Clatous ChamaClatous Chama
  • Yanga SC vs Simba sc, Juni 25 2025 kivumbi kitawaka kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
  • Wachezaji hatari kutoka Yanga SC vs Simba SC wapo wengi wakiongozwa na kinara wa mabao Jean Ahoua na mkali wa pasi Pacome.
  • Simba SC 0-1 Yanga SC ni matokeo ya mzunguko wa kwanza mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Yanga SC vs Simba SC Juni 25 2025 kivumbi kitawaka Uwanja wa Mkapa. Ni mchezo wa mwisho kukamilisha msimu wa 2024/25. Timu zote mbili mechi zao zilizopita zilivuna pointi tatu muhimu.

Uwanja wa Mkapa
Uwanja wa Mkapa sehemu ya kazi Juni 25 2025.

Soma hii: Mechi namba 184 Yanga SC vs Simba SC ni pasua kichwa

Yanga SC ilivuna pointi tatu kwa ushindi wa mabao 5-0 Dodoma Jiji. Simba SC ilipata ushindi wa bao 1-0 Kagera Sugar. Juni 25 2025 mwisho wa ubishi kwa wababe hawa wawili kuvuja jasho.

Yanga SC kwenye msimamo ni nafasi ya kwanza pointi 79 baada ya kucheza mechi 29. Tofauti yao na Simba SC ni pointi moja. Simba SC ina pointi 78 kwenye msimamo ikiwa nafasi ya pili.

Hapa tunakuletea wachezaji wenye hatari ndani ya uwanja. Ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Simba SC 0-1 Yanga SC ilikuwa baada ya dakika 90. Uwezo wao kwenye kufunga ama kutengeneza nafasi za mabao ni mkubwa ikiwa ni baadhi namna hii:-

Clement Mzize wa Yanga SC

Mzize Clement (-)
Mzize Clement mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC ni Juni 25 2025 sio Juni 15 2025

Clement Mzize mechi mbili mfululizo amekuwa akitoa pasi za mabao. Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Juni 18 2025 na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Juni 22 2025. Pasi zote za mabao alimpa kiungo mshambuliaji Clatous Chama.

 Mzize kafunga mabao 13 ndani ya Yanga SC kati ya mabao 81. Ni pasi tano ametoa akihusika kwenye jumla ya mabao 18. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia.

Pacome Zouzoua wa Yanga SC

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua ni mchezaji mwenye hatari. Kasi yake kwenye kufunga na kuwa na jicho lakuona hatari ni kubwa. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao mawili Juni 18 2025 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Pacome Z (-)
Pacome kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Pacome kibindoni ana mabao 11 na kutoa pasi 9 za mabao hivyo kahusika kwenye mabao 20 kati ya 81 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza ligi kwa msimu wa 2024/25.

Prince Dube hatihati kuikosa Kariakoo Dabi

Prince Dube mwenye mabao 13 na pasi 8 za mabao kuna hatihati akakosekana kwenye Kariakoo Dabi. Dube alipata maumivu mchezo dhidi ya Tanzania Prisons. Kwenye mchezo huo alitumia dakika 22 nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama.

Maxi Nzengeli wa Yanga SC

Mfungaji wa bao la kwanza kwenye ligi ndani ya Yanga SC ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar. Katika mchezo wa raundi ya 30 alifunga bao moja dhidi ya Dodoma Jiji. Mguu wake wa kulia una balaa kubwa ni miongoni mwa wachezaji wenye hatari anajua kufunga na kutoa pasi za mabao.

Clatous Chama wa Yanga SC

Chama Jr
Chama Jr kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alianzia benchi na alipoingia alifunga. Mchezo dhidi ya Dodoma Jiji alianza kikosi cha kwanza na alifunga. Anakumbukwa mzunguko wa pili Kariakoo Dabi alianzia benchi alipoingia pigo lake la faulo likabadili upepo.

Shomari Kapombe wa Simba SC

Kapombe
Kapombe Shomari beki wa Simba SC. Source: Simba SC.

Beki wakupanda na kushuka, amekuwa na hatari kwenye kusababisha penati ndani ya uwanja. Mchezo dhidi ya JKT Tanzania dakika ya 90 alichezewa faulo ndani ya 18. Faulo hiyo ilileta penati iliyofungwa na Ahoua.

Steven Mukwala wa Simba

Mguu wa kulia wa Mukwala wa Simba SC una hatari kubwa. Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar dakika ya 17 alifunga bao la ushindi. Pasi ya Duchu aliitumia vizuri akiwa ndani ya 18, Uwanja wa KMC Complex.

Nyota huyo mbali na kufunga anajua kutengeneza pasi za mabao. Ni pasi tatu za mabao katengeneza akiwa amefunga jumla ya mabao 13 hivyo kahusika kwenye mabao 16 ya Simba SC iliyofunga mabao 69 baada ya mechi 29.

Jean Ahoua wa Simba SC

Mukwala na Ahoua
Mukwala na Ahoua nyota wa Simba SC. Source: Simba SC.

Hatari yake ni kwenye mguu wa kulia ndani ya uwanja. Kahusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili. Alianza kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Ahoua kafunga mabao 15 akitumia mguu wa kulia. Kafunga bao moja kwa pigo la kichwa ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu. Kwenye mchezo huo Ahoua alifunga hat trick yake ya kwanza.

 Ellie Mpanzu wa Simba SC.

Maandalizi ya kazi ya kesho- #NguvuMoja
Mpanzu nyota wa Simba SC. Source: Simba SC.

Ellie Mpanzu mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Kwenye mchezo dhidi ya KenGold alifunga bao moja akiwa nje ya 18 na alitoa pasi kwa Leonel Ateba. Mpanzu alipachika bao dakika ya 22 akiwa nje ya 18.

Ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo kwenye mechi kubwa. Hatari yake akiwa nje ya 18 ama ndani ya 18 katika kufanya maamuzi. Hakuanza kikosi cha kwanza dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wote wa Yanga SC na Simba SC wanahatari wakiwa uwanjani. Hakuna ambaye anatabirika kutokana na aina ya mchezo husika. Inawezekana wale waliotajwa wakaanza kikosi cha kwanza Juni 25 2025 ama kuanzia benchi kulingana na mipango ya timu itakavyokuwa.

Share this: