- Wiki ya Mwananchi jiji la Dar litapambwa na rangi za njano na kijani kila kona ikiwa ni utambulisho wa Wanajangwani.
- Yanga Day tamasha bab kubwa Afrika ambalo ni maalumu kwa utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa kikosini 2024/25 linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa.
- Majina ya Balla Conte, Doumbia na Mohamed Hussen Zimbwe Jr yanatajwa kuwa kwenye orodha ya nyota wanaosubiriwa kutambulishwa mbele ya umati mkubwa.
Yanga Day Septemba 12 inasubirwa kwa shauku kubwa na mashabiki. Hili ni tamasha maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25. Kwenye tamasha hilo maalufu kama Wiki ya Mwananchi kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki Yanga SC vs Bandari.
Paisha kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda wakuvuna mamilioni ni sasa hivi kwa rubani bila matatizo yoyote. Ni rahisi sana cheza Aviator sasa upate mgao wako.

Yanga Day 2025 kuwa Ijumaa
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa wengi wanajiuliza kwa nini Yanga Day iwe ni Ijumaa? Kamwe aliongeza yote hayo yalitokana na ugumu wa ratiba. Kulikuwa na hatihati tamasha hilo lisifanyike.

“Ilikuwa ni kazi kubwa kupata ratiba hii ya Yanga Day Ijumaa kutokana na ratiba kuwa ngumu. Ilibaki kidogo tusiwe na tamasha hili. Ukweli ni kwamba haikuwa rahisi. Tumepata Ijumaa na tumefanya maandalizi mazuri hivyo mashabiki wawe tayari.
“Uwanja wa Mkapa wenyewe ni mashahidi kulikuwa na CHAN 2024. Mbali na hilo kulikuwa na maandalizi ya timu ya taifa kucheza mechi za Kombe la Dunia. Hapo unaona namna ratiba ilivyokuwa.”
Hapa tunakuletea orodha ya wachezaji wapya watakaotambulishwa Yanga SC
Andy Boyeli
Andy Boyeli ana miaka 24 ni mali mpya ndani ya Yanga SC. Mshambuliaji huyo alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 2025 alitambulishwa kuwa Mwanajangwani.
Lassine Kouma
Amekabidiwa jezi namba 8 iliyokuwa ni utambulisho wa Khalid Aucho raia wa Uganda. Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Kiungo huyu kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien. Anasubiriwa kutambulishwa Yanga Day, Wiki ya Mwananchi.

Soma hii: Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC
Balla Conte
Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.
Offen Chikola
Kiungo mshambuliaji Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo.
Casemiro
Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa katika wachezaji watakaotambulishwa Septemba 12 2025.
Ninju
Yanga Day itakuwa na beki chipukizi ambaye usajili wake ulikuwa na mvutano kati ya Azam FC ambao ni wamiliki na Yanga SC. Mwisho Yanga SC walikaa na Azam FC wakamaliza suala hilo. Ni Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Yanga SC Julai 27 2025.
Ecua Elastin
Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.
Doumbia
Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Staa huyo ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi kwa wengine.
Zimbwe Jr
Yanga SC ilimtambulisha Mohamed Hussen rasmi Agosti 6 2025 saa sita usiku baada ya tetesi kuwa nyingi. 2024/25 alikuwa katika kikosi cha Simba SC ambapo huko alikuwa ni nahodha. Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru.
Zimbwe Jr alitwaa tuzo ya beki bora msimu wa 2021/22. Ana tuzo ya MVP msimu wa 2016/17. Msimu wa 2023/24 alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu ni mchezaji bora ambaye atakuwa na uzi wa Yanga SC 2025/26.
Edmund John
Nyota huyu alitambulishwa Agosti 15 2025. Yanga SC ilimtambulisha Edmund John ambaye msimu wa 2024/25 alikuwa mali ya Singida Black Stars. Nyota huyo alitambulishwa kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Rayon Sports 1-3 Yanga SC. Kwenye mchezo huo Edmund alianzia benchi. Septemba 12 2025 anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa.
Assinki

Soma hii: Yanga SC yamsajili Frank Assinki kutoka Ghana kwa mkopo | Usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Yanga SC Agosti 21 2025 ilimtambulisha nyota mpya kuelekea msimu wa 2025/26 ambaye ni beki wa kati. Anaitwa Frank Assinki ambaye ni raia wa Ghana na msimu wa 2024/25 alikuwa ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.
Kauli mbiu ya Yanga Day 2025/26
Yanga SC kauli yao kuelekea msimu wa 2025/26 inakwenda kwa jina la Tunapiga Kichwani Tu. Kamwe aliweka wazi kuwa sababu ya kauli mbio hiyo ni kutaka kuongeza dozi tu. Msimu wa 2024/25 ilikuwa ni wewe haugopi?
Hitimisho
Yanga Day mbali na mchezo wa kirafiki wa kimataifa kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii. Zuchu anatarajiwa kuwa miongoni mwao watakuwa jukwaani. Meja Kunta, Dogo Paten nao wanatarajiwa kuwa kwenye tamasha hilo.


