- Historia imeandikwa Septemba 12 2025 kwa tukio kubwa kufanyika ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.
- Yanga SC 1-0 Bandari FC goli la mapema dakika ya pili ya mchezo likifungwa na Ecua ambaye ni ingizo jipya limedumu kwa muda wa dakika 88.
- Kituo kinachofuata ni Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC, Uwanja wa MkapaSeptemba 16 2025 Ngao ya Jamii.
Yanga SC 1-0 Bandari FC mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Mchezo huu ulikuwa ni hitimisho la kilele cha Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025. Kampuni ya SportPesa amba oni wadhamini wakuu wa Yanga SC walikuwa hatua kwa hatua katika maandalizi.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda mchache ila ukiwa hewani na Kindege cha SportPesa kwako itakuwa kicheko. Kuna mamilioni ambayo yanakusubiri sasa hivi. Unachotakiwa kufanya ni kucheza Aviator upate mgao wako.

Yanga SC 1-0 Bandari FC, kilele cha Wiki ya Mwananchi
Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Yanga SC ilifunga bao mapema kipindi cha kwanza. Mfungaji wa bao hilo ni Celstin Ecua. Pasi ilitolewa na mshambuliaji Prince Dube.

Hili ni goli la kwanza kwa Ecua kufunga akiwa na uzi wa Yanga SC katika mchezo wenye mashabiki wengi. Mbinu za Romain Folz ilikuwa ni kushambulia wakipiga pasi mojamoja mpaka kufikia lango. Pasi ya Farid Mussa haikupotezwa na Dube ambaye alipiga krosi ya juu ikakutana na Ecua aliyefunga bao pekee kwa Yanga SC.
Mchambuzi Hans Rafael amzungumzia Ecua
Mchambuzi wa michezo Tanzania, Hans Rafael amemzungumzia winga Ecua kuhusu ubora wake. Hans kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna hii: “Explosive winga mwenye mikato ya wembe, mguu wake wa kushoto una kata zaidi ya kisu cha buchani. Anajua muda wa kukimbia sana na muda wa kupooza ili ku-link up na wenzake.
“Kwenye 1v1 ni kiyama kukabiriana nae. Ukisikia Ball dencer basi likumbuke jina la Selestine Ecua. Huyu ni mtu wa mpira kabisa. Hili ni Balaa jingine Tanzania.”
Kikosi cha Yanga SC vs Bandari FC
Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Bandari FC mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mkapa. Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga anavaa jezi 39. Israel Mwenda anavaa jezi namba 33. Farid Mussa anavaa jezi namba 17. Bakari Mwamnyeto 3. Assink ingizo jipya anavaa jezi 36. Aziz Andambwile anavaa jezi namba 2, Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji anavaa jezi namba 7.
Kouma huyu anavaa jezi namba 8, Prince Dube anavaa jezi namba 29, Shekhan anavaa jezi namba 20, Ecua anavaa 11 hawa wameanza kikosi cha kwanza.
Wachezaji wa akiba ni Aboutwalib Mshery, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Ninju. Shomari Kibwana,Mohamed Hussein, Boka, Casemiro, Conte. Duke Abuya, Mudathir Yahya, Doumbia, Sure Boy, Dennis Nkane, Offen Chikola, Edmund John na Boyel.
Mbinu za Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz

Hans amezungumzia pia kuhusu mbinu za Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz. Hans ameandika namna hii: “Kwenye phase ya kwanza ya ujenzi (Build-Up) anamtaka namba 6 wake kushuka chini katikati ya mabeki wawili wa kati ili kutengeneza back 3 ya uongo. Kisha Farid Mussa anaingia ndani kama 6 wa uongo ili kuongeza passing option.
“Kwenye “fast break” kocha anamtaka namba 6 (Andambwile & Balla Conte) na beki wa kati wa kulia (Frank Assink) ku-switch upande kwa kupiga pin points kwa winga wa kushoto (Ecua) kisha upande wa pili wa kulia kuzingirwa na wachezaji watatu mpaka wanne wa Yanga SC kuelekea back post ili kukamilisha shambulizi. Magoli ya Yanga SC yatafungwa sana back-post kama lile goli la Ecua. Huu ni mtego wao mpya.
“Bila mpira Yanga SC ya Folz inaweka sana pressure kwenye 4-1-4-1 na kurejesha umiliki haraka sana. Yes! Falz ball imeanza kuonekana ndani ya Tanzania,”.
Burudani zakutosha Kilele cha Wiki ya Mwananchi

Soma hii:Mkutano mkuu wa Yanga SC 2025: Mambo 10 yaliyotikisa ‘Super Dome’ leo
Katika tamasha la leo kulikuwa na burudani za kutosha. Msanii Zuchu alifanya kazi yake kubwa kwa ajili ya kunogesha shughuli kubwa. Katika kuimba na kucheza kulikuwa na shangwe kubwa mwanzo mwisho kwa mashabiki wengi ambao walijitokeza Uwanja wa Mkapa.
Hitimisho
Yanga SC 1-0 Bandari FC ya Kenya ni kengele kuelekea msimu mpya 2025/26. Baada ya tamasha la Wiki ya Mwananchi, Kariakoo Dabi inafuata. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 16 2025.


