Real Madrid vs Bayern (-)Real Madrid vs Bayern (-)
  • Leo Jumanne April 4, 2026 katika Uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu, moto utawaka.
  • Ni Real Madrid vs Bayern Munich, mchezo ambao ni wa mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali, ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA Champions League quarter Final’.
  • Ni vita ya mastaa wakubwa wa Dunia kama, Kylian Mbappe, Vinicius Jr dhidi ya Harry Kane na Michael Olisse. Je, nani Kwenda Nusu Fainali? Makala hii inakupa dondoo muhimu za mchezo huo.

Kitaumana leo Jumanne katika Uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu, ni Real Madrid vs Bayern Munich. Mchezo huu ni wa mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali, ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA Champions League quarter Final’. Ni vita ya mastaa kama Kylian Mbappe, Vinicius Jr dhidi ya Harry Kane na Michael Olisse. Je, nani Kwenda Nusu Fainali? Makala hii inakupa dondoo muhimu za mchezo huo.

SOMA HII PIA: Best stadium in the world

Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator- 800Mil

Real Madrid vs Bayern Munich h2h

h-h
h-h

Timu hizo zimekutana mara 28 katika historia ya michezo ya mashindano mbalimbali, ambapo Real Madrid wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 13. Bayern Munich wao wameshinda mechi 11 pekee, huku mechi 4 zikiisha kwa matokeo ya sare. Timu hizi mbili zimekutana mara nyingi kuliko timu nyingine zozote katika historia ya mashindano haya, na hii itakuwa mara ya 29. Je, nani kuibuka mbabe leo? Dakika 90 zitatoa majibu.

Vikosi vinavyotarajia kuanza Real Madrid vs Bayern Munich

Real Madrid

Kipa: Lunin

Walinzi: Alexander-Arnold, Rudiger, Huijsen, Carreras

Viungo: Valverde, Tchouameni, Pitarch, Guler

Washambuliaji: Mbappe, Vinicius Jr.

Bayern Munich

Kikosi cha Bayern
Kikosi cha Bayern

Kipa: Neuer

Walinzi: Stanisic, Upamecano, Tah, Laimer

Viungo: Kimmich, Goretzka, Olise, Gnabry,

Washambuliaji: Diaz, Jackson

SOMA HII ZAIDI: MADRID VS BARCELONA MOTO UTAWAKA LEO WEKA MKEKA WAKO SPORTPESA

Habari za timu

Real Madrid

Mbappe (-)
Mbappe: Source 433

Real Madrid ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa kwenye historia ya mashindano haya ya Ulaya, ikiwa imeshinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara 15. Madrid wameanza kwa kusuasua msimu huu na kushuhudia wakimpoteza kocha, Xabi Alonso na timu kuichukua kocha, Alvaro Arbeloa. Los Blancos wanauendea mchezo huu, wakiwa wametoka kwenye kipigo cha kushtua cha mabao 2-1 dhidi ya Mallorca. Matokeo ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiri mbio zao za kusaka taji la La liga, huku wapinzani wao wakuu Barcelona wakiongeza pengo hadi pointi 7.

Katika hatua za awali, Real Madrid waliifunga Benfica 3-1 kwenye mchujo, kisha wakaishinda Manchester City 5-1 katika hatua ya mtoano ya 16 bora. Kama ilivyoelezwa kwenye h2h, Real Madrid wana rekodi bora zaidi wanapokutana na Bayern, wakiwa wameshinda mara 13 na kupoteza 11 katika mikutano 28. Hawajapoteza mechi yoyote kati ya mechi 9 zilizopita (ushindi 7 na sare 2). Historia inaeleza kuwa katika mara 4 zilizopita, Real Madrid walipoiondoa Bayern, waliishia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa.

Bayern Munich

Bayern Munich wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa katika kiwango kizuri msimu huu, wamepoteza mechi 2 tu kati ya 43 katika mashindano yote. Kipigo chao cha mwisho kilikuwa Januari 24, dhidi ya Augsburg wakichapwa mabao 2-1. Katika mfumi wa ligi msimu huu, walimaliza nafasi ya 2 nyuma ya Arsenal na kufuzu moja kwa moja hadi 16 bora. Katika mtoano waliichapa Atalanta kwa jumla ya mabao 10-2. Katika Bundesliga, wanaongoza kwa tofauti ya pointi 9, na wwishoni mwa wiki walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Freiburg baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0.

Taarifa za majeruhi

Real Madrid

Real Madrid watamkosa Thibaut Courtois na Rodrygo kutokana na majeraha, huku Ferland Mendy na Dani Ceballos wakiwa na shaka kama watapatikana. Kylian Mbappe ndiye mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu huu akiwa na mabao 13. Staa huyo anatarajiwa kuanza pamoja na Vinicius Junior leo.

Bayern Munich

Kwa upande wa Bayern, Sven Ulreich, Cassiano Kiala, David Santos na Wisdom Mike hawatakuwepo kutokana na majeraha. Harry Kane pia yuko kwenye hatihati ya kuanza, iwapo staa huyo hatakuwepo basi, Nicolas Jackson anaweza kuanza kama mshambuliaji kiongozi akisaidiwa na Luis Diaz, Serge Gnabry na Michael Olise.

SOMA HII PIA: Bayern Munich’s Epic Showdown: 3 Wins Each vs Leverkusen

Utabiri na Hitimisho

Real Madrid vs Bayern historia
Real Madrid vs Bayern historia

Real Madrid vs Bayern Munich sio tu mchezo, bali ni ‘the crash of Titans’ yaani ni vita ya klabu kubwa 2. Kwa kawaida, Real Madrid huwa na kiwango kizuri katika Ligi ya Mabingwa, hasa wanapocheza nyumbani. Bayern Munich wamekuwa bora msimu huu, lakini rekodi ya Real Madrid dhidi yao inawapa Los Blancos wanaocheza nyumbani nafasi nzuri ya kushinda.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.