbuiza | Ubaya Ubwela pasua kichwa

Hitimisho
Kocha mpya Simba SC anapenda kushambulia akiwa uwanjani hivyo kutakuwa na mabadiliko makubwa katika mechi zijazo. Kocha huyo ni mkataba wa miaka miwili amesaini kama ilivyokuwa kwa Fadlu. Yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kazi.


