Mpanzu na KibuMpanzu na Kibu
  • Joto la Kariakoo Dabi linazidi kupanda kwa kasi kwa wababe wawili kuvuja jasho uwanjani.
  • Yanga SC vs Simba SC Septemba 16 kazi kubwa kufanyika uwanjani kwa wababe wawili kusaka taji.
  • Yanga SC waliwafunga Simba SC kwenye Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali 2024/25.

Yanga SC vs Simba SC wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa zimebaki siku 6 wababe hawa kukutana. Joto linazidi kupanda kila mmoja akivutia kwake. Ni mchezo wa kwanza unaoashiria kufunguliwa kwa pazia la LigI Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

Muda ni sasa ukiwa hewani unavuna mamilioni. Rahisa sana kwa rubani anayepaisha Kindege cha SportPesa. Cheza Aviator upate mgao wako.

image

Yanga SC vs Simba SC wanagombania taji gani?

Yanga SC vs Yanga SC
Ahmed Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC Septemba 16

Yanga SC na Simba SC wanagombania taji la kwanza uwanjani. Ni taji la Ngao ya Jamii (Community Shield). Baada ya dakika 90 atafahamika nani atakuwa mshindi wa taji hilo kwa msimu wa 2025/26.

Ipo wazi kwamba Yanga SC wanateta taji hilo ambalo walitwaa mwanzo wa msimu wa 2024/25. Katika fainali iliyochezwa Agosti 11 2024 Uwanja wa Mkapa walipata ushindi. Ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 4-1 Azam FC.

Fainali hiyo ilikusanya jumla ya magoli matano. Magoli manne kutoka Yanga SC. Goli moja kutoka kwa Azam FC.

Goli pekee la Azam FC lilifungwa na kiungo mshambuliaji Feisal Salum. Ni dakika ya 13 kiungo huyo mshambuliaji aliwanyanyua mashabiki wa Azam FC. Ni dakika tano pekee goli hilo lilidumu kwa kuwa Yanga SC walicharuka na kuweka mzani sawa kisha wakaongeza magoli manne yaliyowapa ushindi.

 Yanga SC ilikuwa inanolewa na Miguel Gamondi. Ni Prince Dube alianza kuweka usawa dakika ya 18, Chadrack Boka alifunga dakika ya 27, Aziz Ki dakika ya 30. Mshambuliaji Clement Mzize alifunga goli la nne dakika ya 90.

Yanga SC wakitwaa taji, Simba SC iliangukia nafasi ya tatu

Yanga Ngao
Yanga SC na taji la Ngao ya Jamii.

Soma hii: Yanga SC vs Simba sc, Juni 25 2025 kivumbi kitawaka

Wakati Yanga SC ikitwaa taji la kwanza, Simba SC iliangukia nafasi ya tatu. Ilianza msimu ikiwa haina taji tofauti na mpinzani wake. Nafasi ya pili ilikuwa mikononi mwa Azam FC na ile ya nne ilikuwa mikononi mwa Coastal Union.

Kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu bao pekee la ushindi kwa Simba SC lilifungwa na Saleh Karabaka. Dakika ya 10 Uwanja wa Mkapa bao hilo lilifungwa na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Ndani ya dakika 80 Coastal Union walikwama kupata bao mbele ya Simba SC.

Yanga SC waliifunga Simba SC Kariakoo Dabi

Msimu wa 2024/25 hauwa mzuri kwa Simba SC mbele ya Yanga SC. Mchezo wa kwanza walikutana katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii. Wababe hawa walikutana Agosti 8 2024.

Simba SC ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0. Matokeo hayo yaliwaondosha Simba SC kucheza fainali Ngao ya Jamii. Ni mshindi wa tatu ilikwenda kucheza Simba SC huku fainali ikiwa ni Yanga SC vs Azam FC.

Katika mchezo huo Simba SC ilipoteza dakika ikiwa imebaki. Ni dakika ya 44 goli hilo lilifungwa. Mfungaji alikuwa ni Maxi Nzengeli ambaye ni kiungo mshambuliaji.

Maxi Nzengeli neno lake kwa mashabiki

Maxi
Maxi kiungo mshambuliaji wa Yanga SC.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC Juni 25 2025 matukio makubwa mawili kufanyika

Kiungo Maxi Nzengeli amesema watapambana kupata matokeo mazuri. Nzengeli amesema wapo tayari kwa mapambano. Hivyo wataingia uwanjani kwa hesabu za kusaka ushindi.

“Kwa mashabiki ninawaambia kwamba tupo tayari kwa ushindani. Maandalizi ambayo tunafanya ni kwa ajili ya mech izote. Tupo tayari na tunaamini tutafanya vizuri mashabiki wawe pamoja nasi.”   

Huyu hapa Steven Mukwala wa Simba SC

Mshambuliaji wa Simba SC, Steven Mukwala amesema wamefanya maandalizi mazuri. Kambi ambayo walikuwa Misri wana imani itakuwa na matokeo mazuri. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.

“Tulikutana nao kwenye mechi iliyopita tukafungwa. Kwa sasa hatuna jambo la kuomba msamaha ambacho tunahitaji ni ushindi. Kambi yetu ya Misri ilikuwa nzuri hivyo tutafanya kazi kubwa kutafuta matokeo,”.  

Yanga vs Simba SC inapigwa mapema

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja pekee. Yote ni kufuatia mabadiliko ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji. Awali, mashindano haya yalikuwa yakihusisha nusu fainali mbili na kisha fainali.

Mabadiliko hayo yamesababishwa na ugumu wa ratiba, ikiwemo Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za CHAN zilizomalizika Agosti 30. Mara baada ya Ngao ya Jamii, vilabu vya Tanzania vitakuwa kazini kwa michezo ya raundi ya awali ya mashindano ya CAF.

 Hitimisho

Yanga vs Simba ni mechi kubwa Afrika. Uwepo wa wachezaji wapya unaongeza ushindani kwenye mchezo huu. Dakika 90 zitaamua nani atatwaa taji hilo.

image
Share this: