Job- Injnia na BaccaJob- Injnia na Bacca
  • Mtambo wa mabao 18 kuendelea kukiwasha ndani ya Yanga SC dili likifia hatua nzuri.
  • Nahodha wa makombe kuna hatihati kuondoka ambapo matajiri wa Dar, Azam FC wanatajwa kuiwinda saini yake.
  • Mfungaji bora Muungano Cup 2025 kuna uwezekano akabaki Jangwani

MABOSI wa Yanga SC hawana utani kwa wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu wa 2024/25 wakiwa wameanza kufanya mazungumzo na wachezaji, uongozi wao ili kuboresha na kuongeza mikataba yao.

Hapa tunakuletea baadhi ya wachezaji wa Yanga SC ambao wanatajwa kuwa kwenye mazungumzo na mabosi wa timu hiyo kuongeza kandarasa zao kuelekea 2025/26 namna hii:-

Maxi Nzengeli

Kiungo huyu mshambuliaji wa Yanga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi anaingia kwenye orodha ya viungo ambao wanajua kufunga na kutengeneza nafasi za mabao ndani ya uwanja.

Maxi tuzo
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Kwenye msimu wa 2024/25 ni mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya kikosi cha Yanga ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika ilikuwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Ilikuwa ni Agosti 29 2024 ambapo alipachika bao hilo dakika ya 25 akitumia mguu wa kulia akiwa nje ya 18 zama za Miguel Gamondi. Kwenye mchezo huo Yanga ilikomba pointi tatu kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga SC. Bao la pili kwa Yanga lilifungwa na Clement Mzize.

Ukiweka kando kufunga bao la kwanza kwenye mchezo wa ligi, katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC alipachika bao moja ilikuwa dakika ya 44 akiwa ndani ya 18 Uwanja wa Mkapa.

Anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuongezewa mkataba mwingine kuendelea kutimiza majukumu ndani ya kikosi hicho ambacho kina taji la Muungano Cup 2025.

Kwenye Muungano Cup, Maxi alitwaa tuzo ya mfungaji bora alipomaliza mashindano akiwa na mabao mawili katika mabao hayo moja alifunga kwenye mchezo wa fainali dhidi ya JKU SC lililokuwa la ushindi.

Pacome Zouzoua

KIUNGO
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, 2024/25. Source: Yanga SC.

Mkali kwenye mguu wa kulia akiwa ndani ya uwanja, rai awa Ivory Coast, Pacome anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na mabosi wa Yanga SC ili kuongeza mkataba wake asalie Jangwani.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga SC wapo kwenye mazungumzo na Pacome ili kumuongezea mkataba mpya abaki ndani ya kikosi hicho kuendelea kutimiza majukumu yake.

Ndani ya ligi Pacome kahusika kwenye mabao 18 akiwa kafunga mabao 9 na kutoa pasi 9 za mabao msimu wa 2024/25 ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Rekodi zinaonyesha kuwa kakomba dakika 1,364 ndani ya uwanja kwenye mechi 23 ambazo alicheza alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Azam Complex kwenye Dar Dabi hali iliyomfanya awe nje kwa muda.

Yao Kouassi

Beki huyu wakupanda na kushuka amekuwa nje kwa muda akipambania hali yake jambo ambalo limefanya asiwe kwenye majukumu yake. Ni Kibwana Shomari, Israel Mwenda wamekuwa wakipishana upande ambao alikuwa anacheza mara kwa mara alipokuwa fiti.

Ni mechi 7 beki huyo kacheza kwa msimu wa 2024/25 akikomba dakika 538 mchezo wake wa mwisho kuonekana akiwa na uzi wa Yanga SC ilikuwa Desemba 19 2024, Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo alikomba dakika 90 na ubao ulisoma Yanga 3-2 Mashujaa FC baada ya hapo amekuwa nje kwa muda. Taratibu anazidi kurejea kwenye ubora ambapo inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga SC wanahitaji kumuongezea kandarasi nyingine azidi kuwa Jangwani.

Dickson Job

Job Dick ( )
Job Dick beki wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Source: Yanga SC.

Beki wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC, kandarasi yake inatarajiwa kugota mwisho msimu wa 2024/25. Alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotwaa Muungano Cup 2025 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU SC.

Ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga kwenye eneo la ulinzi ambapo kacheza jumla ya mechi 22 kati ya 26 zilizochezwa na vinara hao wa ligi wakiwa na pointi 70.

Katika mechi hizo 22 Job rekodi zinaonyesha kuwa kakomba dakika 1,912 uwanjani. Safu ya ulinzi ya Yanga SC ni namba mbili kwenye kufungwa mabao machache ambayo ni 10 namba moja kufungwa mabao machache ni Simba SC ikiwa imefungwa mabao 9 ndani ya ligi.

Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC inahitaji kuendelea kupata huduma ya Job ambaye aliibuka hapo akitokea kikosi cha Mtibwa Sugar ambayo imerejea kwa mara nyingine ndani ya ligi baada ya kushuka daraja na msimu wa 2024/25 ilikuwa inashiriki Championship.

Bakari Nondo

Nondo
Bakari Nondo beki wa Yanga SC 2024/25. Source: Yanga SC.

Beki huyu ambaye ni nahodha wa Yanga SC kuna hatihati akaondoka ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hajawa chaguo la kwanza huku mabosi wa Azam FC wakitajwa kuwa kwenye rada za kuwania saini yake.

Ni mechi 16 kacheza kakomba dakika 896, kwenye Muungano Cup 2025 wakati Yanga wakirejea na taji hilo alipewa nafasi kucheza.

Share this: