Dickson Job (-)Dickson Job (-)
  • Hatua ya awali kwenye anga la kimataifa inaanza kutimua vumbi kwa timu kushuka uwanjani kusaka ushindi.
  • Yanga SC watachuana na vijana wa Angola Wiliete SC kwenye CAF Champions League 2025.
  • Romain Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC kwenye kibarua kingine baada ya kushinda mbele ya Simba SC.

Yanga SC watachuana na vijana wa Angola Wiliete SC kwenye msururu wa kwanza wa CAF Champions League 2025. Mechi hii itafanyika Septemba,19, 2025, Uwanja wa 11 de Novembro. Huu ni mchezo wa hatua ya awali utapigwa saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Timu zote mbili zimebainisha kuwa utakuwa mchezo mzuri.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Ni muda wa kupaisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi. Rahisi sana na inawezekana. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

Wiliete SC vs Yanga SC Romain abainisha mpango kazi

Wiliete SC vs Yanga SC
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz. Source: Yanga SC.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz alikiongoza kikosi kufanya mazoezi ya mwisho Septemba 18 2025. Leo anatarajiwa kutupa karata yake ya kwanza kimataifa. Kocha huyo amebainisha wapo tayari kwa ushindani.

“Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika tutakuwa ugenini. Haya ni mashindano makubwa na tutakuwa kwenye nchi nyingine. Tunatambua kuhusu ushindani na ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri.

“Tuna ratiba ngumu ambayo inatukabili ila ni muhimu kuwa makini na kupata matokoe. Kitu ambacho ninaweza kukwambia ni kwamba tumefanya maandalizi kwa ajili ya mchezo. Kikosi kipo tayari na tunahitaji kucheza mchezo wetu kwa umakini,”.

Soma hii: Wiliete SC vs Young Africans SC CAFCL: ‘LIVE’, vikosi, H2H, Utabiri, Yanga Yatua Angola kibabe

Yanga SC na historia yake katika anga la kimataifa

Bacca Angola
Bacca beki wa Yanga SC kwenye maandalizi nchini Angola. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

Yanga SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25 hawajawa na rekodi nzuri katika anga la kimataifa. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 iliishia katika hatua za makundi. Malengo makubwa kwa msimu wa 2025/26 ni kuvunja rekodi hiyo ili kufikia malengo makubwa kimataifa.

Hali ya kikosi cha Yanga SC

Moses Etutu, daktari wa Yanga SC amebainisha kuwa wachezaji wapo fiti asilimia kubwa.Kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ameweka wazi ni kwa asilimia chache yanatofautiana na Tanzania.

“Tunashukuru Mungu baada ya Dabi hatujawa na wachezaji ambao ni majeruhi. Kidogo kwenye mechi kubwa huwezi kukosa migongano lakini wachezaji wote wapo tayari. Ni Yao, (Attohoula) ambaye huyu taarifa yake tulishatoa huyu hayupo fiti kwa asilimia 100 kwa ajili ya mchezo wetu.

“Wachezaji wetu wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo. Kidogo hali ya joto ipo chini tofauti na Dar. Ila hilo siwezi kusema kwamba itakuwa ni tofauti. Joto ambalo lipo ni sawa kwa kuwa hakuna tofauti yoyote,” alisema Etutu.

Nahodha wa Yanga SC Bakari Mwamnyeto aomba dua

Bakari Mwamnyeto nahodha wa Yanga SC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mapambano. Baada ya kufika Angola alibainisha kuwa maandalizi yamekwenda vizuri. Aliongeza kuwa wanahitaji maombi kutoka kwa mashabiki wote.

“Wachezaji wote wapo vizuri na wana ari asilimia 100. Kikubwa ambacho kinahitajika ni ushindi kwenye mchezo wa kwanza. Tumepata nafasi kuona namna wapinzani wetu walivyo.

“Benchi la ufundi limetuonyesha ubora wao na udhaifu wao. Tunaamini kupitia madhaifu yao tutayatumia ili kupata matokeo mazuri. Mashabiki ambao hawapo Angola tunaamini kwamba wapo nasi. Hivyo tunawaomba watuombee dua ili tupate matokeo mazuri,” alisema Mwamnyeto.

Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC kuhusu wapinzani

SportPesa yaipa Yanga SC Bilioni 21.7
Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Droo ya Caf Champions League 2025/26

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema: “Tumekuwa na program tofauti. Mchezo utakuwa mzuri na wapinzani wetu hawa wanaweza kuwa wapya kwa Watanzania. Lakini ukizungumza na watu wa Angola wanakuambia kuhusu ubora wao. Ni moja ya timu sumbufu.

“Huu ni mchezo wa mtoano hivyo ni muhimu kufanya vizuri katika mchezo wa kwanza. Tunauzoefu kuliko wao hilo lipo wazi hivyo tutatumia hiyo kama silaha kwa ajili ya mchezo wetu muhimu ili tusonge mbele,” alisema Kamwe.

Skudu wa Wiliete SC

Kiungo wa Wiliete SC Skudu Makudubela amesema: “Timu yetu imejiandaa vizuri. Tunatazamia mchezo kuwa mgumu na wenye ushindani. Ninafikiri timu zote zimejiandaa vizuri hivyo tunatarajia kuwa na burudani katika vipindi vyote viwili. Kipindi cha kwanza na kipindi cha pili. Ninaifahamu Yanga SC na unajua ninamfahamu mwalimu pia,”.

Kuhusu Wiliete Klabu ya Angola

Wiliete SC ni klabu ya Angola inayopatikana huko Benguela. Ingawa ni klabu mchanga, imethibitisha kasi ya ukuaji wake kwa kushiriki kwenye ligi kuu ya Angola (Girabola), na kushika nafasi za juu kabisa.

Septemba 14 2018 ilianzishwa baada ya kupita madaraja ya chini walipanda daraja na kwenda ligi kuu. 2024‑2025, Wiliete SC walishika nafasi ya pili katika ligi yao ya Angola. Hii iliwapa tiketi ya kushiriki CAF Champions League kwa mara ya kwanza katika historia yao. Wilite wanatumia uwanja wa nyumbani wa Estádio Nacional de Ombaka ulioko Benguela, unaochukua mashabiki 35,000.

Hitimisho

Wiliete SC vs Yanga SC wababe hawa watakuwa kazini katika anga la kimataifa. Mchezo wa pili wa marudiano utaamua timu ipi itakwenda hatua inayofuata. Uzoefu unawapa Wanajangwani nafasi kupata matokeo kwenye mchezo wa leo.

image
Share this: